Niulize chochote kuhusu injini za magari madogo na pickup zinazotumia Petroli

Niulize chochote kuhusu injini za magari madogo na pickup zinazotumia Petroli

Kiongozi Prado kula mafuta yenye injini ya 3rz, inakula wastani wa lita 5 kwa hapa mjini dar, je ni sawa au kuna shida?

NB : nimebadilisha injection na fuel pump lakini bado haijabadili ulaji

Sent using Jamii Forums mobile app
Hapo kidogo hujaeleweka ...nadhani ulitaka kumaanisha prado yenye injini ya 3rz kula mafula lita 1 kwa km 5 kwa mji wa dar...

Labda nijibu hivi na wengine wataongezea...

Hiyo injini ni 2.7 L electronic fuel injection...ambayo ina kawaida ya kula mafuta lita 15 kwa km 100 kama unae desha mjini....hapa ina maana kila lita moja itakupa km 6.6 kwa foleni za Dar...

Sasa kama yako imeshuka kutoka 6.6 mpaka km 5 kwa lita ni dhahiri kuwa ni ulaji wa kawaida kwa ukubwa wa injini ukilinganisha na foleni za Dar.. japo uchakavu wa injini unaweza kuchangia kuongezeka kwa ulaji wa mafuta. ...

Jaribu kukagua air filter yako na spark plugs...weka zike genuine DENSO, NGK au BOSCH ziwe iridium zile zenye ncha nyembamba maarufu kama plug za sindano....bei yake imechangamka sana.....pia fuel filter angalia ina hali gani..
Pia amnagalia aina ya injini oil unayotumia..
Recommended SAE VISCOSITY ya hiyo injini ni 5w 30, 10w 30 ndiyo utafurahia...ukitumia SAE 40 unaweza kukutana na matatizo kama hayo ya kushuka uwezo wa kubana mafuta..

Ukizingatia hayo unaweza kupandisha hicho kiwango angalau ukapata km 5.8 kwa lita....si rahisi kupata 6.6 kwa sababu kumbuka injini itakuwa na miaka zaidi ya 10...
Hizo injini zilisitishwa production yake mwaka 2004.

Hugh way unaweza kupata mpaka km 11 kwa lita kwani ina uwezo wa kula lita 9 kwa km 100..

Wataalamu zaidi wataongezea...


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Boeing 747, Sae 40 ni oil mahususi kwa ajili ya caterpillars, generator na machine za viwandani na ndo maana hata bei yake ni ndogo na zimebaki kampuni chache sana zinazozalisha oil hii
 
Toyota RAV4 2006 model DBA-ACA36W AWD engine inakula oil na hamna sehemu inavuja. Approximately 500-800km unakuta imepungua kiasi flani. Tatizo litakua nini na solution ni nini?
Pole mkuu...
Mwaenye uzi nadhani amepata dharura kidogo...ila naimani akija atajibu maswali yote vizur..

Lakini na mimi nijibu hivi..

Je, unapata moshi wa blue kwenye gari yako...?
Kama ndiyo, gari yako itakuwa inaunguza oil...

Je, rangi za Spark plugs zako zikoje..?
Kama zimejaa ukurutu mweusi( oily deposit.). ni wazi kwamba gari lako linaunguza oil...

Sababu kuu za gari kuunguza oil ni
1.Uchakavu wa piston rings...hapa gari litapoteza uwezo wa compression na kiasi cha oil kitapenya kwenye kuta za cylinders kupitia piston rings na kuunguzwa kwenye combustion chamber..

Suluhisho...tafuta fundi mzuri akague rings kama zimechoka uweke mpya, tatizo litakwisha.

2. Uchakavu wa valve guide na seals za intake valves...hivi kama vimechoka au seals kama zimekatika, oil itakuwa inafyonzwa kwenye combustion chamber wakati wa kitendo cha intake kinapofanyika...
Suluhisho ni kutafuta fundi mzuri akague na kubadili seals zilizochoka..

*3........Sababu ya tatu ambayo si rasmi inayozungumzwa mitaani ni aina ya oil unayotumia....inasemekana kuna oil fake ambazo zikipata joto kali sana zina evaporate hivyo kufanya kiasi cha oil kupungua....hii ni MYTHS lakini huenda ina ukweli....tuepuke cheap oils..

HITIMISHO....
Kama umejiridhisha vya kutosha kuwa hakuna sehemu yoyote oil inapovuja, ( make sure that no any external leakage of oil) , pia kama unatumia oil zenye viwango vizuri kutoka kampuni zinazoamika, basi wazi kuwa gari lako linakabiliwa na tatizo namba 1 au 2 au zote 1 na 2....

Tafuta fundi mzuri anayejua weledi wa kazi yake akukagulie kwa sababu hayo matatizo yanahusika na sehemu nyeti za injini yako....epukana na fundi mwenye papara kwenye ufunguaji wa engine.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Boeing 747,
Asante kwa majibu.
1. Moshi unaotoka ni mweupe tu ile asubuhi gari likiwashwa.
2. Nishabadili plug mara kadhaa, na nilikuta zina utando mweusi nikabadili ile seal kwenye top engine...

Kwa ushauri wako huu ishu itakua kwenye 1 na 2 hapo. Nitatafuta fundi mzuri aicheki vyema..

asante sana.
 
Wakuu nnakigari changu Aina ya Verrosa , Kuna muda inakosa nguvu kabisa, Sasa wataalam wakanishauri nibadili gear box, nikabadili lakini bado tatizo Hilo naliona bado linarejea.
Ushauri wazee

Sent using Jamii Forums mobile app
Yan mkuu verrosa unaiita kigari? Sisi wenye vibaby walker tusemeje.......
 
Habari za asubuhi wana Jamii Forum,

Naombeni msaada wa haraka kidogo, nina gari aina ya Suzuki Wagon R+ ina tatizo la kukata moto wakati nipo kwenye mwendo ila ndani ya dakika 1, 2, unawasha tena na kuondoka , na ilikuwa na tatizo la kumiss lakini nilipeleka kwa fundi na kurekebishwa (nilibadili fuel pump, fuel filter, kusafisha kabureta, kupuliza air cleaner ) na miss haikuondoka na baada ya hapo tukagundua ilikuwa ni ignition coil na nyaya zake , baada ya kubadili gari ilikuwa poa.

Ndio sasa limekuja hilo tatizo la kufifia kwenye mwendo na kutaka moto.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
mkuu kichuguu nina tatizo toyota ist nikiwasha gari asubuhi kuna mlio unagonga ist ya mwaka 2003 nilishawahi kubadili gasket fundi aligundua oil inavuja kwani ilikuwa inapungua mara kwa mara nimepata hofu itanihitaji kubadili engine nyingine naomba unitumie namba yako Mr kichuguu
 
Nimenunua gar, huu uzi nilikuwa siufatilii sasa lasm naanza kuuchungulia naweza pata ufumbuz wa matatizo nitakayokutano nayo kwenye ndinga yangu


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Kwa kawaida hakuna tatizo lolote kwa gari kwenda umbali mrefu bila kusimama iwapo ina maji ya kutosha na oil haijachoka. Ule muda unaosimama kwenda uwani, kula na kuongeza mafuta hutosha sana kupumzisha injini ya gari lako, siyo lazima ipoe.
Ahsante sana kichuguu kwa maelezo yako hakika umesaidia wengi ila swali langu ni moja tu, hivi kwenye radiator tunatakiwa kuweka maji au coolant/ antfreez wanayouza madukani? naomba msaada wako tafadhari.
 
Tumia anti-freeze; usiweke maji kwenye injini yako. Faida za Antifreeze ni hizi.

(1) Maji yale yana madawa ya kuzuia kutu kwenye radiator.
(2) Maji yale yana madawa yanayosaidia maji yazunguke kwa urahisi ndani ya injini (viscosity yake ni ndogo sana kuliko maji ya kawaida)
(3) Maji yale hayageuki kuwa mvuke kwa haraka, yanahimili hadi zaidi ya digrii 100 kabla hayajawa mvuke. Hiyo ni salama sana kwa injini yako kwani maji ya kawaida yanageuka mvuke haraka sana yakishafika digrii 100, na kusababisha injini yako iwe na mvuke tu badala ya kuwa na maji ya kupooza.
 
Back
Top Bottom