Kichuguu
Platinum Member
- Oct 11, 2006
- 17,048
- 22,790
- Thread starter
-
- #821
Hello.
Mm sio fundi ila pia
Nimepitia tatizo kama lako na gari imepona...
Kuharibikia kwa Knock sensor hakusababisihi transmission ishindwe; kwa hiyo ile knock sensor haikuwa tatizo lenyewe ingawa ni vizuri liligundulika na kutatatuliwa. Tatizo kubwa sana nadhani ni hiyo EMU; magari ya kati ya mwaka 2000 had 2010 yalikuwa computer tatu hivi: ile ya injini , ya transmission, na ya airbags . Kwa kawaida ECU huwa hazifi kirahisi sana ndiyo maana siyo jambo linaloongelewa sana na mafundi; kwa sababu wanategemea hizo computers kufanya diagnosis. Kwa RAV4 kufa computer ya transmission ilikuwa ni makosa ya kifundi huko Toyota katika kudesign magari yale.
Haya matatizo yanayotokana na design mbovu huwa yanarekebishwa na mtengezaji mwenyewe (Recall). Baada ya kusoma post yako, nimepitia data bases za recalls, na kweli inaonyesha kuwa Rav 4 zote za kuanzia mwaka 2000 hadi 2003 zililikuwa na matatizo hayo ya computer ya transmission, na mwaka 2006 Toyota ilifanya recalls za magari hayo ili kubadilisha computer hiyo ya Transmission.
Hata hivyo, ndiyo hivyo tena, siyo watu wote waliokuwa na RAV4 hizo waliitikia mwito, ndiyo maana yanakuja kujitokeza baadaye. Sijui kama tatizo kwenye zile computer lilikuwa ni programming au ni unit yote (hardware) ndiyo ilikuwa mbovu. Nikipata nafasi nitatafuta kwenye records za Toyota niangalie kama walikuwa wanabadili computer yote au walikuwa wanaiprogram upya. Kama tatizo lilikuwa ni hardware lakini wewe umeflush program tu, tatizo linaweza kurudi huko mbeleni, na kama tatizo lilikuwa ni program tu, basi hongera sana na pole kwa kuhangaika vile.