Niulize chochote kuhusu injini za magari madogo na pickup zinazotumia Petroli

Niulize chochote kuhusu injini za magari madogo na pickup zinazotumia Petroli

Hello.
Mm sio fundi ila pia
Nimepitia tatizo kama lako na gari imepona...

Kuharibikia kwa Knock sensor hakusababisihi transmission ishindwe; kwa hiyo ile knock sensor haikuwa tatizo lenyewe ingawa ni vizuri liligundulika na kutatatuliwa. Tatizo kubwa sana nadhani ni hiyo EMU; magari ya kati ya mwaka 2000 had 2010 yalikuwa computer tatu hivi: ile ya injini , ya transmission, na ya airbags . Kwa kawaida ECU huwa hazifi kirahisi sana ndiyo maana siyo jambo linaloongelewa sana na mafundi; kwa sababu wanategemea hizo computers kufanya diagnosis. Kwa RAV4 kufa computer ya transmission ilikuwa ni makosa ya kifundi huko Toyota katika kudesign magari yale.

Haya matatizo yanayotokana na design mbovu huwa yanarekebishwa na mtengezaji mwenyewe (Recall). Baada ya kusoma post yako, nimepitia data bases za recalls, na kweli inaonyesha kuwa Rav 4 zote za kuanzia mwaka 2000 hadi 2003 zililikuwa na matatizo hayo ya computer ya transmission, na mwaka 2006 Toyota ilifanya recalls za magari hayo ili kubadilisha computer hiyo ya Transmission.

Hata hivyo, ndiyo hivyo tena, siyo watu wote waliokuwa na RAV4 hizo waliitikia mwito, ndiyo maana yanakuja kujitokeza baadaye. Sijui kama tatizo kwenye zile computer lilikuwa ni programming au ni unit yote (hardware) ndiyo ilikuwa mbovu. Nikipata nafasi nitatafuta kwenye records za Toyota niangalie kama walikuwa wanabadili computer yote au walikuwa wanaiprogram upya. Kama tatizo lilikuwa ni hardware lakini wewe umeflush program tu, tatizo linaweza kurudi huko mbeleni, na kama tatizo lilikuwa ni program tu, basi hongera sana na pole kwa kuhangaika vile.
 
Habari mkuu,
Nilifanya diagnosis kuhusu gari yangu kuwa speed ndogo na odometer kusoma speed kuwa let's say unaona kabisa upo 70km/hr ila odometer itasoma 95 - 100km/hr.

Mtu wa diagnosis akaniambia strainer na "Knock sensor bank 1" ndio zina shida, je nikibadilisha gari yangu itakuwa poa? Maana hata kubadili gear haipo Safi kuna muda inaishia gear namba 3, gari yangu ni Rav4 kilitime automatic transmission.
Wala usiende mbali kihivyo !
Wrong speed readings kwa kiasi kikubwa inachangiwa na wrong tyre size ,which turns to wrong diff ratio, that ratio imekuwa precisely calculated na engine power capacity ,
Kubadilisha sensor hakutakusaidia, Sana Sana utapata speed readings sawa Ila engine bado ita struggle kubeba mzigo .

Una option mbili hapo , zote Ni costly though! Moja ubadilishe tairi zote ili upate ratio sahihi ya diff , opt ya pili Ni kubadilisha diff yenyewe

Sent
 
Wala usiende mbali kihivyo !
Wrong speed readings kwa kiasi kikubwa inachangiwa na wrong tyre size ,which turns to wrong diff ratio, that ratio imekuwa precisely calculated na engine power capacity ,
Kubadilisha sensor hakutakusaidia, Sana Sana utapata speed readings sawa Ila engine bado ita struggle kubeba mzigo .

Una option mbili hapo , zote Ni costly though! Moja ubadilishe tairi zote ili upate ratio sahihi ya diff , opt ya pili Ni kubadilisha diff yenyewe

Sent
Nashukuru mkubwa nitafanyia kazi ushauri wako, nione itakuwa vipi.!

Sent from my STK-L21 using JamiiForums mobile app
 
Usishangae kuhusu utambulisho huu. Mimi sasa ni ASE Certified Service Consultant wa magari madogo yanayotumia petroli hasa ya Ford, GM, na Chrysler.

Nimepata license yangu hivi majuzi tu mwaka huu baada ya kuitafuta kwa muda kidogo through part-time activities kwani hiyo siyo kazi yangu kuu.

Certification hiyo inahitaji siyo tu kufaulu mtihani wake, lakini pia uwe na uzoefu wa kutosha kwenye auto-repair shop.

Nimekamilisha experience hiyo inayotakiwa mwaka huu na kupata license yangu.

Kwa vile injini nyingi za petroli zinafanana katika utendaji, jisikie free kuniuliza swali lolote kuhusu matatizo ya injini ya gari yako model yoyote inayotumia mafuta ya petroli.

Siahidi kuwa majibu yangu yote yatakuwa ni sahihi, lakini sehemu kubwa itakuwa ni sahihi, na hata yale ambayo hayatakuwa sahihi yanaweza kukusadia kujua wapi pa kuanzia.

Mkuu Kichuguu Habari. Kuna gari yangu ya Toyota (Saloon) imeanza matatizo ya Clutch kutokupeleka mafuta vizuri kila baada ya Tuta au inapopanda mlima hivyo kusababisha gari kutokuwa na nguvu. Mafundi waliosha Nozzles kwa Tina na kukagua Plugs, Pump ya mafuta, Enjector na mkaa unaoshika nozzle ambapo gari ilirudia nguvu zake kwa alau kwa 70%.

Gari imetembea kwa siku kadhaa na ghalfa jioni moja taa ya check Engine ikaanza kuwaka na kufanya nguvu za gari kupungua sana (Unakanyaga mafuta ila gari inatembea taratibu tu). Baadhi ya wataalamu wamenishauri niangalie gearbox kwani yamkini gari inachelewa kubadili gear toka namba 2 kwenda 3. Mkuu unadhani nini tatizo la hili gari ikizingatia kwamba mafuta yanapoenda vizuri Engine ina nguvu sana??



Ahsante
 
Mkuu Kichuguu Habari. Kuna gari yangu ya Toyota (Saloon) imeanza matatizo ya Clutch kutokupeleka mafuta vizuri kila baada ya Tuta au inapopanda mlima hivyo kusababisha gari kutokuwa na nguvu. Mafundi waliosha Nozzles kwa Tina na kukagua Plugs, Pump ya mafuta, Enjector na mkaa unaoshika nozzle ambapo gari ilirudia nguvu zake kwa alau kwa 70%...
Toyota Model gani na ya mwaka gani
 
Mbona dip stick ya Brevis imeandikwa nisibadilishe ATF
Ni kweli kuwa magari mengi wanadai ATF ni lifetime, lakini ukweli siyo huo, wanachokuzuia to ni kuwa usimwage yote bali uwe unaongezea kidogo kidgo kadri level invyopungua kulingana na dipistick yako; na wanachukulia kuwa gari ikifika umri fulani inakuwa haitembei tena. Ushauri wa mafundi wengi unaonyesha kuwa hakuna ATF ambayo inadumu lifetime, hasa kwa vile watu wengi huendesha magari yao kwa muda mrefu zaidi ya umri ambao watengenezaji walitegemea.

Na hivyo ATF nayo hupungukiwa nguvu kutokana na joto na gearbox la mara kwa mara na baada ya muda fulani inakuwa haifanyi kazi kama mwanzo.

Kuna vikaratsi fulani (kama litmus paper) vya kutestia ATF kulingana vinavyobadili rangi. Vikibadilika rangi kufikia kiasi fulani basi utalazimika kumwaga hiyo ATF hata kama mtengezaji alisema usimwage.

Angalia hapa

Automatic Transmission Fluid Diag. Pads | OTC Tools
 
Asante kwa taarifa
Ni kweli kuwa magari mengi wanadai ATF ni lifetime, lakini ukweli siyo huo, wanachokuzuia to ni kuwa usimwage yote bali uwe unaongezea kidogo kidgo kadri level invyopungua kulingana na dipistick yako; na wanachukulia kuwa gari ikifika umri fulani inakuwa haitembei tena. Ushauri wa mafundi wengi unaonyesha kuwa hakuna ATF ambayo inadumu lifetime, hasa kwa vile watu wengi huendesha magari yao kwa muda mrefu zaidi ya umri ambao watengenezaji walitegemea, na hivyo ATF nayo hupungukiwa nguvu kutokana na joto na gearbox la mara kwa mara na baada ya muda fulani inakuwa haifanyi kazi kama mwanzo. Kuna vikaratsi fulani (kama litmus paper) vya kutestia ATF kulingana vinavyobadili rangi. Vikibadilika rangi kufikia kiasi fulani basi utalazimika kumwaga hiyo ATF hata kama mtengezaji alisema usimwage.

Angalia hapa

Automatic Transmission Fluid Diag. Pads | OTC Tools
 
Mkuuu naomba msaada katika hili

Swali la ufahamu.Nina Harrier old model nimelinunua kwa mtu. Nimekaa nalo miaka miwili. Lina tatizo la kukata stabilizer bar nimeshabadilisha zaidi ya 5. Nini inaweza kuwa sababu?
 
Mkuuu naomba msaada katika hili

Swali la ufahamu.Nina Harrier old model nimelinunua kwa mtu. Nimekaa nalo miaka miwili. Lina tatizo la kukata stabilizer bar nimeshabadilisha zaidi ya 5. Nini inaweza kuwa sababu?
Za mbele au za nyuma
 
Za mbele mkuu
Nadhani shock absorber unazotumia ni za saizi ndogo kulingana na uzito wa gari lako hasa mbele huwa ni kuzito zaidi ya nyuma kwa sababu ya injini.

Au unatumia shocksober za aina mbili tofauti, ile ya kushoto siyo sawa na ile ya kulia. Sababu ya pili inaweza kuwa una wheel alignment mbaya kwa hiyo unapoenedsha magurudumu ya mbele yanakuwa kama yanavutana, ila hilo utalijua haraka kwa kuona matairi ya mbele yanaliwa upande mmoja haraka sana.

Stabilizer inaweza kufanya kazi zaid ya miaka kumi bila kuwa na madhara yoyote iwapo unahakikisha kuwa una shock absrober za saizi ya gari. Ubovu ni kuwa wakati mwingine wafanya biashara wanatuletea bidhaa duni.

Check shock absorber tu.
 
Nadhani shock absorber unazotumia ni za saizi ndogo kulingana na uzito wa gari lako hasa mbele huwa ni kuzito zaidi ya nyuma kwa sababu ya injini. Au unatumia shocksober za aina mbili tofauti, ile ya kushoto siyo sawa na ile ya kulia. Sababu ya pili inaweza kuwa una wheel alignment mbaya kwa hiyo unapoenedsha magurudumu ya mbele yanakuwa kama yanavutana, ila hilo utalijua haraka kwa kuona matairi ya mbele yanaliwa upande mmoja haraka sana. Stabilizer inaweza kufanya kazi zaid ya miaka kumi bila kuwa na madhara yoyote iwapo unahakikisha kuwa una shock absrober za saizi ya gari. Ubovu ni kuwa wakati mwingine wafanya biashara wanatuletea bidhaa duni.

Check shock absorber tu.
Mkuuu ubarikiwe sana
 
Mkuu habari samahani gari bibi mkubwa inasumbua sana ni RAVA 4 KILL TIME ukiiwasha tu inaanza kugonga kwenye injini injini ikikaaa kama daki 7 hivi inatualia inaacha kugonga fundi kahangaika kufungua sampu kasafisha lakini bado tu, kanishauri kubadili vitu vingi mpk nimemuona kam anabahatisha
 
Mkuu habari samahani gari bibi mkubwa inasumbua sana ni RAVA 4 KILL TIME ukiiwasha tu inaanza kugonga kwenye injini injini ikikaaa kama daki 7 hivi inatualia inaacha kugonga fundi kahangaika kufungua sampu kasafisha lakini bado tu, kanishauri kubadili vitu vingi mpk nimemuona kam anabahatisha
RAV4 za mwaka 2000 mpaka 2003 zilikuwa na matatizo ya computer ya Transmission; angalia kama hilo lilishughulikiwa. Ila kugonga kelele sana wakati wa kustart inawezekena timing belt au timing chain imeanza kulegea.
 
RAV4 za mwaka 2000 mpaka 2003 zilikuwa na matatizo ya computer ya Transmission; angalia kama hilo lilishughulikiwa. Ila kugonga kelele sana wakati wa kustart inawezekena timing belt au timing chain imeanza kulegea.
Mkuuu nashukuru sana

sent from HUAWEI
 
Back
Top Bottom