Niulize chochote kuhusu injini za magari madogo na pickup zinazotumia Petroli

Niulize chochote kuhusu injini za magari madogo na pickup zinazotumia Petroli

Mkuu habri ya asubuhi . Naomba kuuliza hiv gar linapopungua oil kwenye gia box inaweza ikasababisha gar kutetemeka saingine kuzima au kuwasha taa ya check ingine?... Na tatizo la oil kupungua kwenye gear box sababu inaweza kuwa ni nini
 
Oxygen sensor na spark plugs hazikuwa na umuhimu wa kubadili labda kama kulikuwa na dalili nyingine lakini siyo hiyo ya coolant kuisha haraka. Jibu kamili la kukusaidia linahitaji ukaguzi wa sehemu kadhaa za injini yako. (1) Clynider head gasket umesema umebadili, hilo linaweza kuwa ni jambo jema kwa sababu cylinder ghead gasket husabaisha maji yavunje na kuingia kwenye cylinder, jambo ambalo siyo zuri kwa uhai wa injini..
Engine Oil nilibadili jana. Tena ikiwa imetembea km 650 tu toka nibadili mara ya mwisho.

Radiator ilisafishwa na maji ya presha kabla sijaweka ile top cover. Ila kama inavuja ndo sijafahamu hilo.
 
Msaada Tafadhali
Gari Yangu Ina tatzo
Nilikua nimeipaki karbia sku tatu sasa wakati naitoa ile naingia barabaran ilitoa wimbi moja la Moshi balaa (mweupe) kwa sababu ilikua jion skuweza kufanya chochote ...kesho yake nikalitumia Moshi uliendelea kutoka lakin badae ulikata.

Baada ya siku mbili Moshi vile vile wingu la moshi..! Nikabadili oil Moshi ukaendelea kutoka kidogo badae ukakata fundi akasema imekula ringi hlo sikutaka kulipa uzto.! ila gari Yangu ilikua na shida ya pump ya mafuta je inaweza kua tatzo?
 
Engine Oil nilibadili jana. Tena ikiwa imetembea km 650 tu toka nibadili mara ya mwisho.

Radiator ilisafishwa na maji ya presha kabla sijaweka ile top cover. Ila kama inavuja ndo sijafahamu hilo.
Basi angalia water pump.
 
Gari yangu nikiwa nashuka mteremko kwa speed hata nikifika eneo ambalo gari inaanza kupunguza mwendo cha ajabu rpm inabaki juu na engine unaisikia kabisa ina rev. Inakaa kidogo then inashuka normal.
 
Gari yangu nikiwa nashuka mteremko kwa speed hata nikifika eneo ambalo gari inaanza kupunguza mwendo cha ajabu rpm inabaki juu na engine unaisikia kabisa ina rev. Inakaa kidogo then inashuka normal.
Inawezekana oil yako imechoka; kagua oil halafu ikiwezekana uibadilishe. Vile vile inawezekana throttle yako ina uchafu; kuna mafuta ya kusafishia throttle.
 
Inawezekana oil yako imechoka; kagua oil halafu ikiwezekana uibadilishe. Vile vile inawezekana throttle yako ina uchafu; kuna mafuta ya kusafishia throttle.
Oil haina shida. Nitajaribu hiyo throttle
 
Niliona mahali kwamba kwa Suzuki Escudo 2.0 ya mwaka 2006, recommended Engine oil ni 5w 30. Ila katika pitapita zangu kwenye vituo vya Total nikagundua siku za karibuni wanaketa 5w 40 na hakuna kabisa 5w 30.

Hili likanifanya nizame google kucheki kama itanifaa. Nikakutana na article mahali ambayo pengine ilinifungua macho kuhusu tofauti ya hizi oil mbili. Pia ikanieleza jambo kuwa pengine 5W 40 ni nzuri zaidi huku kwetu ambako joto linazidi nyuzi 25 wakati mwingi. Naambatanisha link ya hilo andiko

Nini Ushauri na maoni yako??

5w30 vs 5w40: Which Oil is the Best| Difference between 5w30 and 5w40 |
 
Niliona mahali kwamba kwa Suzuki Escudo 2.0 ya mwaka 2006, recommended Engine oil ni 5w 30. Ila katika pitapita zangu kwenye vituo vya Total nikagundua siku za karibuni wanaketa 5w 40 na hakuna kabisa 5w 30. Hili likanifanya nizame google kucheki kama itanifaa. Nikakutana na article mahali ambayo pengine ilinifungua macho kuhusu tofauti ya hizi oil mbili. Pia ikanieleza jambo kuwa pengine 5W 40 ni nzuri zaidi huku kwetu ambako joto linazidi nyuzi 25 wakati mwingi. Naambatanisha link ya hilo andiko
Nini Ushauri na maoni yako??

5w30 vs 5w40: Which Oil is the Best| Difference between 5w30 and 5w40 |
Ni kweli nusususu lakini siyo kweli kamili. Ni kwamba kuanzia oili namba 40 na zaidi ni nzito sana na ni kwa magari makuukuu ambayo yameshakula sana pistons rings , main bearings, con-bearings pamoja na valve seaters, kwa hiyo oili nzito ya 40 na zaidi inakuwa inaziba vizuri mapengo yaliyokwisha jitokeza. Kama gari lako linatumia hydraulic valve lifter, hayo yanaweza kuziba matundu yake haraka sana kwa sababu ya uzito wake ukaanza kupata matatizo mengine ya gari kuanza kuwa na miss zisizokuwa za lazima.

Watu wanaposema nchi za joto, sijui huwa wana maana joto gani; hata kukiwa na joto sana nje, haliwezi kufika digrii 50 lakini injini inafanya kazi kwa joto la kuanzia digrii 90 mpaka kama 110 tu hivi. Utaona kuwa joto la injini tayari ni kubwa kuliko joto la nje.

Tunaofanyia nchi za baridi huwa tunakuwa na summer za joto kubwa sana kuliko hata Dar es Salaam lakini bado tunatumia hizo 40 kwa tahadhari sana hasa baada ya compression test kuonyesha kuwa injini imeanza kupunguza pressure. Ukimwekea mtu oil namba 40 hata wakati wa summer atalalamika gari linaunguruma vibaya baada ya matengezo.
 
Niliona mahali kwamba kwa Suzuki Escudo 2.0 ya mwaka 2006, recommended Engine oil ni 5w 30. Ila katika pitapita zangu kwenye vituo vya Total nikagundua siku za karibuni wanaketa 5w 40 na hakuna kabisa 5w 30. Hili likanifanya nizame google kucheki kama itanifaa. Nikakutana na article mahali ambayo pengine ilinifungua macho kuhusu tofauti ya hizi oil mbili. Pia ikanieleza jambo kuwa pengine 5W 40 ni nzuri zaidi huku kwetu ambako joto linazidi nyuzi 25 wakati mwingi. Naambatanisha link ya hilo andiko
Nini Ushauri na maoni yako??

5w30 vs 5w40: Which Oil is the Best| Difference between 5w30 and 5w40 |
Pamoja na maelezo mazuri ya link uliotuambatanishia mwisho wa siku ujumbe wa maana kwa ajili ya gari yako uko pale kwenye neno conclusion ambapo amesema "unatakakiwa/ kushauriwa kutumia oil ambayo watengenezaji wameshauri" mwisho wa kunukuu hivyo kitendo cha kuona total hawaweki oil ya 5w30 kikakufanya uamini kwamba sio oil sahihi kwa gari yako utakua unajidanganya bure, wale ni wafanya biashara na wanaleta mzigo mwingi unaotoka sana lakin sio washauri wa biashara kwamba wanachokushauri ndicho unatakiwa ukinunue,

no siku wateja wakiwa wengi na kuanza kutumia 5w30 kuliko 5w40 nao watabadilika pia hivyo kitu cha msingi kwenye gari yako kama unataka uishi nayo miaka mingi ni kutumia recommended oil na ufanye service kwa angalau kati ya 3000-5000 miles ambayo ni kama km 5000-7000 kama tu umetumia synthetic oil na genuine oil filter ila kama umetumia mineral oil badilisha oil kila baada ya km 2000-2500
 
Pamoja na maelezo mazuri ya link uliotuambatanishia mwisho wa siku ujumbe wa maana kwa ajili ya gari yako uko pale kwenye neno conclusion ambapo amesema "unatakakiwa/ kushauriwa kutumia oil ambayo watengenezaji wameshauri" mwisho wa kunukuu hivyo kitendo cha kuona total hawaweki oil ya 5w30 kikakufanya uamini kwamba sio oil sahihi kwa gari yako utakua unajidanganya bure, wale ni wafanya biashara na wanaleta mzigo mwingi unaotoka sana lakin sio washauri wa biashara kwamba wanachokushauri ndicho unatakiwa ukinunue, no siku wateja wakiwa wengi na kuanza kutumia 5w30 kuliko 5w40 nao watabadilika pia hivyo kitu cha msingi kwenye gari yako kama unataka uishi nayo miaka mingi ni kutumia recommended oil na ufanye service kwa angalau kati ya 3000-5000 miles ambayo ni kama km 5000-7000 kama tu umetumia synthetic oil na genuine oil filter ila kama umetumia mineral oil badilisha oil kila baada ya km 2000-2500

Unachosema ni kweli kabisa ila msingi wa swali ulikuwa ukweli kwamba kwenye hiyo article wanasema hizi oil hazina tofauti sana, ingawa ipo kwenye viscousity na mazingira ambayo zinafaa kutumika. Na mwandishi alionyesha kama vile kwenye mazingira ya joto 5W 40 inaweza kuwa bora zaidi. Manufacturers recommendations sio kitu cha kupuuzia ila sio msaafu na ndio maana niliuliza
 
Ila bado kwa hali ya hapa kwetu nchini Tanzania na hasa kwa wakazi wa tunaoish jijin dar es salaam na mikoa jirani best oil kwa ajili ya gari yako hasa hizi saloon tumia 5w30
 
Ni kweli nusususu lakini siyo kweli kamili. Ni kwamba kuanzia oili namba 40 na zaidi ni nzito sana na ni kwa magari makuukuu ambayo yameshakula sana pistons rings , main bearings, con-bearings pamoja na valve seaters, kwa hiyo oili nzito ya 40 na zaidi inakuwa inaziba vizuri mapengo yaliyokwisha jitokeza. Kama gari lako linatumia hydraulic valve lifter, hayo yanaweza kuziba matundu yake haraka sana kwa sababu ya uzito wake ukaanza kupata matatizo mengine ya gari kuanza kuwa na miss zisizokuwa za lazima. Watu wanaposema nchi za joto,...
Kuna mtu amewekewa oil ya 20W50 kwenye Rav4 yake.

Nahisi ishakufa sasa.
 
Kuna mtu amewekewa oil ya 20W50 kwenye Rav4 yake.

Nahisi ishakufa sasa.
Labda imeshakula vyuma sana hivyo anataka kuwa anazibaziba mapengo kwa oil, vinginevyo injini hiyo haitadumu sana. Nashangaa kuwa oili hizo ni nyingi sana Dar es Salaama wakati huku kwetu ni chache sana; hata ile website aliyoleta mchangiaji mmoja inasema wazi kabisa kuwa oil hizo hazipatikani sana
 
Mkuu nmeku PM

Sent from my SM-A920F using JamiiForums mobile app
 
Labda imeshakula vyuma sana hivyo anataka kuwa anazibaziba mapengo kwa oil, vinginevyo injini hiyo haitadumu sana. Nashangaa kuwa oili hizo ni nyingi sana Dar es Salaama wakati huku kwetu ni chache sana; hata ile website aliyoleta mchangiaji mmoja inasema wazi kabisa kuwa oil hizo hazipatikani sana
Gari mpya kabisa. Hata km 80,000 haijafika.
 
Back
Top Bottom