Niulize chochote kuhusu injini za magari madogo na pickup zinazotumia Petroli

Niulize chochote kuhusu injini za magari madogo na pickup zinazotumia Petroli

Wakuu naomba msaada wenu natumia gari aina ya Toyota Raum.

Siku hizi mbili gari yangu imekua ikikosa nguvu haswa mlimani pamoja na kuchelewa kubadili gia pia imeandamwa na miss nyingi.

Injini 4E

Naomba msaada wa ushauri nn cha kufanya
 
Mkuu Kichuguu asante sana kwa uzi huu.

Nina Nissan X-Trail ya mwaka 2002, nliinunua kwa mzee mmoja hivi. Ni namba B ila kiukweli mzee aliitunza vizuri sana. Sasa nlipoichukua nadhani nlii-abuse(maji ya Dawassa n.k), nikaitumia kama miezi mitatu ikaanza kuchemsha, nikaipeleka kwa washkaji wa uchochoroni wakaichokonoa mara kadhaa mpaka nlipojua nimeua injini...
Toa belt alafu washa usikie kma muungurumo umepungua. Ukipungua cheza na belingi za izo pulls.
 
Viongozi habari, nina prado 95, ina tatizo la kuyumba sana barabarani nikiwa spidi kuanzia 70 tu, nimebadilisha vitu vyote vya mbele kama boljoint, tyrod nk, nimepima wheel balancing /alignment, lakini bado, je tatizo linaweza kuwa nini?
 
Ni zipi dalili za coil zile za kwenye Injini ya 4E kufu ?

Na je ni madhara gani yanaweza kutokeaa baada ya hizo coil kufa?
 
Ni zipi dalili za coil zile za kwenye Injini ya 4E kufu ?

Na je ni madhara gani yanaweza kutokeaa baada ya hizo coil kufa?
Zikifa gar inamiss, inachekewa kuwaka, inazima zima ghafla na inatumia mafuta mengi. Pia mosh unaweza kuwa unatoka wenye harufu ya fuel.
 
Japo siye uliyeniuliza swali
Je, ni knock sensor inareport error au knock sensor ni mbovu?

Muhimu kujua pia mambo ya usomaji wa RPM yana uhusiano mkubwa na CRANKSHAFT POSITION SENSOR na KNOCK SENSOR kwapamoja.
Nashukuru sana,
kwa jinsi fundi alivyoniambia ni kuwa knock sensor ndio ina shida!
 
Nashukuru sana,
kwa jinsi fundi alivyoniambia ni kuwa knock sensor ndio ina shida!
Ni moja ya sensor muhimu sana maana inahusika na "timing" ya uchomaji wa mafuta (ignition timing) kwa kuhusishanisha na uelekeo wa piston. (Yaani piston ikiwa juu au top dead center ndo muda wa kuchoma mafuta)

Ikiharibika inasababisha gari kutumia mafuta mengi kutokana na mafuta kuchomwa bila mpangilio, kukosa nguvu unapokuwa na spidi au kubeba mzigo, na hata injini ku-knock hivyo ni muhimu sana kuirekebisha mapema

Tumsubiri mkuu Kichuguu atueleweshe zaidi
 
Ndiyo zipo. Sisi tunalipia kwa mwaka kuweza kusoma service manual ya gari yoyote online. Niambie model ya gari lako na mwaka wake kama nitaipata nitadownload na kukuwekea hapa
Mkuu nisidie manua book ya carina T. I
 
Mkuu nisidie manua book ya carina T. I
Nimeshatafutia watu wengi lakini mwishowe inashindikana; nina access na vitabu vya magari ya Kimarekani na Kanada tu. Kwa hiyo nimekuwa nashindwa napata vitabu vya magari mengi yaliyoko Tanzania ambayo siyo ya kimarekani. Kuna baadhi ya magari ya kijapani ambayo kuna model zilizoko Marekani pia kama vile Landcruiser V8 na Camry tunaweza kupata, lakini kwa magari mengi ni mbinde. Hata hivyo nitajaribu nikienda kwenye karakana yetu
 
Mkui nisaidie hata hizo pdf za magari hayo
 
Habari mkuu,
Nilifanya diagnosis kuhusu gari yangu kuwa speed ndogo na odometer kusoma speed kuwa let's say unaona kabisa upo 70km/hr ila odometer itasoma 95 - 100km/hr.

Mtu wa diagnosis akaniambia strainer na "Knock sensor bank 1" ndio zina shida, je nikibadilisha gari yangu itakuwa poa? Maana hata kubadili gear haipo Safi kuna muda inaishia gear namba 3, gari yangu ni Rav4 kilitime automatic transmission.
Samahani, swali hili sikulion mapema.

Lina majibu mawili; (1) Kuhusu speedometer kusoma 90km/hr wakati gari lina mwendo mdogo kunasababishwa na ama matairi kutokuwa na upepo wa kutosha au kutumia matairi madogo ambayo siyo saizi ya gari. (2) Knock Sensor Bank 1 ( yaani kushoto kwa V-Engine) kufa hakuna uhusiano wowote na speedometer, ila inapunguza sana nguvu za injini, na gari haiwezi kuongeza mwendo hata ukikanyaga pedeli mpaka mwisho. Kwa kawaida utatakiwa kubadilisha knock sensors pande zote mbili za injini (yaani bank 1 na bank 2)
 
Ni moja ya sensor muhimu sana maana inahusika na "timing" ya uchomaji wa mafuta (ignition timing) kwa kuhusishanisha na uelekeo wa piston. (Yaani piston ikiwa juu au top dead center ndo muda wa kuchoma mafuta)

Ikiharibika inasababisha gari kutumia mafuta mengi kutokana na mafuta kuchomwa bila mpangilio, kukosa nguvu unapokuwa na spidi au kubeba mzigo, na hata injini ku-knock hivyo ni muhimu sana kuirekebisha mapema

Tumsubiri mkuu Kichuguu atueleweshe zaidi
Umejibu vizuri. Labda niongezee tu kuwa inawezekana knock sensor yenyewe kufa linaweza lisiwe tatizo kubwa sana, ila tatizo ni pale knock sensor inapeleka message kwenye computer kuwa injini inaunguza mafuta hovyo hovyo yaani kuna uncontrolled milipuko kwenye cylinder. Hilo ndilo jambo baya zaidi
 
Wakuu naomba msaada wenu natumia gari aina ya Toyota Raum.

Siku hizi mbili gari yangu imekua ikikosa nguvu haswa mlimani pamoja na kuchelewa kubadili gia pia imeandamwa na miss nyingi.

Injini 4E

Naomba msaada wa ushauri nn cha kufanya
Most likely fuel pressure regulator yako au fuel pamp vimechoka. Hiyo miss inakuwa inasababishwa na mafuta kuingia kwenye injector yakiwa na pressure ndogo sana hivyo hayachomwi ipasavyo, na ndiyo maana gari inakosa nguvu. Sasa hivi gari litakuwa linakula mafuta sana
 
Mkuu habari naomba kuuliza je zipi dalili za kufeli kwa pump ya oil na suruhu yake ni ipi asante
 
Viongozi habari, nina prado 95, ina tatizo la kuyumba sana barabarani nikiwa spidi kuanzia 70 tu, nimebadilisha vitu vyote vya mbele kama boljoint, tyrod nk, nimepima wheel balancing /alignment, lakini bado, je tatizo linaweza kuwa nini?

Nadhani hivyo ulivyobadili vilikuwa siyo tatizo lenyewe ndiyo maana mafundi wazuri huwa hawakimbilii kubadili vitu kiholelea, inabidi fundi wako afanye diagnosis nzuri badala ya kukuambia ubadili kila kitu.

Tatizo kubwa lako kubwa ni stabilizer bars; huwa zinashikiliwa na rubber bushings, ambazo ndizo zitakuwa zimechoka au kulegea. Angalia zaidi zile stabilizer bars za nyuma ambazo huwa ndizo zinazoyumbisha gari zaidi ya zile za mbele.

Halafu pia angalia steering stabilizer kama gari yako inayo. Mwishoni kabisa zile shock absober zako pia zinaweza zinakuletea matatizo hayo, hasa iwapo zile rubber bushings zake zimekwisha hata kama damping effect ya shock abs zako bado ni nzima kuwa ukipita kwenye korongo husikii shock, zile rubber bushings zake zikichoka zote utapata matatizo ya gari kuyumba pia
 
Ni zipi dalili za coil zile za kwenye Injini ya 4E kufu ?

Na je ni madhara gani yanaweza kutokeaa baada ya hizo coil kufa?
Ignition coil zikifa, injini itapa misfire; na madhara yake ni kuwa zikifa zote, basi injini haiwaki. Na iwapo zitakufa baadhi halafu ukaendelea kuendesha gari na miss hizo basi utakuwa unaharibu main bearing za gari yote na unaweza kuua injini ikahitaji overhaul.

Injini zenye knock sensor huweza kuzimika kabisa iwapo kuna misfire kubwa, knock sensor itaiamboa computer ya gari ikate mafuta, na injini itasimama ghafla.
 
Kichuguu

Gari yangu ina shida ifuatayo.

Mwanzo ilikuwa na shida ya coolant kuisha haraka.

Nikabadili radiator top cover na cylinder head gasket na oxygen sensor bank 1 na plugs zote.

Tukajaribu kuweka maji kuangalia kama yataendelea kuisha haraka. Hayakuisha, tukiwasha gari inachemka sana kuliko kawaida, yanaruka pale juu ya mdomo wa radiator. Fundi akasema tutoe thermostat, tulivyoitoa maji yalikuwa fresh kuchemsha kukaisha.

Fundi akasema tuiondoe thermostat moja kwa moja, nikakataa. Akasema basi nikalete mpya.

Nikafika home, nikajaribu kama ile thermostat ni nzima. Nikaichemsha kwenye maji ya moto mpaka 100°C. Ikawa inafunguka fresh. Nikiitoa kwenye maji moto inajifunga. Nikajua thermostat ni nzima. Ila naogopa kuirudisha kwenye gari manake inaweza kuua engine.

Najiuliza, kama thermostat ni nzima? Kwanini nikiiweka kwenye gari inachemka sana? Au kuna tatizo lingine tofauti na hilo? Au ninunue thermostat mpya hivyohivyo regardless hii kuiona ni nzima bado?
 
Kichuguu

Gari yangu ina shida ifuatayo.

Mwanzo ilikuwa na shida ya coolant kuisha haraka.

Nikabadili radiator top cover na cylinder head gasket na oxygen sensor bank 1 na plugs zote...
Oxygen sensor na spark plugs hazikuwa na umuhimu wa kubadili labda kama kulikuwa na dalili nyingine lakini siyo hiyo ya coolant kuisha haraka. Jibu kamili la kukusaidia linahitaji ukaguzi wa sehemu kadhaa za injini yako. (1) Cylinder head gasket umesema umebadili, hilo linaweza kuwa ni jambo jema kwa sababu cylinder head gasket huweza kusababisha maji yavuje na kuingia kwenye cylinder, jambo ambalo siyo zuri kwa uhai wa injini. (2) Kuna jambo amabalo hukuliongelea ni hali ya oil wakati wa kubadilisha.

Iwapo maji yanavuja ndani ya injini, kuna yale yanaoingia kwenye oil samp na baada ya muda oil inakuwa majimaji kabisa jambo ambalo pia siyo zuri kwa uhai wa injini. Sehemu mojawapo ambapo coolant nyingi hupotelea ni kwenye radiator hasa iwapo ina kutu na kuna vijitundu vya kutu vimeanza kujitokeza.

Maji hayo huyaoni yakidondoka bali huwa yanapotea kwa mvuke tu. Umesema ulibadili mfuniko wa radiator ambalo ni jambo zuri pia lakini huenda ni radiator yenyewe inayotakiwa ichekiwe; kuna process inatwa radiator flush ambao unaweka maji ya bomba kwa kutumia mpira wa bustani na kusukuma maji ndani ya radiator kutokea chini. Kukiwa na vitundu vitaonekana wakati wa flush, na itasaidia pia kuondoa kutu- radiator zote zina kutu (usishangae). Baada ya hapo, sababu kubwa ya thermostat kuwa inafanya kazi lakini haifunguki ni kwa sababu water pump yako haina nguvu; unatakiwa kuibadili hiyo pia.

Zaidi ya hapo kuna visehemu vingine vidog vidogo vya kukagua kama vile mipira yako ya maji iko sawa na vitu kama hivyo; ila in general ushauri wangu ni kuwa badili water pump, halafu safisha radiator; usiondoe thermostat. Jambo hilo kuhusu radiator nilishawahi kuliongolea huko nyuma kwenye thread hii.
 
Back
Top Bottom