Kichuguu
Platinum Member
- Oct 11, 2006
- 17,048
- 22,790
- Thread starter
- #721
Peleka gari ichekiwa kwa computer kabla hujalipia matengezo. Sehemu kubwa ya tatizo lako ni sensor fulani inaitwa MAF (Manifold Air Flow) imekufa; kama hiyo ni nzima basi manifold air pressure (MAP) sensor inaweza kuwa imekufa. Sehemu kubwa ya matatizo yako inaelekea kuwa injini haipati hewa ya kutosha wakati unaanza.Ukiwasha gari asubuh silencer haikai inazima mpaka uwashe mara 2 au mara 3, halafu ukitembea baada ya muda inawasha check engine...sema check engine kuna siku inawaka na siku nyingine haiwak kabisa aua inawaka na kupotea...ila mpaka uendeshe gari kwa muda flan hiv
Vitu vingine ambavyo mimi sivipi uzito sana ni pamoja na betri kuwa haina nguvu ya kutosha au gari kuwa na oil iliyochoka au nzito sana (hili linawezekana sana Tanzania kwa vile watu wengi wanatumia SAE40 na SAE50 kwenye injini ndogo). Check betri yako na oil kabla ya kupeleka gari kwenye computer scan. kama gari yako ina geji ya betri na geji ya oil basi unategemea kuwa unaona geji hizo zikisoma zaid ya nusu.