Niulize chochote kuhusu injini za magari madogo na pickup zinazotumia Petroli

Niulize chochote kuhusu injini za magari madogo na pickup zinazotumia Petroli

Labda umeweka matairi madogo kuliko saizi yake, au matairi yako hayana upepo wa kutosha.Kuhusu injini kukosa nguvu, inaweza kutokana na sababu mbili kubwa;
(1) Gearbox yako haina mafuta (ATF) ya kutosha au yashachafuta sana na filter imeanza kuziba
(2) Fuel pump imechoka haipeleki mafuta ya kutosha kwenye injini

Baada ya hizo mbili kubwa nyingine ndogo ndogo ni pamoja na air filter kuwa chafu, fuel pressure regulator kuchoka, fuel filter (kama inayo- magari mengi ya kisasa fuel filter imejengewa kweye fuel pressure regulator) kuziba.
Nashukuru sana mkuu, nitapeleka kwa fundi acheki hivyo vitu maana imekuwa kero.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Labda umeweka matairi madogo kuliko saizi yake, au matairi yako hayana upepo wa kutosha.Kuhusu injini kukosa nguvu, inaweza kutokana na sababu mbili kubwa;
(1) Gearbox yako haina mafuta (ATF) ya kutosha au yashachafuta sana na filter imeanza kuziba
(2) Fuel pump imechoka haipeleki mafuta ya kutosha kwenye injini...
Mkuu samani, nina toyota starlet ilikuwa ina chemsha niaamua kubadili gascate, ila baada ya kubadili shida nyingine ikajitokeza ya gari kukosa nguvu, haichanganyi kwa wakati hasa kwenye milima, mafundi wakashauri nibadili plug...nikafanya hvyo ila tatizo likawa bado liko pale pale

Wakanambia nibadili fuel pump na fuel filter nikafanya hvyo. Tatizo likapungua kidogo ila bado gari haijarud katika nguvu ile ya mwanzo.

Kumbuka kabla ya kuanza kuchemsha ilikuwa na nguvu ya kutosha kabisa. Naomba ushauri maana inpoelekea naweza ambiwa nibadili injini au gearbox. Kwa mwenye uzefu na starlet au ugojwa kama huu naomba ushauri.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Bavaria,
Ni cylinder head gasket kuchoka au cylnder head yenyewe imepasuka; huo moshi mweupe unatokana na maji kuingia ndani ya cylinder na kuchanganyikana na mafuta wakati kuchomwa, na hivyo mafuta hayachomwi sawasawa ndipo unapata moshi mweupe..
KICHUGUU UKO VIZURI na wanajamvi wote hapa wanaotusaidia sisi ambao hatuna uzoefu na magari

Hawa mafundi wetu huku mtaani wanatuulia MAGARI yetu kwa upumbavu wao. mfano, Mimi gari yangu inayotumia petrol inatoa moshi mweupe mwingi hawa mafundi wetu wananiambia rings piston zimekufa nifanye overhaul nikakataa na kuamua kuipack gari toka miezi mitatu iliyopita

Kupitia hapa naendelea kujifunza mengi sana sana
 
Mkuu samani, nina toyota starlet ilikuwa ina chemsha niaamua kubadili gascate, ila baada ya kubadili shida nyingine ikajitokeza ya gari kukosa nguvu, haichanganyi kwa wakati hasa kwenye milima, mafundi wakashauri nibadili plug...nikafanya hvyo ila tatizo likawa bado liko pale pale

Wakanambia nibadili fuel pump na fuel filter nikafanya hvyo..
Mafundi wako hao siyo mafundi makini na wamekuingiza gharama kubwa bure tu. Gari kuchemsha tu siyo dalili ya cylinder head gasket kuharibika; kuna dalili nyingine zilitakiwa zionekane kabla hujabadili cylnder head gasket; kwa mfano maji kuisha haraka, kutoa moshi mweupe, na oil kuharibika mapema.

Sasa kama injini ilikuwa inachemsha lakini bado ina maji na wala haitoi moshi mweupe tatizolilikuwa ni ama water pump au radiator tu. Baada ya kubadili gasket hiyo huoni ikichemsha siyo kwa sababu ulitatua tatizo ila kwa vile sasa injini haifanyi kazi sana kwa kuwa unasema haina nguvu.

Kutokuwa na nguvu huko kunaweza kuwa kunasababishwa na kuwa Cylinder head gasket haikuwekwa sawasawa kwa hiyo kuna sehemu inavujisha pressure huenda kutoka cylinder moja kwenye cylinder nyingine au walifunga gasket hiyo bila kuwa makini wakaangusha uchafu (mchanga) kwenye cylinder na kusababisha piston rings zisagike. Ila inawezekana pia kuwa katika kuweka cylnder head gasket, walifungua sehemy nyingine kwa bahati mbaya kama tappets na kuzihamisha clearance yake bila kujua

Kwa bahati mbaya sina jibu la mkato mpaka niikague gari hiyo kwa kufanya pressure test na vile vile kupima tappet clearances zote. Pole sana ndugu yangu, mafundi hao wa kubabaisha wamekutia hasara ya bure tu. Fundi mzuri hawezi kuwa anatoa majibu la kujaribujaribu eti labda gasket, halafu labda plugs halafu labda fuel pump, mwishowe atakuambia badili injini yote. Huyo siyo fundi. Tatizo ni kwamba hapo kwetu hatuna utaratibu wa kuwa leseni za ufundi wa magari, kijana yoyote akiwa spana boi na kujua kubadili oil akavaa ovaroli lenye mafutamafuta basi anaitwa fundi.
Nina
 
Kichuguu gari yangu imetembea km 186000 oil gani nzuri Mimi nilitumia s40 je nataka nibadilishe
Kama ni gari ndogo ya petroli, SAE 40 ni nzito sana, tumia SAE30 au 10W-30. Ila kama ni gari ya diseli au ni gari kubwa kidogo basi unaweza kuendelea kutumia hiyo SAE40
 
KICHUGUU.
Gari ni ya petrol ilipoanza kutoa moshi mweupe mwingi hawa mafundi wa chini ya miembe wakaniambia badili oil tatizo litaisha oil imechoka sana na wakatumia uelewa wangu finyu wa magari wakasema S40 ndo kiboko yao kwa kuwa gari yangu ni ya miaka 2002 nikakubali

Sasa baada ya kubadili oil tatizo LA moshi likakata kama wiki hivi Ila badae likarudi tena na yule fundi akasema kwa confidence ya hatari RINGI IMEKULA HIYO badili au nunua MSWAKI hapa nikatumia akili kidogo ya kukataa mpaka Leo gari liko ndani nimelifungia kwa kukosa matibabu halisi

Ila sasa kupitia wewe na wengine wengi hapa jamvini nimeanza kupata mwanga cha kufanya

Kama una cha kuniongeze tafadhali nitapokea kwa mikono miwili KWA KUWA MWEZI HUU WA SITA NATAKA KUTIBU TATIZO

NATANGULIZA SHUKRANI ZANGU ZA DHATI KWA WOTE MLIONIFUNGUA MACHO HAPA JF
 
Mkuu Kichuguu
Gari yangu yenye 4E engine inagonga sana kwenye mashine, fundi kashauri tuishushe mashine shaft ikapimwe kisha tubadili meni na koni, je inaweza kuwa sahihi?

Gari inatembea kama kawaida na ina nguvu yake ila tatizo ni engine kugonga.
 
Mkuu Kichuguu
Gari yangu yenye 4E engine inagonga sana kwenye mashine, fundi kashauri tuishushe mashine shaft ikapimwe kisha tubadili meni na koni, je inaweza kuwa sahihi?

Gari inatembea kama kawaida na ina nguvu yake ila tatizo ni engine kugonga.
Aliloshauri fundi linaweza kuwa ni kweli lakini inategemea umekuwa unatunza gari namna gani, hasa kuhusu oil. Sababau kubwa ya mainbearing na Connrod bearings kufa ni kuendesha gari bila oil au kuwa na oil chafu kwa muda mrefu. Na kama hilo limetokea utakuwa unaona gari lako linakuwashia taa ya oil hata kama ukibadili oil, wakati mainbearings zimekufa ni lazima itakuonyesha taa ya oil tena. Bila kuona taa ya oil, ninakushauri usikimbilie kubadilisha hizo bearing, kwani zinahitaji umakini sana na sehemu kubwa ya mafundi huwa wanaokesea jinsi ya kuziweka, na inakuwa unarudia kubadilisha mara kwa mara na kuchosha injini yako zaidi.

Mimi ningeshauri kwanza ucheck hydraulic valve lifters au tappets; katika injini nyingi, kelele za injini husababishwa na hizo lifters kwa silimia kama 80% kuliko main bearings. Hizo lifters zinasukumbwa kwa oil na huwa zina vijitundu vidogo sana vya kupitisha oil; ukiwa na oil chafu inaweza kuziba hivyo vijitundu na kusababisha lifter hizo zisifanye kazi, hali inayojidhihirisha kwa hiyo knocking sound. Wakati mwingine hata kama oil ni safi, unga wa chuma utokanao na msuguano huweza kuingia na kuziziba.

Ndiyo maana katika service ya gari unapofikia kubadilisha spark plugs, huwa pina unashauriwa uangalie hizo hydraulic lifters. Kwenye shop yetu huwa tunazibadilisha baada ya km 150,000 hata kama bado zinafanya kazi; siyo kazi kubwa kuzibadilisha na wala hazigharimu sana. Set ya lifter 16 kwa V-8 engine zinauzwa kati ya dola 40 mpaka dola 65 ambayo ni sawa na bei ya Main na Con-bearings. Lakini kazi ya kubadilisha bearings ni kubwa sana inayoweza kuchukua siku mabili au tatu, wakati lifters ni kazi ya kama saa moja tu.
 
Aliloshauri fundi linaweza kuwa ni kweli lakini inategemea umekuwa unatunza gari namna gani, hasa kuhusu oil. Sababau kubwa ya mainbearing na Connrod bearings kufa ni kuendesha gari bila oil au kuwa na oil chafu kwa muda mrefu. Na kama hilo limetokea utakuwa unaona gari lako linakuwashia taa ya oil hata kama ukibadili oil, wakati mainbearings zimekufa ni lazima itakuonyesha taa ya oil tena. Bila kuona taa ya oil, ninakushauri usikimbilie kubadilisha hizo bearing, kwani zinahitaji umakini sana na sehemu kubwa ya mafundi huwa wanaokesea jinsi ya kuziweka, na inakuwa unarudia kubadilisha mara kwa mara na kuchosha injini yako zaidi...
Akhsante sana mkuu.
Taa ya oil huwa inachelewa kuzima mpaka gari itembee kama dakika mbili hivi ndiyo inazima, niliwahi kuambiwa shida hiyo ya taa ya oil kuchelewa kuzima ni oil filter ni feki ninunue iliyoandikwa Toyota, nikabadili ikawa safi ila baada ya muda ikawa vile vile mpaka ikafikia gari kuanza kugonga engine.
 
Mkuu KICHUGUU hiv error ya SYSTEM TOO LEAN ukiweka gari kwenye mashine ya diagnosis inamaamisha nn
Too lean maana yake ni kuwa injini inaingiza hewa nyingi kuliko mafuta; siyo vizuri kuendesha injini ambayo ni too lean kwa muda mrefu bila kujua chanzo chake ni nini kwa vile kuna sababu ambazo zinaweza kuua injini yote na vile vile kuna sababu ambazo hazina madhara sana kwenye injini. Sababu moja ya kuogopwa ni pale njia ya hewa inapokuwa na matundu, hivo hewa inayopita kwenye intake air flow sensor ni ndogo kuliko hewa halisi inayoingia kwenye injini. Sababu ya pili ni pale injector hazifanyi sawasawa na hivyo zinapitisha mafuta machache sana kuliko yanyohiyaji.

Sababu zote hizi ni mbaya sana zinaweza kuharibu injini yako, ni lazima uzidhibiti haraka sana; hizi huandamana na injini kupungua nguvu. Kati ya sababu ambazo hazina madhara ni pamoja na oxygen sensor mojawapo kuwa mbovu, ikawa inapeleka taarifa kwenye computer kuwa kuna oxygen nyingi wakati siyo hivyo; tatizo la sensor ni kero tu ya kuona warning kwenye dashboard lakini injini haidhuriki.
 
Akhsante sana mkuu.
Taa ya oil huwa inachelewa kuzima mpaka gari itembee kama dakika mbili hivi ndiyo inazima, niliwahi kuambiwa shida hiyo ya taa ya oil kuchelewa kuzima ni oil filter ni feki ninunue iliyoandikwa Toyota, nikabadili ikawa safi ila baada ya muda ikawa vile vile mpaka ikafikia gari kuanza kugonga engine.
Ebu nieleze kidogo kuhusu hiyo taa ya oili; je inabaki imeweka kwa muda gani. Inaweka kubaki imewaka kwa muda wa robo saa hivi au ni dakika mbili tatu tu. Kuchelewa kuzima kwa taa ya oil siyo tatizo sana iwapo ishishazima inabaki vile vile hadi inji itakaposimama. tatizo ni pale taa hhiyo itakuwa inawaka na kuzimazima bila utaratibu wowote. Kagua hizo Valve lifters kwanza kabla ya kufanya overhaul ya engine.
 
Mkuu natumia gari ina engine ya 1NZ FE toka ije na kilomita efu 57 hadi sasa ina kilomita 97 asee sijawahi weka recommended oil yake ya 5w 30 au 10w 30 ni mwendo wa sae 40 na service ya mwsho jamaa aliniwekea 20w 50 baada ya kupita pita humu ndio nikaelewa kuhusu elimu ya oil je naweza kurudi kwny 5w 30 au 10w 30 au too late mkuu Kichuguu
Ebu nieleze kidogo kuhusu hiyo taa ya oili; je inabaki imeweka kwa muda gani. Inaweka kubaki imewaka kwa muda wa robo saa hivi au ni dakika mbili tatu tu. Kuchelewa kuzima kwa taa ya oil siyo tatizo sana iwapo ishishazima inabaki vile vile hadi inji itakaposimama. tatizo ni pale taa hhiyo itakuwa inawaka na kuzimazima bila utaratibu wowote. Kagua hizo Valve lifters kwanza kabla ya kufanya overhaul ya engine.
 
Mkuu natumia gari ina engine ya 1NZ FE toka ije na kilomita efu 57 hadi sasa ina kilomita 97 asee sijawahi weka recommended oil yake ya 5w 30 au 10w 30 ni mwendo wa sae 40 na service ya mwsho jamaa aliniwekea 20w 50 baada ya kupita pita humu ndio nikaelewa kuhusu elimu ya oil je naweza kurudi kwny 5w 30 au 10w 30 au too late mkuu Kichuguu
Rudi kwenye oil yake- tumia 10W-30 au SAE30 kama inapatikana, tena utashangaa injini yako itakavyotulia. Bado hujachelewa sana
 
Electronic Power Steering (EPS) failure inapotokea maana yake ni kuwa ile motor inayokusaidia kuzungusha steering wakati wa kupiga kona inakuwa haifanyi kazi sawasawa, kwa hiyo hupeleka data kwenye computer ya injini (ECU) ambayo hukata umeme usiende kwenye motor hiyo kabisa, ndiyo maana steering yako inakuwa ngumu sana...
We jamaa uko vizuri Sana
Mimi Ni fundi umeme
Nnakuelewa japo sio upande was magari
Ila unaelezea kama mtu anaejua,,,sii kuotea
Bigg up
 
Too lean maana yake ni kuwa injini inaingiza hewa nyingi kuliko mafuta; siyo vizuri kuendesha injini ambayo ni too lean kwa muda mrefu bila kujua chanzo chake ni nini kwa vile kuna sababu ambazo zinaweza kuua injini yote na vile vile kuna sababu ambazo hazina madhara sana kwenye injini. Sababu moja ya kuogopwa ni pale njia ya hewa inapokuwa na matundu, hivo hewa inayopita kwenye intake air flow sensor ni ndogo kuliko hewa halisi inayoingia kwenye injini. Sababu ya pili ni pale injector hazifanyi sawasawa na hivyo zinapitisha mafuta machache sana kuliko yanyohiyaji. Sababu zote hizi ni mbaya sana zinaweza kuharibu injini yako, ni lazima uzidhibiti haraka sana; hizi huandamana na injini kupungua nguvu. Kati ya sababu ambazo hazina madhara ni pamoja na oxygen sensor mojawapo kuwa mbovu, ikawa inapeleka taarifa kwenye computer kuwa kuna oxygen nyingi wakati siyo hivyo; tatizo la sensor ni kero tu ya kuona warning kwenye dashboard lakini injini haidhuriki.

Ukiwasha gari asubuh silencer haikai inazima mpaka uwashe mara 2 au mara 3, halafu ukitembea baada ya muda inawasha check engine...sema check engine kuna siku inawaka na siku nyingine haiwak kabisa aua inawaka na kupotea...ila mpaka uendeshe gari kwa muda flan hiv
 
Back
Top Bottom