Niulize chochote kuhusu injini za magari madogo na pickup zinazotumia Petroli

Ahsante nitakupa feedback
 
Habarini za majukumu naomba kueleweshwa nanna ya kubadilisha rugha kwenye radio za gari za ist
Hiyo sijui; itabidi utafute kitabu cha hiyo gari. Magari mengi ya kimarekani huwa ya kibonyezo cha SET na kibonyezo cha NEXT. Kwa hiyo ukibonyeza SET na kufuatiwa na NEXT mara kadhaa utaona lugha zinabadilika hadi ile lugha unayotaka.
 
Mkuu kichuguu
Habari ya Leo..pole na Nazi
Gari yangu inanisumbua ktk mfumo wa mpumuaji ...Kama kawaida mafund wetu ni waharibifu Sana kiasi nimeshaingia gharama kubwa Sana..mara wanatoa kifaa hiki unanunua kile lkn bado tatz haliishi.

Gar yangu nikiwa folen au nikiachia moto ikawa ktk speed ndogo inazima2na mara nying inakuwa inaanza kwa kustuka stuka zen inazma...ukiwasha inawaka vzr unaenda ukishuka au kuachia moto tena inazima ah ukitembea speed chini ya10 inakata.....

Nimecheki air filter iko poa na haina uchafu,air filtrr sensor ni nzima ...kimsingi vitu vyote ni vizima ktk mfumo wa hewa.....sasa naona nanaambiwa tu mara hiki kibovu unabadili bola1...naona naingia loss tu....

Naomba msaada wako mkuu...gari inazima..hata nimejaribu kuinua muungurumo nao baada ya muda mfupi unashuka kutoka1 hadi nusu...na hatimae linazima zima bila sababu.,

Hapo nyuma ilichemsha nikawa nimeitumia kwa umbali wa km 3 hivi..kucheki maji yalikuwa yanatoka kwenye mfumo kurud ktk reserve na yanachemka na kumwagika na ndo chanzo cha kuchemsha....nafikiri baada km ya mwez hivi ndo imeanza huu mchezo sasa wa kuzima ikiwa umesimama au kuwa KTM mwendo mdogo...

Tafadhari msaada wako...nawasilisha
 
Mkuu kichuguu
Habari ya Leo..pole na Nazi
Gari yangu inanisumbua ktk mfumo wa mpumuaji ...Kama kawaida mafund wetu ni waharibifu Sana kiasi nimeshaingia gharama kubwa Sana..mara wanatoa kifaa hiki unanunua kile lkn bado tatz haliishi...
Niambie vitu ambavyo umeshabaidilisha bila mafanikio
 
Gari yangu inaniwashia check engine nikishatembea umbali mdogo nilishaipeleka service na fundi nmemwambia ila ttzo bado lipo yeye fundi anasema ameangalia vitu muhimu vyote vipo sawa
 
Engine check yangu inawaka tu' na fundi aliniambia ameangalia vtu vyote vya muhimu vipo sawa' tangu aniambie hivyo nmeshaitumia miezi mi2 na ipo tu vzr ttzo sijui ni nini'
Engine Check ikiwaka ni lazima kuwe na hitilafu fulani. Jibu sahihi litapatikana tu kwa kuinganshia na computer scanner kusoma code zake...
 
Hiyo sijui; itabidi utafute kitabu cha hiyo gari. Magari mengi ya kimarekani huwa ya kibonyezo cha SET na kibonyezo cha NEXT. Kwa hiyo ukibonyeza SET na kufuatiwa na NEXT mara kadhaa utaona lugha zinabadilika hadi ile lugha unayotaka.
Ahsante mkuu
 
Mkuu kuna gari lina shida limeanza hivi juzi yaani kula mafuta mengi na kutoa moshi mwingi pia plugs zinawahi kuisha nguvu .pia ukibadilisha kutoka D kwenda R inakita sana au unapoongeza gia inakita hii imeanza baada ya kubadilisha control engine iliyokuwepo ni IMO sasa imewekwa ya kawaida .je haya matatizo yatayamalizwaje?
 
Kunawezekana kuwapo kwa mchanganyiko wa matatizo yanayoingiliana. Gia kugota husababishwa na ama mafuta ya gearbox kupungua, clutch ya transmission kuchoka, au engine mounts na transmission mounts kuchoka au kulegea.

Lakini vile vile inawezeka ndani ya transmission kukawa na matatizo hasa ile computer ya transmission ikawa inasoma spigi ya injini vibaya au enginen speed sensor ikawa haifanyi kazi vizuri kwa hiyo computer haijui sawasa kama injini inekwenda kwa spidi gani kuahikisha kuwa gera box nauo inajipanga sawasawa kulingana na mzunguko wa injini.

Kula mafuta mengi pia kunasababishwa na vitu vingi sana lakini kwa tatizo lako inawezekana sana kwamba cluctch ya transmission yako ndiyo inayosababisha mgoto wa transmission na vile vile injini kula mafuta, yaani haipeleki torque yote kwenye matairi kwa hiyo gari linakuwa kama halina nguvu inabidi ubonyeze accelerator muda wote; ukiacha acceleator linasimama.

Spark plugs huwa hazifi mapema na wala hayo matatizo niliyotaja hapo juu hayana uhusianao na sapark plug kufa. Inawezekana kuwa unatumia sparkplugs substandard, au zinakuwa hazikufungwa vyema na hivyo kusababisha ziwe zinachoma vibaya vibaya. Je, injini yako ina vibrate sana na kuchemka haraka? Kama ina vibrate sana na kuchemaka haraka basi huenda spark plugs hazifungwi vizuri.

Kuna kipimo cha kufungia spark plugs ingawa kwetu wanatu wengi huwa wanafunga hadi wajisikie tu. Vinginevyo inawezekana fuel filter yako imechoka ikwa hiyo inapitisha uchafu pia. Vinginveyo labda oil au coolant inavuja kwenye combustion chambe (Cylinder head gasket au cylinder head imepasuka)

kwa jumula matatizo ya gari lako yanahitaji ukaguzi mzuri kwani yanaweza kuwa yanahusiana au hayahusiani. (1)Cluch plates- Hata automatic transmission ina clutch plates, (2) Cranks rotation sensor, (3) Transmission fluid, (4) Fuel filter, (5) Ufungaji wa Spark plugs, (6) Uvujajai wa oil/ coolant kwenye combustion chamber ( je oil na coolant kwenye gari huwa zinakiwasha haraka haraka?
 
Engine check yangu inawaka tu' na fundi aliniambia ameangalia vtu vyote vya muhimu vipo sawa' tangu aniambie hivyo nmeshaitumia miezi mi2 na ipo tu vzr ttzo sijui ni nini'
Inawezekana matataizo ni kwenye exhaust system; yaani catalytic converter. Huwa haina matatizo sana kwenye injini bali inachafua mazingira. Magari mengi yenye umri mrefu kuazia miaka minane na kuendelea hukumbwa na adha hiyo hata kama hayajatembea umbali mrefu. Kwani scan ya Computer inasemaje?
 
boss nna vitz old model taa ya check engine na mimi inawaka nilifungua top cover ilikuwa inavujisha nikaifunga vizuri now haivujishi tena ,but check engine inawaka,nikatoa ile switch nikaisafisha but still inawaka shida inaweza kuwa nini
shukran
 
boss nna vitz old model taa ya check engine na mimi inawaka nilifungua top cover ilikuwa inavujisha nikaifunga vizuri now haivujishi tena ,but check engine inawaka,nikatoa ile switch nikaisafisha but still inawaka shida inaweza kuwa nini
shukran
Maelezo yako hayako sawa; ulifungua top cover ya nini. Halafu Check engine light sababu yake itajulikana tu kama unaipelekea gari yako kwenye computer scan, ila ukiniambia ni nini kilikuwa kinavuja ninaweza kuhis tatizo ni ni nini ila bado itabidi uende kwenye computer scan.
 
Pale taa ya oil inapowaka na kuzima gari ikiwa mwenye mwendo na gari kubadilisha Muungurumo tatizo huwa ni nini? Muda mwingine ikiiacha inakaa vizuri ila ikienda safari ndefu inatokae hiyo?
 
Pale taa ya oil inapowaka na kuzima gari ikiwa mwenye mwendo na gari kubadilisha Muungurumo tatizo huwa ni nini? Muda mwingine ikiiacha inakaa vizuri ila ikienda safari ndefu inatokae hiyo?
Inawezekana oil pressure sensor imekufa; inaposhindwa kupelea pressure ya kutosha kwenye computer, basi computer inashindwa kuongoza injini vizuri ndipo unasikia muungurumo unabadilika.
 
Taa ya check engine inawaka baada ya iuscan inaleta error ya SYSTEM TOO LEAN nshabadilisha air mass sensor kama mara 3 hv lakin tatzo bado
 
Taa ya check engine inawaka baada ya iuscan inaleta error ya SYSTEM TOO LEAN nshabadilisha air mass sensor kama mara 3 hv lakin tatzo bado
Kama injini ina nguvu kama kawaida basi Intake manifold inaweza kuwa inavuja; yaani baada kupita kwenye air flow sensor kuna hewa nyingine inaingia kwenye injini bila kupimwa na air flow sensor. Kama injini haina nguvu, basi huenda injector zako hazifanyi kazi vizuri kwa hiyo haziingizi mafuta ya kutosha kwenye injini. Vinginevyo inawezekana oxygen sensor yako imekufa, inapeleka namba mbaya kwenye computer
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…