Electronic Power Steering (EPS) failure inapotokea maana yake ni kuwa ile motor inayokusaidia kuzungusha steering wakati wa kupiga kona inakuwa haifanyi kazi sawasawa, kwa hiyo hupeleka data kwenye computer ya injini (ECU) ambayo hukata umeme usiende kwenye motor hiyo kabisa, ndiyo maana steering yako inakuwa ngumu sana.
Hii motor hufanya kazi kwa kusoma nguvu inayotakiwa na steering kwenye kupiga kona fulani wakati wewe unazungusa hiyo steering, halafu huamua kiasi cha umeme wa kuepelea kwenye motor hiyo kusudi ibebe mzigo huo badala yako. Sasa basi, wakati mwingine hutokea kwa bahati mbaya tu kwamba computer ilipata spike ya data mbaya lakini hakuna tatizo; ukizima injini na kuondoa waya mmoja wa betri kwa robo saa na kustart gari tena itafanya kazi tu. Ila kama haifanyi kabisa hata ukishazima injini na kuondoa waya mmoja wa betri, basi kwa kisi kikubwa itakuwa ni steering torque sensors zinahitaji kubadilishwa, au kwa kiasi kidogo sana labda ni motor yenyewe imechoka.
Kiwango kidogo zaidi na ambacho ndicho serious sana ni pale ile gearbox inayoendesha steering yako itakuwa ndiyo imekufa. Hayo ndiyo maeneo makubwa matatu ya kuangalia.
Kupata jibu halisi, ipeleke gari yako ikafanyiwe coomputer scanning kujua tatizo halisi linatoka wapi. Kama sehemu zote hizo ni sawa kabisa, basi inawezekana alternator yako ndiyo imechoka haipeleki umeme wa kutosha unaohitajiwa kuendesha motor hiyo.