Mkuu kuna gari lina shida limeanza hivi juzi yaani kula mafuta mengi na kutoa moshi mwingi pia plugs zinawahi kuisha nguvu .pia ukibadilisha kutoka D kwenda R inakita sana au unapoongeza gia inakita hii imeanza baada ya kubadilisha control engine iliyokuwepo ni IMO sasa imewekwa ya kawaida .je haya matatizo yatayamalizwaje?
Kunawezekana kuwapo kwa mchanganyiko wa matatizo yanayoingiliana. Gia kugota husababishwa na ama mafuta ya gearbox kupungua, clutch ya transmission kuchoka, au engine mounts na transmission mounts kuchoka au kulegea.
Lakini vile vile inawezeka ndani ya transmission kukawa na matatizo hasa ile computer ya transmission ikawa inasoma spigi ya injini vibaya au enginen speed sensor ikawa haifanyi kazi vizuri kwa hiyo computer haijui sawasa kama injini inekwenda kwa spidi gani kuahikisha kuwa gera box nauo inajipanga sawasawa kulingana na mzunguko wa injini.
Kula mafuta mengi pia kunasababishwa na vitu vingi sana lakini kwa tatizo lako inawezekana sana kwamba cluctch ya transmission yako ndiyo inayosababisha mgoto wa transmission na vile vile injini kula mafuta, yaani haipeleki torque yote kwenye matairi kwa hiyo gari linakuwa kama halina nguvu inabidi ubonyeze accelerator muda wote; ukiacha acceleator linasimama.
Spark plugs huwa hazifi mapema na wala hayo matatizo niliyotaja hapo juu hayana uhusianao na sapark plug kufa. Inawezekana kuwa unatumia sparkplugs substandard, au zinakuwa hazikufungwa vyema na hivyo kusababisha ziwe zinachoma vibaya vibaya. Je, injini yako ina vibrate sana na kuchemka haraka? Kama ina vibrate sana na kuchemaka haraka basi huenda spark plugs hazifungwi vizuri.
Kuna kipimo cha kufungia spark plugs ingawa kwetu wanatu wengi huwa wanafunga hadi wajisikie tu. Vinginevyo inawezekana fuel filter yako imechoka ikwa hiyo inapitisha uchafu pia. Vinginveyo labda oil au coolant inavuja kwenye combustion chambe (Cylinder head gasket au cylinder head imepasuka)
kwa jumula matatizo ya gari lako yanahitaji ukaguzi mzuri kwani yanaweza kuwa yanahusiana au hayahusiani. (1)Cluch plates- Hata automatic transmission ina clutch plates, (2) Cranks rotation sensor, (3) Transmission fluid, (4) Fuel filter, (5) Ufungaji wa Spark plugs, (6) Uvujajai wa oil/ coolant kwenye combustion chamber ( je oil na coolant kwenye gari huwa zinakiwasha haraka haraka?