Niulize chochote kuhusu injini za magari madogo na pickup zinazotumia Petroli

Vip kuhusu ractis new model
 
Bila shaka taa unayoiona ni hii
...Hii ni taa ya joto la engine...ikiwaka blue means engine ipo katika hali ya baridi, injini ikipata moto taa hii inatoweka.

Injini ikipata joto lililopitiliza kiwango au gari likichemsha taa hiyo itawaka nyekundu..

Kuhusu kujua kama oil inahitajika kubadilisha au imepungua kwa kuangalia signal kwenye dash board, si magari yote yenye option hiyo.. Magari mengi tuliyonayo ni lazima upime kiwango cha oil kwa deep stick iliyopo kwenye engine..

Kujua kama muda wa kumwaga oil umefika, hapa unaweza kutumia clock ya gari lako kupiga hesabu za umbali uliotembea tangu ubadilishe oil kwa mara ya mwisho..
Kwa mfano

Mile age ya gari lako inasoma Km 40000 nw umeweka oil mpya na filter kwenye mile age hiyo...inategemea na aina ya oil ila mara nyingi tunakadiria km 3000 ndipo umwage tena oil...

Hivyo utachukua mileage ya km 40000 +3000=43000.....maana yake utaendesha gari lako likifikisha km 43000 kwenye clock, utabadilisha tena oil....
 
2AZ vs 5S ipi ni Bora kwenye perfomance, fuel consumption, uimara na service.
 
Suzuki Swift inawaka taa ya EPS kwenye dashboard halafu usukani unakuwa mgumu, mafundi wangu wameshindwa kutengeneza utansaidiaje kwa hilo mkuu.
Ulitatua hili tatizo mkuu, nimeface the same problem kwa suzuki swift.
 
Mkuu Safi Sana Kwa Uzi...

Naomba Unisaidie Gari Yangu Ni IST, Huwa Nikiiwasha Asubuhi Au Hata Muda Wa Jioni Wa Kutoka Kazini Kuna Kamlio Flani Kama Ka Mluzi Kanakwenda Sambamba Na Starter Ya Engine...
Na Hata Nikianza Kukanyaga Mafuta Kidogo kidogo Kanaendelea Na Badae Gari Ikichanganya Kanapoteaa...
Tatizo Linaweza Kuwa Nini?
 
hiyo ni belt ya oltanetor
 
Inaweza kuwa ni belt imelegea kama ulivyoshauriwa hapo juu au kuna sehemu hewa inavuja kidogo kwenye intake manifold, au spark plugs zina masizi sana kiasi kuwa zinapokuwa baridi haziwaki sawasawa na kusababisha misfire ndogo ndogo. Ni vigumu kukupa jibu kamili bila kusikia mlio wenyewe
 
Mcheki huyu LEGE
Hilo tatizo la la electronic Power Steering nilimjibu huyu; labda hajapata mafundi wa wazuri wa kuangalia vile vitu vidogovidogo nilivyomtajia kabla ya kuangalia yale makubwa. Lama mpaka leo bado analo, basi nlinasababishwa na mambo madogomadogo tu; yapo kadhaa
 
Seen, umemjibu vizuri mkuu
 
Mkuu, swali langu ni kwamba unawezaje kutambua kuwa hii oil ukiiweka kwenye engine kuja kubadilisha ni mpaka maili au km kadhaa mpaka zipite.. 3000, 5000 au 10000.??

Swali lingine ni kuhusu oil grades zinavyoelezewa...
Mfano hii 15w40, wanasema oil huwa thin (15w) ilikuwe na uwezekano wa kuiwasha engine kwa urahisi na engine ikisha waka at normal operating temp ile oil hugeuka na kuwa nzito (40) nahitaji kujua je kweli??

Swali la mwisho ni kuhusu oil zinazoandikwa kwa kupewa viscosity moja tu mfano hii SAE 40, Je hii inamaanisha oil itabaki katika viscosity hiyohiyo bila kujalisha joto la engine litakuwa namna gani???
 
Maswali yako yote nilishayajibu huko nyuma, Nitaanza na maswali mawili ya mwisho kurudi nyuma.

Oil zinazotumika katika nchi za baridi pia huwa zina namba mbili, kwa mfano 10W-30. Ile namba inyoishia W ni kwa ajili ya nchi za baridi wakati wa Winter. Ile namba ya pili ndiyo ya kwetu zaidi wakati gari linafanya kazi vizuri. Ila kwa vile kuna sehemu hapa kwetu (kama Mufindi) ambako baridi hufikia lile la nchi za Scandinavia, basi oil nzuri kwako itakuwa ni 5W-30; ila ukitumia SAE 30 uko salama pia lakini siyo wakati wa baridi Mufindi.

Ubadilishaji wa oil hautegemei aina ya oila uliyoweka bali unategemea injini yenyewe. Kila gari ina kitabu kinachoonyesha utabadilisha oil kila baada ya muda gani. Watengenezaji wa magari hujua vyuma vyao vinasagikaje na ndio maana wanasema baada ya muda fulani oil inakuwa imejaa vumbi la vyuma, hivyo ibadilishwe.
 
Wadau Nina swali, Hivi Toyota Kluger yenye cc3000 ukinunua yenye km 120,000 unaweza kaa nayo miaka hata 8? Matumizi ni kutembea km let say 9,000 kwa mwaka. Wazoefu wa hii gari msaada wenu tafadhali.
 
Hivi engine hii ya gari dogo la petrol unaweza weka mafuta ya kupikia badala ya oil ikiwa umezidiwa sana?mafuta ya Korie siyo haya ya alizeti.
 
Hivi engine hii ya gari dogo la petrol unaweza weka mafuta ya kupikia badala ya oil ikiwa umezidiwa sana?mafuta ya Korie siyo haya ya alizeti.
SIjui, ila nimeshasikia kweli kuwa kuna mafuta mengine ya kupikia yanaweza kutumika kama oil kwenye injini ndogondgo, hasa mafuta ya mizeituni. Lakini hayawezi kudumu kwa mufa mfrefu.
 
SIjui, ila nimeshasikia kweli kuwa kuna mafuta mengine ya kupikia yanaweza kutumika kama oil kwenye injini ndogondgo, hasa mafuta ya mizeituni. Lakini hayawezi kudumu kwa mufa mfrefu.
So yanaweza tumika kama dharura? Je nikiwasha gari ikawaka then nikachomoa battery itazima?gari za miaka ya 2000 kushuka chini.
 
So yanaweza tumika kama dharura? Je nikiwasha gari ikawaka then nikachomoa battery itazima?gari za miaka ya 2000 kushuka chini.
swali la kwanza: inawezekana, ingawa itetegemea unatumia mafuta ya aina gani,na unakwenda umbali wa muda mangapi. Usitumie Mafuta yenye smoke point ndogo na viscosity ndogo!

swali la pili: jibu ni ndiyo iwapo alternator yako ni nzuri. engine zote huwa hazitumia battery, bali wakati wa kustart tu. Baada ya hapo umeme wote unaohitajiwa na gari hutoka kwenye alternator. Ndiyo maana unashauriwa wakati unastart injini vitu vyote vya umeme viwe OFF: hasa taa, AC, radio, seat heater, rear window defrogger, na wiper.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…