Niulize chochote kuhusu injini za magari madogo na pickup zinazotumia Petroli

Mkuu inshort huna engine,nenda nunua engine swaki weka...hiyo engine yako hata uki overhaul utapoteza pesa tu..kifupi ni kwamba Kwanza engine yako umesha ua head gaskets na probably cylinder head imepinda kabisa because of overheating, so engine inachanganya maji na oil na vyote vinachomwa kwenye combustion chamber ndo maana waona moshi,, lakini pia yawezekana rings za pistons zimekufa so hata compression ni ndogo lakini pia rings zina ruhusu oil kupanda kwenye combustion chamber kwakua hazifanyi kazi yake ya ku seal..

Sent from my TECNO KC8 using JamiiForums mobile app
 
Okey... Na mswaki kikawaida inakua safi kabisa au ndio la mentali tu kujaribu jaribu... Afu makadilio kama ngap hivi??? Na maeneo gani kati ya ilala na tandale ni uhakika??
Usije enda nunua injini tandare mkuu, 90% ni mbovu... Nenda ilala kwa wapemba wanao import from Dubai..au kuna wajapan pale ilala wana gereji yao inaitwa Yokohama utapata injini kinanda...chuguza isiwe na carbon kwenye top cover ya injini au kifuniko cha oil..pia kama utaona upande wa exhaust kukiwa na uweusi mwingi busi usiinunue hiyo injini kwakua inakua inachoma oil nyingi..

And next time ukisha rekebisha gari yako hakikisha una badill oil after every 3000km or 4000 km kama watumia fully synthetic oil...nakama watumia mwaka mzima kutembea km 4000 basi kila badili oil after 6months.

Pia kama ni mtu wa trip fupi fupi unazima na kuwasha gari frequently...basi oil pia uchoka haraka kwa design hii ya matumizi ya gari kwakua wakati wa kuwaka gari umwaga mafuta mengi, so kuna mafuta hupenda kwenye piston rings na kwenda kwenye sump ya oil na ku-contaminate oil..but ya hapo oil hu breakdown..

Sasa ukiweka na oxidation because of excessive engine temperature, baada ya muda ile oil uanza kutengeneza mabonge bonge kama uji..hikifikia hali hii. Huu uji hung'ang'ania rings za oil, huziba njia za oil, oil filter pia huziba, pia rings ziki ng'ang'ania kwa muda mrefu sehemu moja then huanza kuchimba cylinder walls sasa hapa ndo utakuta piston zina anza kucheza cheza, gari ina anza toa moshi mweusi, compression inashuka gari inakosa nguvu au inakua na miss nyingi zisizo isha, pia kwakua njia za oil zimeziba basi utakuta na taa ya oil inawaka kwakua oil pressure ni ndogo kwenye injini hence excessive wear because lubrication is not enough..hapa ndo vyuma uanza kusagana na vvti system kushindwa kufanya kazi kwakua vvti inahitaji oil pressure kufanya kazi..ndo una anza sikia gari inaunguruma kama cherehani na miungurumo mingine ya ajabu ajabu...

Sent from my TECNO KC8 using JamiiForums mobile app
 
Engine kinanda used 1NZ kutoka japan ni karibia milioni mbili kutoka befoward na hapa bongo zipo kibao tu for a lower price. Kwaio chagua ww tu, au fanya overhaul ila uende kwa mafundi wasafi wanaoipenda nakuijua kazi yao tu. Lakini Kutoboka mfuko ni muhimu
 
Mkuu Gari Yako inajizima ukiwa umewasha AC au umezima AC Tuanzie Hapo Ntakupa Jibu na je ikijizima Si unawasha tu fresh
 
Shukrani saaana mzeee hapa ni kujichanga tu kudaka mswaki mpya. .

Sasa kwa kipindi hiki vipi gari niipak au niendelee kuiburuza tu haina shida... Maana nina miez miwili mbele ya kujikusanya kupata mswaki , na gari nahitaji saana kuitumia. Vip siwez sababisha matatizo sehemu zingine??
 
Kwamba bongo inakuwa rahisi kuliko japan sio. .. !?

Kutoboka hakuepukiki hapa
 
Nimeiuwa engine kizembe saana... In km 100000 tu dadek... Ila ukiweka engine ingine... Ndinga si mpya kabisa
 
Ni PM namba yako
 
WaTz wenye fani fulani fulani hamjui kabisa customer care na hamjui namna nzuri ya kum approach mteja...
Ningeweka my contact hapa, but shida kidogo yeye ani pm namba yake ntampigia kumpa msaada to the best of my knowledge free of charge.

Kama kuna kosa basi sorry sana.

Namna ya attend cooling system issues sometimes inakua ina depend na design ya cooling system..so commenting general comments kwenye kitu probably kinahitaji specific comment ni muhimu kuwasiliana na mtoa mada husika au kuona gari ili kuona valid comment inayo endana na prevailing situation.
 
Mimi gari yangu Mark II 110 engine JZX110 2.5. Tatizo langu ni gari ikishawaka nikatembea kwa muda kama dakika 5 nikisimama hata kwenye taa nikianza kuondoka kuna sauti flani inajitokeza kama crrr nikikanyaga mafuta zaidi inapotea sijui tatizo ni nini Naomba unisaidie
 
Ni zaidi ya km 10000, hadi mlio wa gari ukaanza kuchenj, siku naibadili nikakuta ukoko kabisa umeganda nikafungua sample tukakwatua woote na kusafisha tukaweka ingine iliyoliwa
Kwa hiyo hata kuchek oil ulikuwa huchek?? Mbona ni mzembe hivyo,?
 
Kwa hiyo hata kuchek oil ulikuwa huchek?? Mbona ni mzembe hivyo,?
Sasa ningejuaje km oil imeisha,. Afu sio uzembe..... Utaratibu wa kila ukiamka unadip stick kupima oil kila siku sio good aiseee,. Gari mpya unaikagua kagua nini..... Dashb board ipp kukupa maelekezo
 
Mkuu kwa kipindi hiki ambacho gari imeua gasket seal, piston na cylinder head...

Inatembea ila kuna time inatoa moshi mwingi saana.

Je naweza kuitembelea hivi hivi bila madhara ypyote!?

Na kuna njia gani ya kupunguza huu moshi?


Maaana nahitaji saana matumiz ya gari huku nikijichanga kununua mswaki
 
Samahani wadau iv normal temperature gauge ya gari inatakiwa iweje,je iwe katikati au iwe chini ya katikati?
 
Karibu tena kwa huduma mkuu... hope una enjoy gari yako sasa baada kulitibu. Na asante kwa kutuamini.
 
Nahitaji gia boksi ya Toyota Townace van - automatiki.
Maelezo yake ni:

Make: Toyota
Model: TOWNACE
Model number: KR26
Year: 2005
Transmission : Automatic
Chassis no: KR4250045318
Engine no: GKKR42V
Engine type: 7K
 
Ni sahihi kwa gari lenye engine ya 5A FE kutumia oil ya 5W30 Fully synthetic? Kama jibu ni ndiyo, je itembee kilometer ngapi hadi next service? Natanguliza shukurani
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…