Niulize chochote kuhusu injini za magari madogo na pickup zinazotumia Petroli

Niulize chochote kuhusu injini za magari madogo na pickup zinazotumia Petroli

Nini maana ya vvti

Sent using Jamii Forums mobile app

Variable Valve Timing with intelligence (VVT-i) ni mfumo wa kufungua valve za intake na exhaust kwa kuruhusu ufunguaji wa valves kadhaa kuingiliana ili kuongeza ufanishi katika utendaji wa injini husika. Valve timing ya kawaida ambamo camshaft inafungua valve kutokana na timining iliyoweka kwa kutumia timing belt kila valve inafunguka kwa mtindo ule ule. VVT-i inabadilisha timing hiyo kwa kutumia hydraulic pressure kubadilisha timing position ya camshaft kulingana na spidi ya injini.
 
Engine check ya Harrier kuwaka bila hitilafu kwenye Engine. Nini la kufanya?
Haiwezi kuwaka bila hitilafu mkuu..mm nifundi umeme nakuhakikishia haiwezi kuwaka bila kuwa na hitilafu hiyo ni sign kwamba kuna mambo kwenye engine hayajakaa sawa
 
Variable Valve Timing with intelligence (VVT-i) ni mfumo wa kufungua valve za intake na exhaust kwa kuruhusu ufunguaji wa valves kadhaa kuingiliana ili kuongeza ufanishi katika utendaji wa injini husika. Valve timing ya kawaida ambamo camshaft inafungua valve kutokana na timining iliyoweka kwa kutumia timing belt kila valve inafunguka kwa mtindo ule ule. VVT-i inabadilisha timing hiyo kwa kutumia hydraulic pressure kubadilisha timing position ya camshaft kulingana na spidi ya injini.
Mkuu hapo kwenye exhaust valve ni gari chache sana ndio hufungwa OCV switch kwenye camshaft ya exhaust..nyingi huwa kwenye inlet valve peke yake
 
Kuna faida gan na madhara yoyote ya kutoa thermostat kwenye gari?
Mambo mengi yanawezekana inategemea utaweka nini badala yake. Ukiondoa na kuacha njia ya coolant wazi, basi injini itakuwa nzito kwani haitafikia joto la kufanya kazi sawasawa, na inaweza kusaga piston rings zake na cranckshaft bearings zake haraka sana, na kuhitaji overahaul. Ukiondoa na kuziba kabisa tundu lake, basi injini itachemsha na kuweza kusababisha engine block au cylder head ipasuke.

Kwa nini uondoe thermostat kwanza? Ni kitu cha bei ndogo sana isiyozidi dola 7.
 
Juzi gari niliweka idle kwa dk kama 30 then baadae Engine ika heat kidogo but kwenye dashboard alama ya temp haiku display, but kwenye tank la maji ya reserve maji yakawa yanatoka then kufungua mfuniko wa rejeta maji yakawa yamepungua kidogo so fundi aka suggest tutoe thermostat
 
Tatizo lako linaweza kuwa na vyanzo vingi kidogo. Kama dashboard gage ya joto haikuwa imezidi, basi inawezekana injini ilikuwa haija-overheat.
(a) Je, ulifungua rejeta wakati injini ikiwa ya moto au baada ya kupoa? (b) Je kwenye coolant reservoir kulikuwa na mapovu (bubbles)? (c) Je mlipotoa thermostat mliweka nini na kulitokea nini kwenye utendaji wa gari?(yaani gage ya joto iliongezeka hadi kufikia nusu au ilibaki palepapale)?
 
thermostat hatujaitoa bado but fund alisema tuitoe baada ya kumweleza hilo tatzo. na hilo tatizo limetokea baada ya kuweka gari idle kwa muda mrefu kama dk 30 ikiwa idle haitembei. Mfuniko wa rejeta nilifungua baada ya kama dk 10 na kwenye coolant reservoir kulikuwa na maji yanatoka kwa kasi na pia ukiweka gari idle kwa muda mrefu lazma lipate ipate moto? gari ni TOYOTA IST
 
Nasita kukupa jibu la moja kwa moja kwani bado naona uwezekano wa kuwepo kwa majibu mengi; ngoja tuanze na lile linalooneka kuwa na yamkini kubwa. Je ukishaanza kuendesha katika mwendo wa kawaida baadaye injini inarudi katika hali yake ya kawaida? Iwapo ni hivyo basi thermostat siyo mbaya ila inawezekana radiator yako ina kutu imeanza kuziba, kwa hiyo iwapo gari haitembei, upepo unaopuliza hautoshi kupooza injini mpaka uwe katika spidi ya kuvuta upepo mwingi. Je huwa unaweka maji ya bomba au maji yale ya kijani? Maji ya bomba huleta kutu haraka sana kwenye raditor. Mwambie fundi wako aikague radianto aone kama inahitaji kuflush. Vile vama gari ina feni ya umeme inawezekana fuse ya feni yako imekufa kwa hiyo feni haifanyi kazi kabisa ya kupuliza kwenye radiator yako, na kama feni inaendeshwa kwa mkanda, basi inawezekana mkanda umechoka; injini nyingi siku hizi hutumia feni za umeme, kagua fuse ya feni.
 
Gari yangu toyota raum 2003 nitumie mpaka sasa 52000km nitumie oil gani (engine & gearbox)

Sent using Jamii Forums mobile app
Engine 10W-30, na iwapo gearbox ni ya manual basi 80W-90, na kwa gearbox ya automatic soma kitabu chake. Kila gearbox ya automatic ina mafuta yake, kwa gari ya Toyota inawezekana ni Type T-IV lakini soma kitabu kwanza.
 
Inapofikisha angalau kilometa ngapi, tuhesabu injini ya pick up imeshachoka

Sent using Jamii Forums mobile app

hakuna jibu moja; injini inaweza kuchoka hata bila kutembea kilomita nyingi, na vile vile gari inaweza kuwa imetembea kilomita nyingi bila injini kuchoka. Injini ya gari inayoendeshwa kwenye barabara zenye foleni sana kama mijini huchoka mapema ikiwa na kilomita chache tu kuliko gari inayotumika kwenye ruti ndefu za kwenye highway bila kusimamasimama.

Vile vile injini ya gari ambayo haifanyiwi service kwa wakati wake itachoka mapema sana kuliko injini ambayo hufanyiwa service sawasawa hata kama magari hayo yanatumiwa katika mazingira yanayofanana. Na mwisho gari ambayo hutumika kubebea mizigo mizito mara kwa mara huchoka mapema kuliko ile isiyobeba mizigo.

Kwa hiyo hakuna jibu moja kwenye swali lako. Gari iliyotumika vizuri huanza kuhesabiwa kuchoka ikifika km 225,000 ila hata hivyo ikiendelea kupewa matunzo mazuri inaweza kuendelea hadi hata kufikia km400,000.
 
Gari ya jamaa yangu (Oppa) mguu wa kulia mbele unachemka sana, amesahuriwa kubadili master cylinder lakini haijasaidia, naomba umsaidie ushauri maana yeye si mtu wa mitandaoni.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Gari ya jamaa yangu (Oppa) mguu wa kulia mbele unachemka sana, amesahuriwa kubadili master cylinder lakini haijasaidia, naomba umsaidie ushauri maana yeye si mtu wa mitandaoni.

Sent using Jamii Forums mobile app

tatizo lake ni dogo sana, ile brake caliper haina grisi inayotakiwa. Kuna gris maalumu ya brake anatakiwa aiweke. Overheating hutokea baada ya kukanyaga brake zinakuwa hazirudi mpaka mwisho, kwa hiyo gari linatembea wakati brake imeshika nusu.
 
Back
Top Bottom