Niulize chochote kuhusu injini za magari madogo na pickup zinazotumia Petroli

Niulize chochote kuhusu injini za magari madogo na pickup zinazotumia Petroli

Asante kwa majibu Mkuu, nitaendelea kukutafuta pindi nitakapohitaji ushauri
hakuna jibu moja; injini inaweza kuchoka hata bila kutembea kilomita nyingi, na vile vile gari inaweza kuwa imetembea kilomita nyingi bila injini kuchoka. Injini ya gari inayoendeshwa kwenye barabara zenye foleni sana kama mijini huchoka mapema ikiwa na kilomita chacvhe tu kliku gari inayotumika kwenye ruti ndefu za kwenye highway bila kusimamasimama. na

Vile vile injini ya gari ambayo haifanyiwi service wakati wake itachoka mapema sana kuliko injini ambayo hufanyiwa service sawasawa hata kama magari hayo yanatumiwa katika mazingira yanayofanana. Na mwisho gari ambayo hutumika kubebea mizigo mizto mara kwa mara huchoka mapema kuliko ile isiyobeba mizigo.

Kwa hiyo hakuna jibu moja kwenye swali lako. gari iliytumika vizuri huanza kuhesabiwa kuchoka ikifika km 225,000 ila hata hivyo ikiendelea kupewa matunzo mazuri inaweza kuendelea hadi hata kufikia km400,000.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Gari yangu asubuhi inawaka single kick ukiitumia baada ya muda ukazima halafu ukae dk nyingi kiasi inawaka kwa taabu hadi unasaidia kwa acc pedal. Tatizo nini ni petrol engine suzuki escuodo

Sent using Jamii Forums mobile app
Kuna sababu kadhaa zinazsababisha matatizo ya namna hiyo; tatizo ambalo ni la kawaida mara nyingi sana ni kuwa ile distributor yako inaweza kuwa imepasuka na inaingiza oil. Ukiiacha kwa mda mrefu sana ile oil inapungua. tatizo la pili ni kwamba huenda crack position sensor yake haifanyi kazi sawasawa, na tatizo la tatu ni fuel pressure regulator inaweza kuwa imeanza kuchoka haiweki mafuta ya kutosha kwenye injini ikiwa ya moto. Mwambie fundi wako akukagulie sehemu hizo tatu. kama zote ziko sawa tuwasiliane tena, vile vile niambie model ya gari na mwaka, kwani technology za magari zitotautiana kwa miaka tofauti.
 
Asante. Mkuu hii ni Suzuki grand escuodo v6 LA TX92W Engine H27A ya mwaka 2002.
Fundi amesikikiza na kuwasha a.eniambia
1. Hilo ni tatizo la pump eti ikipata moto inapungua pressure
Halafu kuna mlio unalia kedekedekede nao ameniambia timing chain pia imeisha

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Asante. Mkuu hii ni Suzuki grand escuodo v6 LA TX92W Engine H27A ya mwaka 2002.
Fundi amesikikiza na kuwasha a.eniambia
1. Hilo ni tatizo la pump eti ikipata moto inapungua pressure
Halafu kuna mlio unalia kedekedekede nao ameniambia timing chain pia imeisha

Sent using Jamii Forums mobile app
Inaweza kuwa ni kweli kwamba fuel pump imeishiwa nguvu, lakini hali hiyo iknapotokea basi gari lako haliwezi kuwa na nguvu kupanda milima au kwenda mwendo kasi. Iwapo gari likishaanza linakwenda bila tatizo lolote hadi pale utakapolizima, wasiwasi mkubwa sana unakuwa ni fuel pressure regulator; kuna magari ambayo fuel pressure regulator imejengewa ndani ya pump hivyo unapotaka kuibadilisha ni lazima ubadili pump yote. Kuhusu timing kuchoka siweze kukuambia mpaka niikague mwenywe. Hata hivyo magari mengi yakianza kupoteza timing lazima taa ya check engine itawaka. Kama taa inawaka na fundi wako amepitisha ile computer yake akaona hivyo basi rekebisha mapema isijekuletea ,majanga makubwa; vinginevyo inawezekana ni tappet moja haifunguki vizuri na hivyo unapata misfire kali sana, jambo ambalo ni rahisi kurekebisha kwa kuondoa cylinder head tu badala ya timing belt ambayo ni kazi kubwa kidogo kubadilisha. Hata hivyo kukiwa na misfirie pia lazima taa itakuonyesha, na utaisoma .kwa kutumia computer scan. Utaalamu wa magari unashauri kuwa ukibadilisha timing belt, lazima pia ubadilishe water pump na idler pulley kwa pamoja.

Halafu sikuangalia kuwa uliandika kuhusu timing chain; jibu langu hapo juu lilikuwa ni kwa timing belt. Magari mengi sana (sehemu kubwa) yenye timing chain huwa hazibadiliswi mpaka gari linakuwa written off; labda kama gari hilo halifanyiwi service sawasawa linatumia oil nzito za SAE50. Nimetafuta kitabu cha Escudo sikukipata, lakini nadhani pia nayo hayabadilishwi timing chain kabisa.
 
mkuu mimi natumia Toyota ist juzi nimeweka nimeweka 20w50. vipi hyo 5W30 itanifaa mkuu??
Wengi wanakosea hapa wanaweka 20w50 mm mwenyewe kina kipindi niliambiwa na fundi wa mtaani niiweke gari ikabadilika ikawa inatoa vimlio wa ajabu ila nilivyoconsult manual na kuanza kutumia 5w30 aisee limetulia sometime unaweza hisi halijawaka..

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Je? Ni double cabin nzuri kwaajiri ya sehemu ambazo hakuna barabara za lami off-road use hasa milimani nasehemu zenye miinuko

Sent using Jamii Forums mobile app
Inategemea ni double cabin gani; ukiwa na Ford F150 au RAM 2500 utapanda hata mlima Kilimanjaro.
1577761372356.png

1577761534632.png
 
Aisee mafundi watatuulia magari yetu. mkuu unashauri nitumie oil namba ngapi kwa toyota ist ina km kama 56000??

Sent using Jamii Forums mobile app
IST tumia 5w30...ukiikosa tumia 10w30....ukitumia moja ya hizi oil nilizokuandikia hata gari lako utalisikia limekuwa jepesi.
Kwa upande wa gear box angalia pale kwenue deep stick watakuwa wamekuandikia..

Asilimia kadhaa naona ist wanatumi t- iv lakini hao hao wamiliki wenyew wakija utasikie nipe atf ya bei rahisi sijui nani ameturoga sisi watanzania na vitu rahisi rahisi na Mara nyingi atf rahisi zinakua hazina ubora na viwango vya kukidhi gearbox yako

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Inaweza kuwa ni kweli kwamba fuel pump imeishiwa nguvu, lakini hali hiyo iknapotokea basi gari lako haliwezi kuwa na nguvu kupanda milima au kwenda mwendo kasi. Iwapo gari likishaanza linakwenda bila tatizo lolote hadi pale utakapolizima, wasiwasi mkubwa sana unakuwa ni fuel pressure regulator; kuna magari ambayo fuel pressure regulator imejengewa ndani ya pump hivyo unapotaka kuibadilisha ni lazima ubadili pump yote. Kuhusu timing kuchoka siweze kukuambia mpaka niikague mwenywe. Hata hivyo magari mengi yakianza kupoteza taiming lazima taa ya check engine itawaka. Kama taa inawaka na fundi wako amepitisha ile computer yake akaona hivyo basi rekebisha mapema isijekuletea ,majanga makubwa; vinginevyo inawezekana ni tappet moja haifunguki vizuri, na hivyo unapata misfire kali sana, jambo ambalo ni rahisi kurekebisha kwa kuondoa cylinder head tu badala ya timing belt ambayo ni kazi kubwa kidogo kubadilisha. Hata hivyo kukiwa na misfirie pia lazima taa itakuonyesha, na utaisoma .kwa kutumia computer scan. Utaalamu wa magari unashauri kuwa ukibadilisha timing belt, lazima pia ubadilishe water pump, na idler pulley kwa pamoja.

Halafu sikuangalia kuwa uliandika kuhusu timing chain; jibu langu hapo juu lilikuwa ni kwa timing belt. Magari mengi sana (sehemu kubwa) yenye timing chain huwa hazibadiliswi mpaka gari linakuwa written off; labda kama gari hilo halifanyiwi service sawasawa linatumia oil nzito za SAE50. Nimetafuta kitabu cha Escudo sikukipata, lakini nadhani pia nayo hayabadilishwi timing chain kabisa.
kwanini ukibadili timing belt lazima pia ubadili water pump na idle pulley? na je kama water pump na pulley ni nzima?
 
kwanini ukibadili timing belt lazima pia ubadili water pump na idle pulley? na je kama water pump na pulley ni nzima?

Vinakufa katika kipindi kimoja ingawa vifo vyao vinaweza kutofautiana kwa kama miezi miwili hivi, lakini idadi ya mizunguko (cycles) yao kabla kuishiwa nguvu ni ile ile. Kwa magari mengi kazi ya kufungua injini ubadilishe timing belt ni sawa kabisa na kazi ya kufanya hivyo kubadili water pump. Kwa hiyo badala ya kurudia kazi hiyo hiyo baada ya muda wa miezi miwili tu, ni afadhali kuifanya mara moja tu kwa kubadili vyote.
 
mkuu naomba kujua oil nzur ya mark 2 gx 90,1G kavu ya mwaka 1994.ahsante

Sent using Jamii Forums mobile app
Milage na matunzo yake yako vipi. Kama ina kilomita zaidi ya 300,000 na haikuwa na matunzo mazuri huko nyuma basi tumia SAE 40 tu. Chini ya hapo bado nitakushauri utumie 10W-30 tu; in fact injini za 1G zilikuwa nzuri sana kuliko injini za magari madogo ya Toyota zilizofuata.
 
Ni zaidi ya 300,000 mkuu.Haikua na matunzo mazur! Je nikitumia 5w-30 nini kitatokea???

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom