Niulize chochote kuhusu injini za magari madogo na pickup zinazotumia Petroli

Niulize chochote kuhusu injini za magari madogo na pickup zinazotumia Petroli

Ningependa kujua je kuna ulazima wa gari iliyotembea umbali mrefu kuachwa katika idle position kwa muda fulani kabla ya kuzimwa?

Na kama ulazima upo, gari iwe udle kwa mda gani, na baada ya kutembea kwa umbali kuanzia km ngapi/masaa mangapi?
Naomba nikujibu ni kwamba kama gari yako ina mfumo wa turbo then better ukitembea umbali mrefu ukishafika subiria kidogo dakika at 10 hadi 15 ndipo uizime....
 
Naomba kuelekezwa Toyota IST toleo la injini bora. Kuna hii ya 1NZ 1.5s, 1NZ 1.5 L edition na kuna ile ya 2NZ 1.3F L edition.

Kwa kifupi sijajua tofauti ya hizi engine za IST, ubora na performance yake kiutendaji.

So naomba tushauriane.
 
Chief samahani, naweza funga engine ya Mercedes Benz 102 kwenye cresta gx 100?

Sent from my itel it1508 using JamiiForums mobile app
Nenda Geartech Performance wapo Kijitonyama. Hapo utakutana na mjapani mwenyewe bingwa wa kufanya modifications, mapping za gari mbalimbali.

Screenshot_20200718-103930.png
 
Kina fobs ambazo ni programmable na kuna ambazo siyo programmable. Kama yako siyo programmable, una kazi kuwa sama ya kutafuta fob nyingine inaiyfanana kabisa, ila kswa babu za kiuslama, unaweza kukuta fob inayofanana na yako iko continent nyingine kabisa. Progrmmable ni raisi sana, wewe nunua yoyote ile umplekee mwenye compute ya kuprogram hizo fobs, holla!
Thanks mkuu. Itabidi nifanye hii
 
Habari mkuu,

Naomba kujua, gari yangu ilikaa bila kufanya kazi kwa miaka2 nimekuja kuiwasha naona rivers inakoswa nguvu .
Tatizo ni nini?

Msaada tafadhari.
 
Mkuu gari inawasha taa ya check ingine lakini ukizima gar na kuiwasha ukatembea kama km1 inawaka tena taa shida itakua n nn?
 
Mkuu gari inawasha taa ya check ingine lakini ukizima gar na kuiwasha ukatembea kama km1 inawaka tena taa shida itakua n nn?
Peleka wakupigie computer scan. Kuna sababu nyingie sana zinazosbabisha taa kuwaka; nyingie haziathiri injini kabisa na nyingine ni hatari sana kwa gari lako.
 
Habari mkuu,

Naomba kujua, gari yangu ilikaa bila kufanya kazi kwa miaka2 nimekuja kuiwasha naona rivers inakoswa nguvu .
Tatizo ni nini?

Msaada tafadhari.

Transmission. Inawezekana kabla ya gari kusimama lilikuwa limeshakula sana clutch plates za transmission na sasa baada ya kukaa, kuna plates zilikauka na hivyo hazishiki tena. Unahitaji kukaguliwa transmission yako yote; njia ya kuanzia ni kuweka mafuta mapya ya transmission, lakini jibu halisi ni pale transmission yote itakapoguliwa
 
Mkuu salama?
Nina gari Suzuki grand escuodo ya 2001 H27. Ilianza tatizo la kutowaka taa ya 4WD ukiingiza, fundinakaunga direct. Baadae tena silencer inakuwa chini kila mara hata ukiiongezea, tena ikiwashan AC inashuka badala ya kupanda, tatizo linaongezeka kila kukicha, mafundi wananiambia wakachezea na control box kuna umeme hauji eti kwenye sensor.

Pia inapoteza nguvu, hili huenda kwa ajilibya catalytic converter kutolewa unga niliwahi kukuuliza sijapata nyingine. Je, shida ya rpm kushuka hadi gari kuwa inazima nini tatizo?
 
Suspect mkubwa ni kuwa huenda alternator yako imekufa; waambie mafundi wakague alternator yako kwanza kabla ya kuanza kuingia mambo mengine ya gharama kubwa. Kama siyo alternator yenyewe, huenda mkanda unaoendesha alternator yenyewe umelegea ingawa hili likitokea utakuwa unaskika mlio wa mkanda kuteleza.
 
Transmission. Inawezekana kabla ya gari kusimama lilikuwa limeshakula sana clutch plates za transmission na sasa baada ya kukaa, kuna plates zilikauka na hivyo hazishiki tena. Unahitaji kukaguliwa transmission yako yote; njia ya kuanzia ni kuweka mafuta mapya ya transmission, lakini jibu halisi ni pale transmission yote itakapoguliwa

Gari yangu ni automatic, situmii clutch, ni mark2 vvti mkuu. Labda ckujiekeza vzr, harafu nguvu inakosekana kwa rivers tu, lakini mbele haina tatizo.
 
Gari yangu ni automatic, situmii clutch, ni mark2 vvti mkuu. Labda ckujiekeza vzr, harafu nguvu inakosekana kwa rivers tu, lakini mbele haina tatizo.
Clutch ya manual ikifa itakusababisha uwe na ugumu wa ku-engage gia zako tu lakini ukishengage, gari litakwenda tu; na manual zina clutch plate moja tu. Ukijaribu kubadili gia utasikia kelele za mkwaruzo. Ndani ya automatic transmission kuna clutch plates nyingi sana kuliko gari ya manual, kila namba ya gia ina clucth plates zake.

Zile huwa zinakufa pia. Kufa kwa transmission huanza kwa kupoteza gia moja halafu itapoteza gea nyingine na mwisho inapoteza zote. Una bahati kuwa ya kwako imeanza kwa kupoteza gia ya nyuma; ingeanza kwa kupotzea gia ya kwanza usingeweza hata kutoka hapo uliko. Ikifa gear ya pili, utaona gari lako linatembea lakini haliwezi kuongeza spidi hata ukikanyaga acceletor pedal mpaka kwenye bati.
 
  • Thanks
Reactions: Cyb
Suspect mkubwa ni kuwa huenda alternator yako imekufa; waambie mafundi wakague alternator yako kwanza kabla ya kuanza kuingia mambo mengine ya gharama kubwa. Kama siyo alternator yenyewe, huenda mkanda unaoendesha alternator yenyewe umelegea ingawa hili likitokea utakuwa unaskika mlio wa mkanda kuteleza.
Inawezekana alternator i fail na gari iwake niwashe taa si betri ndio itatumika? Na temp itapanda?
 
Inawezekana alternator i fail na gari iwake niwashe taa si betri ndio itatumika? Na temp itapanda?
Nimekupa ushauri kulingana uzoefu wangu, usipokubaliana nao basi achana nao hasa ukizingatia kuwa sijakagua gari lako. Betri huwa inajaza nguvu kubwa sana ambayo hukatwa mara moja baada ya gari kustati.

Zamani kulikuwa na kitu kinaitwa"katauti" ili injini ijiendeshe yenyewe kutoka kwenye alternator; siku hizi computer ya injini ndiyo inayokata betri. Kama hubaliani nami jaribu kutafuta sehemu nyingine jibu sahihi ila uhakikishe kuwa mtu anakagua gari lako phyisically.

Magari mengine yana capacitor fulani kwenye alternator, huenda ndiyo inaweza kuwa imekufa; kwa jumla tatizo lako lote linatoka kwenye alternator. Ukipata solution ilete hapa tuijadili. Amini kuwa baada ya muda kidogo gari itaanza ksuhindwa kustart.
 
Nimekupa ushauri kulingana uzoefu wangu, usipokubaliana nao basi achana nao hasa ukizingatia kuwa sijakagua gari lako. Betri huwa inajaza nguvu kubwa sana ambayo hukatwa mara moja baada ya gari kustati. Zamani kulikuwa na kitu kinaitwa"katauti" ili injini ijiendeshe yenyewe kutoka kwenye alternator; siku hizi computer ya injini ndiyo inayokata betri. Kama hubaliani nami jaribu kutafuta sehemu nyingine jibu sahihi ila uhakikishe kuwa mtu anakagua gari lako phyisically.
Kiongozi sijakataa ushauri ni mawazo nilikuwa nawaza, na huenda kuna ukweli maana taa za fog zimekuwa mara siwake mara zizime, asubh gari in start fasta ila baada ya kuendesha inasumbua mpaka ukanyagie.

Asante mkuu ingekuwa uko Tanzania halafu Dar ningekuona
 
Nimetest spark plag mbili kwenye gari hazichomi,nikatest na nozeli mbili za plag hizo hazifanyi kazi pia.Swali he hii linaweza kuwa tatizo la ulaji wa mafuta kiongozi?
 
Nimetest spark plag mbili kwenye gari hazichomi,nikatest na nozeli mbili za plag hizo hazifanyi kazi pia.Swali he hii linaweza kuwa tatizo la ulaji wa mafuta kiongozi?
ndiyo; tena sana. zibadilishe hizo spark plugs na injector nozels ambazo hazifanyi kazi. Zitakuletea matatizo makubwa sana kwnye injini ako hukombeleni.
 
Samahani mkuu kichuguu nikwanini gari ukitoka kuliwasha linatoa moshi mwingi kwenye exhaust halafu likichanganya moshi unapotea?
 
Back
Top Bottom