Niulize chochote kuhusu injini za magari madogo na pickup zinazotumia Petroli

Niulize chochote kuhusu injini za magari madogo na pickup zinazotumia Petroli

Pia gari likiwa likiwa linatoa moshi mweupe hii husababishwa na nini? Pia gari kuwaka halafu engine inakuwa inatetemeka sanaaaa hili nalo linatokana na nini?
 
Mkuu Kichuguu kuna gari hapa aina ya Toyota vitz new model 2005 push to start inasumbua Sana,huwa inazima yenyewe wakati unatembea au kubadilisha gear kwenda reverse au drive. Pia ukiendeshha umbali mfupi kidogo huanza kumiss fire na kushake shake Kisha huzima unakanyaga break unaweka parking ukiwasha linawaka then unatembea halaf hali hujirudia tena baada ya muda. Ila wakat likizima ukiwasha naskia harufu Kali ya oil au petrol ndan ya gar then inapotea naendelea...
Gari ina matatizo mengi sana. Kwa kuanzia kabisa inawezekana pia unaiverload transmission yake kama ilikuwa optimized kwa 990cc lakini sasa unaiendesha kwa 1290cc ambao ni kama 30% overload.

Hiyo overload huweza kuwa inaifanya computer ya transmission kuzimisha gari. Mambo mengine, inawezekana una timing mbaya, yaani timing belt imeshalegea; hiyo inasababisha miss nyingi na vibrations ambazo huzimisha injini.

Baadaye angalia vitu vingine kama injectors na sparkplugs, lakini hizi zikiwa na matatizo huwa yako persistent, siyo ya kutokea vipindivipidi tu kama unavyosema. harufu ya mafuta ni kwa sababu ya misfire, hivyo kunamfuta yanapita bila kuchomwa
 
Gari ina matatizo mengi sana. Kwa kuanzia kabisa inawezekana pia unaiverload transmission yake kama ilikuwa optimized kwa 990cc lakini sasa unaiendesha kwa 1290cc ambao ni kama 30% overload...
Mkuu kichuguu nimeku pm nasubiri msaada wako
 
Write your reply...Nimekukubali Dogo,Wewe ni mtaalam,

Nina Toyoa harrier ya 2000,inaanza sasa kunipa shida mwenye km 190000.Nikiwasha gari Taa ya low oil pressure inawaka,Nikikanyaga pedal nikiwa kwenye idle inazima.

Nikiendesha almost 30 km inawaka tena na engine inachemka.Oil pump inafanya kazi ,ila inaonyesha oil inapungua kwa kasi kwenye sump,pia napocheki maji kwenye radiator nayo yanapungua,water hose pipe zinajaa pressure,ikiwa kwenye joto.

Fundi kasafisha kichujio cha oil lakini bado tatizo lipo, nashauriwa ninunue balance shaft maana haimo kwenye engine ya hiyo 5s kwamba itasaidia kuongeza oil pressure, je nisahii kichuguu?
 
Habari, nina toyota hilux 3l(diesel engine). Ina tatizo la unapotaka kuiwasha ina crank kwa muda mrefu sana ndio inawaka. Battery za gari gari nimezikagua ni nzima kabisa. Na gari ikiwaka inanguruma vizuri wala hakuna sauti ya ajabu. Gari service inafanywa kwa wakati na saa ingine huwa nawahi kwa hata km 1000 kabla
 
Habari, nina toyota hilux 3l(diesel engine). Ina tatizo la unapotaka kuiwasha ina crank kwa muda mrefu sana ndio inawaka. Battery za gari gari nimezikagua ni nzima kabisa. Na gari ikiwaka inanguruma vizuri wala hakuna sauti ya ajabu. Gari service inafanywa kwa wakati na saa ingine huwa nawahi kwa hata km 1000 kabla
Sina uzoefu sana wa magari ya dizeli, ila inawezekana kuwa piston ring zako zimeanza kuchoka. kwa hiyo hazijengi pressure ya kutosha kuunguza mafuta ya dizeli wakati injini bado ni ya baridi. Waambie mafundi wako wakupimie compression test.
 
Write your reply...Nimekukubali Dogo,Wewe ni mtaalam,
Nina Toyoa harrier ya 2000,inaanza sasa kunipa shida mwenye km 190000.Nikiwasha gari Taa ya low oil pressure inawaka,Nikikanyaga pedal nikiwa kwenye idle inazima...
Oil pressure sensor imechoka; badilisha. Haina madhara sana kwenye injini ila inaweza kusababisha tatizo la ghafla sana wakati kweli hakuna oil lakini wewe ukadhani kuwa ndivyo ilivyo.
 
Mkuu kichuguu gari ni passo ilikuwa inaleta taa ya check engine baadae ikaleta taa nyekundu gari ikazima mafundi wakasema imeua engine ikanunuliwa engine mpya Ila modern ileile ikafungwa haina hata wiki bado taa ya check engine inawaka sasa hapo shida ni nini na solution ni opinion?
 
Oil pressure sensor imechoka; badilisha. Haina madhara sana kwenye injini ila inaweza kusababisha tatizo la ghafla sana wakati kweli hakuna oil lakini wewe ukadhani kuwa ndivyo ilivyo.
Mtaalam,oil pressure sensor itatatua hata tatizo la kuoverheat engine huku vilevile hoses zikijaa upepo na kunyonya oil isivyo kawaida? Msaada mtaalam.
 
Mtaalam,oil pressure sensor itatatua hata tatizo la kuoverheat engine huku vilevile hoses zikijaa upepo na kunyonya oil isivyo kawaida? Msaada mtaalam.
Swali lako lilihusu taa ya oil pressure halikuhusu engine overheat. Nitakusaidia sana iwapo ukiuliza swali utoe taarifa kamili kwani matatizo ya gari yako kama web ya buibui; yameungana sehemu nyingi sana. Ukisahau kueleza sehemu mojawapo basi unaweza kuishia kwenye kona ambayo hukutegemea.

halafu mimi siyo dogo; ni kichuguu. Nilikuwa TPDF wakati wa vita ya kagera, kwa hiyo siwezi kuwa dogo leo.
 
swali lako lilihusu taa ya oil pressure halikuhusu engine overheat. Nitakusaidia sana iwapo ukiuliza swali utoe taarifa kamili kwani matatizo ya gari yako kama web ya buibui; yameungana sehemu nyingi sana. Ukisahau kueleza sehemu mojawapo basi unaweza kuishia kwenye kona ambayo hukutegemea.

halafu mimi siyo dogo; ni kichuguu. Nilikuwa TPDF wakati wa vita ya kagera, kwa hiyo siwezi kuwa dogo leo.
Samahani sana kwa hilo la kukuita dogo mkuu post yangu ya awali nilijieleza kuwa ninaposwitch on taa ya onyo kwa low oil pressure haizimi hadi napokanyaga accelerator engine ikiwa idle.

Nikiendesha umbali kama 30 km taa inawaka na pia engine inaoverheat ikiambatana na hose ya radiator kujaa upepo.cooling system na lublication system zimepitiwa na fundi na pumps zinazohusika kwenye system zinafanya kazi.

Radiator imefanyiwa usafi bado tatizo ni lile lile.Fundi anashauri labda ku re install balance shaft ambayo iliondolewa siku za nyuma.Msaada tafadhari.
 
Samahani sana kwa hilo la kukuita dogo mkuu post yangu ya awali nilijieleza kuwa ninaposwitch on taa ya onyo kwa low oil pressure haizimi hadi napokanyaga accelerator engine ikiwa idle.Nikiendesha umbali kama 30 km taa inawaka na pia engine inaoverheat ikiambatana na hose ya radiator kujaa upepo.cooling system na lublication system zimepitiwa na fundi na pumps zinazohusika kwenye system zinafanya kazi. Radiator imefanyiwa usafi bado tatizo ni lile lile.Fundi anashauri labda ku re install balance shaft ambayo iliondolewa siku za nyuma.Msaada tafadhari.
Kumbe uliuliza maswali mengi ila mimi nilijibu moja tu; ni kosa hilo hilo kuwa ulikata swali katika vipande vipande nadhani ukitegemea kuwa nitakumbuka kuwa nimeshakujibu kule; hapana, siweki kumbukumbu hizo.

Kila swali nalijibu pale pale lilivyo, labda kama ungenikumbusha kuwa hilo ni swali la nyongeza kutokana na jibu langu la awali. Sasa nifanyie favor; andika swali lako lote upya katika post moja tu kusudi niweze kuliewa sawasawa na kulijibu vizuri kadri ya uwezo wangu.
 
Kumbe uliuliza maswali mengi ila mimi nilijibu moja tu; ni kosa hilo hilo kuwa ulikata swali katika vipande vipande nadhani ukitegemea kuwa nitakumbuka kuwa nimeshakujibu kule; hapana, siweki kumbukumbu hizo. Kila swali nalijibu pale pale lilivyo, labda kama ungenikumbusha kuwa hilo ni swali la nyongeza kutokana na jibu langu la awali. Sasa nifanyie favor; andika swali lako lote upya katika post moja tu kusudi niweze kuliewa sawasawa na kulijibu vizuri kadri ya uwezo wangu.
Ahsante mtaalam,nina toyota harrier 5s engine ya 2000, km 189000.Imeanza tatizo la kuchemsha baada ya kuwa kwenye mwendo wa km 30 hivi.Kuchemka huko kunaambatana na taa inyoonyesha kwamba engine ina low pressure ya oil.Fundi kakagua system zote mbili lubrication na cooling ,amegundua pump zote zinafanya kazi.

Radiator imesafishwa lakini haijasaidia kuondoa tatizo.wakati wa kuchemka water hose zinajaa hewa na pia oil na maji vinamezwa isivyo kawaida.Fundi anashauri ni reinstall balance shaft kwani haimo ila thermostart inafanya kazi.Samahani naweza kushindwa kunyoosha maelezo kwa vile sina ujuzi na chombo husika.Naomba msaada wako pse.
 
Ahsante mtaalam,nina toyota harrier 5s engine ya 2000, km 189000.Imeanza tatizo la kuchemsha baada ya kuwa kwenye mwendo wa km 30 hivi.Kuchemka huko kunaambatana na taa inyoonyesha kwamba engine ina low pressure ya oil.Fundi kakagua system zote mbili lubrication na cooling ,amegundua pump zote zinafanya kazi...
Kwanza kabisa badilisha cylinder head gasket; hiyo ndiyo inayokuletea matatizo yote hayo na inatakiwa ifungwe vizuri kwa kutumia ile seeal yake nyekundu. Vile vile kagua kama cylinder head and engine block zina nyufa. Baada ya hapo ndipo tunaweza kuanglia ni vitu gani vingine vishaathirika.
 
Back
Top Bottom