Niulize chochote kuhusu magonjwa ya kulogwa

Niulize chochote kuhusu magonjwa ya kulogwa

OMOYOGWANE

JF-Expert Member
Joined
Dec 30, 2016
Posts
4,701
Reaction score
11,920
Habari wakuu,

Kwa ambao hawanifahamu, nipo Bariadi huku Gamboshi napiga bachelor of science in uchawi wenye faida (digrii isiyo rasmi).

Katika uzi huu nitaeleza ninayojua kuhusu mada tajwa hapo juu.

Magonjwa yanayotokana na uchawi ni magonjwa ambayo hayapo kwenye Standard Guideline Treatment (STG) Mara nyingi haya exist ki medical (kitabibu) na daktari akifanya diagnosis inakuwa haipo clear atatoa dawa utaenda utatumia lakini hali ipo vile vile unahama hospitali hata tano lakini hakuna nafuu unayopata na majibu unapewa hayaeleweki.

Au unaumwa unaenda hospitali unapimwa kila kitu unaambiwa hauna tatizo lolote ila unamaumivu tu unapewa dawa za kutuliza maumivu kisha unaambiwa urudi nyumbani ukijiangalia unaona kabisa unaumwa tena sana.

Mara nyingi magonjwa ya kulogwa huwa ni tumbo, kupooza, maumivu yasiyoeleweka, kuchizika n.k

Kiujumla magonjwa ya kulogwa ni magonjwa ambayo hayatambuliki kihospitali.

Nakaribisha maswali yote uliza hapa hapa nitajibu hapa hapa.

Ahsante
 
Ukiwa na Hali ama tatizo.yani huku uraiani unaumwa ama udhaifu inakuwa vigumu kwenda kokote.kisha ukilala usiku unaota.unajiona unasocialize fresh tu huna shida yoyote.

Maanake nini
Hapo kuna uwezekano wa mizimu mibaya kumuandama mtu ndo ysnakuwaga hivyo yaani unajikuta hata kuoa au kuolewa inakuwa ngumu unakuwa upo upo tu halafu unakua mtu wa kuumwa hovyo hovyo

Ila kisayansi watakuambia ni stress au depression waambie wakutibu sasa unaona wanaanza kukupa majibu yasiyolizisha au kukukwepa
 
1.Magonjwa ya kurogwa wapoje?

2.Unatambua vipi kama mtu ana ugonjwa wa kurogwa?
Magonjwa ya kulogwa ni yale ambayo hayaeleweki yaani unajiona unaumwa kabisa ila hospitali wanapima kila kitu hawaoni tatizo

Wakati mwingine unaweza kuwa unaumwa tumbo unapata maumivu makali sana unaenda hospitali wanakuambia vidonda vya tumbo unapiga dawa zinadunda unaenda hospitali nyingine wanakwambia amoeba unapiga dawa zinadunda unarnda hospitali ingine hawaoni kitu wanakusukuma uende bugando unafika huko unaambiwa vidonda vya tumbo unapewa dawa zinadunda

Sijui unanielewa lakini mkuu? Sasa kiroho case kama hiyo mara nyingi mtu anakuwa alilishwa vitu vibaya kimazabe mazambe

Utambuzi wa mtu aliyerogwa ni kutumia kipimo cha asili ungo, kuku, mizimu n.k waliowahi kwenda kwa babu watanielewa
 
Bachela of Science in uchawi😁😁!!
Wachawi waseee sana
Uchawi huwezi kuuona ila utaona matokeo yake.

Neno uchawi ni kitu ambacho hakina maelezo ya kisayansi bado hakijafanyiwa utafiti na kuwekwa public kisha kupitishwa rasmi na taasisi mbali mbali ama serikali
Ila mtu anaonakabisa matokeo

Haya ni maoni yangu kwa ibservations zangu
 
Back
Top Bottom