Niulize chochote kuhusu mizimu

Niulize chochote kuhusu mizimu

Ni kweli ukitaka kujua Mungu wa kweli unauliza mizimu yako? Kumbuka Mungu ni roho na mizimu ni roho, roho zinaonana.
 
Ulishafika kuzimu??
Habari wakuu,

Nipo bariadi gamboshi masomoni nachukua digrii ya uchawi wenye faida.

Mizimu ni roho za watu waliokufa.

Kila mtu ana mizimu. Mizimu ya upande wa kwa baba na ya upande wa kwa mama (mababu na mabibi wote waliokufa)

Mizimu ipo mizuri na mizimu mibaya

Kuna aina zaidi ya >200 za mizimu.

Kama una swali lolote kuhusu mizimu kisayansi au kiroho niulize nitakujibu

Ahsante
A
 
Neno Mizimu ya Ukoo.

Inatokana na ukweli kwamba majini huishi miaka mingi sana tofauti na binadamu. Jini anauwezo wa kuishi zaidi ya miaka 500..hivyo anakuwa ameshuhudia vizazi zaidi ya 7-10 vya binadamu. Kwahiyo kama alikuwa akiabudiwa na babu zako waliokutangulia anaendeleza desturi hiyo kwa uzawa huo kwa vizazi kadhaa .

Mwisho ni kuwa mizimu haina uwezo wa kumnufaisha wala kundhuru mwanadamu isipokuwa kwa idhini ya Mungu.

Mungu akitaka kukupa mtihani wewe mwanadamu anaweza kuruhusu udhurike kwa shari za hao majini na akitaka huwezi kudhurika kamwe.
Sasa kama majini wapo kitambo sana hapa duniani kulinganisha na binadam .......mbona wapo nyuma sana kiteknolojia au kazi yao ni kushangaa tu
 
Mada yako bwana kifupi sana sana usilo lijua nikwamba...
Wewe ni movie halisi.
Na mastermind wa muvi yenyewe ndio hao wasio onekana.kwamatabaka yao wapo wengi sana,kuna mungu,miungu,aliens,mizimu n..k..
Nakila mtu yupo katika koo moja wapo yahizo..tatizo kubwa walio wengi hatujui,hawajui koo zao vizuri...hivo kujikuta hawana msaada wowote ule dhidi ya mashambulizi kutoka katika koo zingine.
Nilazima utambue ukoo wako vizuri ili uungane nao.
Kwakweli😂😂nimecheka sana, ukute Koo yangu ni mizimuni huko halafu naenda kushinda Kwa walokole usiku na mchana na mapambio, vita haziishi...kumbe natakiwa nirudi nyumbani kesi iishe.
 
Ni kwa nini Waafrika wanatukuza mizimu ya kizungu kuliko ya kwao? Kuna ubora katika mizimu?
 
Majini wazuri wanamuabudu na kumtii Mungu wala hawashawishi wanaadamu wamkufuru Mungu.
Hakuna majini WAZURI bali wooote ni waovu.

YESU KRISTO aliwahi kuambiwa kuwa anatumia MKUU WA WAJINI kuyatoa MAJINI.

YESU KRISTO alijibu hivi… Mathayo 12: 25-27

25 Basi Yesu akijua mawazo yao, akawaambia, Kila ufalme ukifitinika juu ya nafsi yake, hufanyika ukiwa; tena mji au nyumba yo yote ikifitinika juu ya nafsi yake, haitasimama.

26 Na Shetani akimtoa Shetani, amefitinika juu ya nafsi yake; basi ufalme wake utasimamaje?

27 Na mimi nikitoa pepo kwa Beelzebuli, je! Wana wenu huwatoa kwa nani? Kwa sababu hiyo hao ndio watakaowahukumu.
____________________________
Kwa mujibu wa YESU KRISTO… MASHETANI au MAJINI yooote lao ni moja maana kama kundi moja lipo hivi na lingine lipo vile basi UFALME WAO hauwezi kusimama!
 
Back
Top Bottom