Niulize chochote kuhusu mizimu

Niulize chochote kuhusu mizimu

Unejuaje kama jirani yako ni mchawi?

Unaweza kueleza viashiria ulivyoviona kwa mfano au kuvihisi?
Nyumba moja vyumba tofauti, likitokea jambo baya mfano nyoka alipita usiku na kaacha alama lazima akuambie, siku kama nne nyumba anatua ndege wa ajabu juu ya paa hasemi chochote(anakwarua hasa). Pia ndugu zake wanadai alimuua mme wake kishirikina.
 
Bado hujajua nini maana ya mizimu!

Mizimu ni mashetani wa kijini ambao wapo hai kabisa. Hakuna mizimu mizuri kwasababu inachochea ushirikina na inapenda kuabudiwa na kuombwa kama Mungu.

Mizimu ni majini waovu ama kwa jina lingine ni mashetani ya kijini.

Majini wazuri wanamuabudu na kumtii Mungu wala hawashawishi wanaadamu wamkufuru Mungu.
Hivi kuna majini wazuri?ndio wapi hao?
 
Kwanini watu mazwazwa wanaamini jambo la kufikirika kama mizimu?
 
Kwann mizimu ilizidiwa nguvu na dini za kigeni na ikashindwa kuwalinda waafrika wasitekwe na dini hizo kama kweli ina nguvu
 
Neno Mizimu ya Ukoo.

Inatokana na ukweli kwamba majini huishi miaka mingi sana tofauti na binadamu. Jini anauwezo wa kuishi zaidi ya miaka 500..hivyo anakuwa ameshuhudia vizazi zaidi ya 7-10 vya binadamu. Kwahiyo kama alikuwa akiabudiwa na babu zako waliokutangulia anaendeleza desturi hiyo kwa uzawa huo kwa vizazi kadhaa .

Mwisho ni kuwa mizimu haina uwezo wa kumnufaisha wala kundhuru mwanadamu isipokuwa kwa idhini ya Mungu.

Mungu akitaka kukupa mtihani wewe mwanadamu anaweza kuruhusu udhurike kwa shari za hao majini na akitaka huwezi kudhurika kamwe.
Mizimu ina nguvu kubwa kuliko majini ina uwezo wa kuishi hadi miaka elf sita.
Mizimu ni viongozi kama DC,RPC,RC.
Kazi yao kuu ni kusimamia ukoo, kabila,taifa,nchi,bara,nk ktk serikali ya shetani mizimu haitaki watu wawe na maendeleo wakiwa na maendeleo wataacha kuiabudu.
 
Mizimu ni roho za ndugu zako (babu na bibi), upande wa mama yako na baba yako.

Namaanisha baba yako ana baba yake baba yake na baba yako (babu) na yeye anababa yake chain inaendelea...........

Hivyo hivyo kwa mama yako, na yeye ana mama yake, mama yake na mama yako naye ana mama yake .... Circle inaendelea.........

Katika hao ndugu zako hapo juu kwa pande zote mbili (kwa baba na kwa mama) wapo waliokuwa matajiri wanamiliki mifugo nyumba na mashamba pia wapo masikini, wagonjwa, walevi, wasimbe n.k

Ikitokea umerithi mizimu ya kimasikini hautayaona mafanikio ikitokea umerithi mizimu ya kisimbe hautakaa udumu na mwanamke au mwanaume utqkufa single.

Matambiko ni njia ya kufukuza mizimu mibaya na kuiita mizimu mizuri

Wqchaga hufanya matambiko kila mwaka waulize watakupa somo

Ahsante
Makabila mengi ufanya matambiko mbona hayana maendeleo.
Wachaga wameiga desturi za wazungu za kurudi nyumbani kila mwaka kukutana kama familia na kufanya tathmini ya nini wamefanikiwa au la.
Wachaga wanatumia kanuni za kiuchumi za wayahudi hizi utumiwa na watu wote weupe duniani kuanzia waarabu, wachina, wahindi na ndio wakinga uzitumia hata wewe ukizitumia unafaulu.ushirikina hauwezi kupa utajiri endelevu
 
Mizimu ni roho za ndugu zako (babu na bibi), upande wa mama yako na baba yako.

Namaanisha baba yako ana baba yake baba yake na baba yako (babu) na yeye anababa yake chain inaendelea...........

Hivyo hivyo kwa mama yako, na yeye ana mama yake, mama yake na mama yako naye ana mama yake .... Circle inaendelea.........

Katika hao ndugu zako hapo juu kwa pande zote mbili (kwa baba na kwa mama) wapo waliokuwa matajiri wanamiliki mifugo nyumba na mashamba pia wapo masikini, wagonjwa, walevi, wasimbe n.k

Ikitokea umerithi mizimu ya kimasikini hautayaona mafanikio ikitokea umerithi mizimu ya kisimbe hautakaa udumu na mwanamke au mwanaume utqkufa single.

Matambiko ni njia ya kufukuza mizimu mibaya na kuiita mizimu mizuri

Wqchaga hufanya matambiko kila mwaka waulize watakupa somo

Ahsante
Mmh! Sasa Mtu umerithi mizimu ya kimasikini halafu eti unaifukuza Kwa kutambikia na kuita mizimu mizuri! Hiyo mizimu mizuri ya kitajiri itoke wapi wakati chain ya mizimu Yako ni ya kimasikini!?
 
Habari wakuu,

Nipo bariadi gamboshi masomoni nachukua digrii ya uchawi wenye faida.

Mizimu ni roho za watu waliokufa.

Kila mtu ana mizimu. Mizimu ya upande wa kwa baba na ya upande wa kwa mama (mababu na mabibi wote waliokufa)

Mizimu ipo mizuri na mizimu mibaya

Kuna aina zaidi ya >200 za mizimu.

Kama una swali lolote kuhusu mizimu kisayansi au kiroho niulize nitakujibu

Ahsante
Nipe Habari kuhusu Mizimu ya kichawi maana mimi ninaye Mzimu wa kichawi ananisumbuwa sana nimfanyaje ili akae pembeni asinisumbuwe.
 
Hata huku story za watu kufufuka zipo

YANI MISUKULE KWAKO NI WATU WALIO FUFUKA AU UNAMAANISHA NINI

KAMA UNAZUNGUMZIA MISUKULE INAYOPOTEZWA KIMAZINGIRA MNADHANI MNAZIKA MTU KUMBE NI MGOMBA WA NDIZI BASI NGOJA NIKUACHE KIDOGO MKUU
 
Makabila mengi ufanya matambiko mbona hayana maendeleo.
Inategemea hilo tambiko linafanyika kwa lengo gani.
Kuna tambiko la kuondoa maradhi (magonjwa), mikosi, nuksi kwa mtu au ukoo, tambiko la kumuaga mtu huko aendako, tambiko la kuomba mali, tambiko la kinga n.k inategemea wanafanya kwa lengo gani
Wachaga wameiga desturi za wazungu za kurudi nyumbani kila mwaka kukutana kama familia na kufanya tathmini ya nini wamefanikiwa au la.
Wachaga wanatumia kanuni za kiuchumi za wayahudi hizi utumiwa na watu wote weupe duniani kuanzia waarabu, wachina, wahindi na ndio wakinga uzitumia hata wewe ukizitumia unafaulu.
Hiyo aya ni jibu la swali lako hapo juu
ushirikina hauwezi kupa utajiri endelevu
Tambiko sio ushirikina
soil1.jpg
 
Mmh! Sasa Mtu umerithi mizimu ya kimasikini halafu eti unaifukuza Kwa kutambikia na kuita mizimu mizuri! Hiyo mizimu mizuri ya kitajiri itoke wapi wakati chain ya mizimu Yako ni ya kimasikini!?
Chain ya babu zako na bibi zako wapo waliokuwa na mafanikio na pia wapo waliokuwa masikini wa kutupwa

Namaanisha kizazi cha babu na bibi zako upande wa baba na mama yaani baba yake na babubyako, baba wa babu yake na babubyako .....chain iendelee

Kama walikuwa matajiri mfano miaka ya 1902 utajiri wao itakuwa mifugo, mashamba mazao, majembe, nyumba ya nyasi au fito kaniki n.k pia vitu luxury vitakuwa pombe ya kienyeji, vitu vya baharini, shanga, vyombo vya asili kama vile vibuyu vyungu, bangili mitungi n.k vyakula luxury kama vile ugali wa mtama n.k

Likifanyika tambiko tegemea kuona baadhi ya hivyo vitu

Wataziomba roho za babu zako wa enzi hizo waliokuwa ma don wakupe baraka mambo yako yafunguke

Wanasiasa wanayajua vizuri matambiko usiwaone hawana akili yanawasaidia, yangekuwa hayawasaidii wasingekuwa wanayafanya na kuyakumbatia

Hata wachaga utaona wanarudi kwao kila disemba ukiwauliza kiundani mmefanya nn huko hawawezi kukuambia kamwe
 
Nipe Habari kuhusu Mizimu ya kichawi maana mimi ninaye Mzimu wa kichawi ananisumbuwa sana nimfanyaje ili akae pembeni asinisumbuwe.
Mizimu ya kichawi isikie tu kwa watu ni hatari sana yaana ni full package inavuruga kila kitu kuanzia nyota, kazi, ndoa mwili mpaka biashara na maradhi juu

Kujinasua nenda kanisani au watafute wazee wako wa ukoo
 
Back
Top Bottom