Niulize chochote kuhusu mizimu

Niulize chochote kuhusu mizimu

Mizimu ni roho za ndugu zako (babu na bibi), upande wa mama yako na baba yako.

Namaanisha baba yako ana baba yake baba yake na baba yako (babu) na yeye anababa yake chain inaendelea...........

Hivyo hivyo kwa mama yako, na yeye ana mama yake, mama yake na mama yako naye ana mama yake .... Circle inaendelea.........

Katika hao ndugu zako hapo juu kwa pande zote mbili (kwa baba na kwa mama) wapo waliokuwa matajiri wanamiliki mifugo nyumba na mashamba pia wapo masikini, wagonjwa, walevi, wasimbe n.k

Ikitokea umerithi mizimu ya kimasikini hautayaona mafanikio ikitokea umerithi mizimu ya kisimbe hautakaa udumu na mwanamke au mwanaume utqkufa single.


Matambiko ni njia ya kufukuza mizimu mibaya na kuiita mizimu mizuri

Wqchaga hufanya matambiko kila mwaka waulize watakupa somo

Ahsante
Ni Wachaga wapi wanaofanya hayo matambiko kila mwaka? Hebu weka ushahidi tuwafahamu tukawaulize
 
Ila kuwa muafrika ni adhabu kwenye uhai na umauti.

Duniani ukute maisha ya mtu yote yalikuwa magumu, unapigika kisawasawa. Kama vile haitoshi, ukifa napo unaenda kuwa mzimu.
Tatizo hatujajua kama ukoshakuwa mzimu utakuwa na maisha ya aina gani, labda mizimu inakula bata huko iliko😀😀
 
Nawezaje kuutumia mzimu wa babu yangu kunitatulia changamoto zangu za kiafya na kimaisha wakati alipokuwa hai nilishindwa kumtumia na pia nilimtelekeza kabisa

Sasa hv hayupo duniani ndio nimeanza kutambua umuhimu wake?
Kuhusu mizimu ya babu yako kukupa mafanikio watafute wachaga watakupa shule

Ila kuhusu mizimu kukuletea shida kiafya hiyo inasumbua watu wengi, wapo wanafungwa uzazi, wapi wanaugua maradhi hayaeleweki wala hayatibiki hospitali ila wakiifuata kanuni za mizimu wanapona kabisa

Ndio wale ambao huvaa mabangili mkononi yale ya asili nadhani umewahi kukutana nao kaa nao vizuri hao watakupa shule na ushuhuda

Ahsante
 
Mkuu kwa sababu una uelewa wa hayo mambo ngoja niulize sijui itakua na uhusiano na mizimu direct au haina. Wanavosema kuna mwanamke ukilala nae mambo yako yataenda vizuri na mwingine ukimlala tu mambo yanakua tasa, hii ni kweli?
Kama ni kwel ntajuaje huyu ana baraka huyu ana mikosi?🙏
 
Sema sema stori ya majini kidogo Ili tupate maswali, mana hapa sioni ndauliza Nini katika kitu ambacho sijui
Nitaleta uzi wake siku nyingine.

Mizimu kisayansi ni genes au DNA ,
Hizi unaweza kurithi upande wa mama yako au wa baba yako. Kuna genes za magonjwa, maradhi, ujasiri, utajiri na ubinafsi.

Uliza upande wa kisayansi nikupe shule.

Ahsante
 
Bado hujajua nini maana ya mizimu!

Mizimu ni mashetani wa kijini ambao wapo hai kabisa. Hakuna mizimu mizuri kwasababu inachochea ushirikina na inapenda kuabudiwa na kuombwa kama Mungu.

Mizimu ni majini waovu ama kwa jina lingine ni mashetani ya kijini.

Majini wazuri wanamuabudu na kumtii Mungu wala hawashawishi wanaadamu wamkufuru Mungu.
Ukisema mashetani ya kijini je kuna mashetani yasiyo ya kijini?
 
kwanini mizimu huwa inapoda usoni...??
Hiyo ni mizimu ya kiganga.

Katika watu elfu moja unaweza kupata mtu mmoja tu. Ktk ukoo unaweza kupata mmoja au asipatikane kabisa mwenye hiyo mizimu ya kiganga inabidi kusubili wajukuu mpaka apatikane mwenye hiyo mizimu.

Mizimu hiyo hupanda usoni (kichwani) ili kumpa mtu uchizi kwa muda (kuteka akili yake) ndio kisha ataanza kuona mambo ya sasa na yajayo ataanza kukuambia,
Ufahamu ukirudi hawezi kukumbuka chochote.

Ili mganga apandishe mizimu lazima achizike kwa sekunde au dakika kadhaa ndio ataona shida yako kitaalamu mnaita ramli.

Nadhani nimejibu swali lako mkuu

Ahsqnte
 
Tatizo hatujajua kama ukoshakuwa mzimu utakuwa na maisha ya aina gani, labda mizimu inakula bata huko iliko😀😀
Mizimu itakula bata kupitia wewe.

Kama unamizimu ya kilevi basi maisha yako yote utakuwa cha pombe, ukiamka asubuhi unaamkia kwenye pombe za kienyeji muda wote unanuka pombe.

Haujawahi kuwaona watu wa dizaini hiyo mkuu?
 
Mkuu kwa sababu una uelewa wa hayo mambo ngoja niulize sijui itakua na uhusiano na mizimu direct au haina. Wanavosema kuna mwanamke ukilala nae mambo yako yataenda vizuri na mwingine ukimlala tu mambo yanakua tasa, hii ni kweli?
Kama ni kwel ntajuaje huyu ana baraka huyu ana mikosi?🙏
Hiyo ni kweli kabisa mkuu, kama huyo mwanamke ana mikosi, nuksi au mizimu ya kimasikini lazima ufilisike au mambo yako yaende mrama.

Ila kuna baadhi ya watu wana mizimu mikali sana mizimu ya ulinzi , akipata mwanamke mwenye mikosi basi litatokea tukio itashindikana kulala na huyo mwanamke. Ila akipuuza yatamkuta ya kumkuta.

Hata baadhi ya watoto wachanga wanamizimu mikali sana, baba akichepuka akarudi nyumbani yaani katoto kataumwa sanaa mtaenda hospitali katalazwa daktari atakuambia ni pneumonia leo kesho atakuambia ni neonatal infection kesho kutwa atakwambia ni kifafa ukimbana anakua hatoi majibu ya kueleweka mpaka unapagawa.

Ila ukiacha tu kuchepuka katoto kanapona. Ukiendelea kanaanza tena yaani ni kila mwezi unakuwa hospitali mpaka manesi wanakujua. Lazima akili ikukae sawa.

Kuna watu wazima wakishaona hivyo wanakufuata wanakupa shule unaona mtoto anapona anaacha kusumbua.

Sijui nimekupa jibu ulilouliza mkuu au bado?
 
Nyuzi za namna hii ni hatarishi kwa maendeleo ya taifa.
Inategemea na uelewa wako ktk haya mambo.

Serikali inachombo maalum cha kuwasapoti na kuwatambua wataalamu wa mambo ya kiroho ya asili na huwa inawaita na kuwasikiliza changamoto wanazopitia

Wewe unaona hayana tija kwako?

Na viongozi wote wa Tiba asili wa kila wilaya wana ofisi kila hospitali ya wilaya au mkoa.

Pia hata hapo muhimbili kipo kitengo cha Tiba asili na mkurugenzi wa sasa ni prof wa SUA
 
Back
Top Bottom