Niulize chochote kuhusu mizimu

Niulize chochote kuhusu mizimu

Hiyo ni kweli kabisa mkuu, kama huyo mwanamke ana mikosi, nuksi au mizimu ya kimasikini lazima ufilisike au mambo yako yaende mrama.

Ila kuna baadhi ya watu wana mizimu mikali sana mizimu ya ulinzi , akipata mwanamke mwenye mikosi basi litatokea tukio itashindikana kulala na huyo mwanamke. Ila akipuuza yatamkuta ya kumkuta.

Hata baadhi ya watoto wachanga wanamizimu mikali sana, baba akichepuka akarudi nyumbani yaani katoto kataumwa sanaa mtaenda hospitali katalazwa daktari atakuambia ni pneumonia leo kesho atakuambia ni neonatal infection kesho kutwa atakwambia ni kifafa ukimbana anakua hatoi majibu ya kueleweka mpaka unapagawa.

Ila ukiacha tu kuchepuka katoto kanapona. Ukiendelea kanaanza tena yaani ni kila mwezi unakuwa hospitali mpaka manesi wanakujua. Lazima akili ikukae sawa.

Kuna watu wazima wakishaona hivyo wanakufuata wanakupa shule unaona mtoto anapona anaacha kusumbua.

Sijui nimekupa jibu ulilouliza mkuu au bado?
Nimekuelewa vema
 
Bado hujajua nini maana ya mizimu!

Mizimu ni mashetani wa kijini ambao wapo hai kabisa. Hakuna mizimu mizuri kwasababu inachochea ushirikina na inapenda kuabudiwa na kuombwa kama Mungu.

Mizimu ni majini waovu ama kwa jina lingine ni mashetani ya kijini.

Majini wazuri wanamuabudu na kumtii Mungu wala hawashawishi wanaadamu wamkufuru Mungu.
Ustaaz Salamaleko.
 
Mizimu ni Mapepo au Majini yanayofutilia ukoo fulani.
Hakuna Mizimu mizuri kwa mfano utakuta ukoo una watu masikini sana na wana Mizimu inayo shindwa kuwakwamua kiuchumi.
Mizimu inapenda kuabudiwa na ina vilinge vya kuiabudu.

Kitu inachopenda kwenye familia ni uganga uchawi tu.
Utasikia mikoba ya babu irithishwe kwa mjukuu ilimrani iendelee kuabudiwa na ukoo husika.
Mizimu ikiona inapotezewa kuabudiwa inaanza kuleta mikosi kwenye ukoo husika kama magonjwa na taabu mbali mbali.
Inaleta taabu Hadi ukoo au familia au mtu husike afanye tambiko (ibada ya Mizimu) ndio apate nafuu.
Ibada halisi ya Mungu ndio njia pekee ya kuiondoa Mizimu katika Koo, Familia, au mtu husika.
 
Habari wakuu,

Nipo bariadi gamboshi masomoni nachukua digrii ya uchawi wenye faida.

Mizimu ni roho za watu waliokufa.

Kila mtu ana mizimu. Mizimu ya upande wa kwa baba na ya upande wa kwa mama (mababu na mabibi wote waliokufa)

Mizimu ipo mizuri na mizimu mibaya

Kuna aina zaidi ya >200 za mizimu.

Kama una swali lolote kuhusu mizimu kisayansi au kiroho niulize nitakujibu

Ahsante
MIZIMU HAINA AKILI NI MAJINI YANAYOCHUKUA SURA ZA WATU WALIO KUFA... HAKIKA KUMJUA YESU NDIO CHANZO CHA MAARIFA
 
Bado hujajua nini maana ya mizimu!

Mizimu ni mashetani wa kijini ambao wapo hai kabisa. Hakuna mizimu mizuri kwasababu inachochea ushirikina na inapenda kuabudiwa na kuombwa kama Mungu.

Mizimu ni majini waovu ama kwa jina lingine ni mashetani ya kijini.

Majini wazuri wanamuabudu na kumtii Mungu wala hawashawishi wanaadamu wamkufuru Mung
HAKUNAGA MAJINI WAZURI MAJINI WALISHAPOTEZA SIFA NIA YAO NI OVU DAIMA HAWANA JEMA WANALO WAZA
 
Mizimu ni roho za watu (ndugu) waliokwisha kuiacha miili yao, na roho zao zimeibaki kutangatanga huku hatma yake ikiwa ni kuzimu...

Iweje wewe mwanadamu mwenye uhai na utashi kamili utake kuongozwa na roho za wafu?
 
Back
Top Bottom