Niulize chochote kuhusu mizimu

Ni kweli ukitaka kujua Mungu wa kweli unauliza mizimu yako? Kumbuka Mungu ni roho na mizimu ni roho, roho zinaonana.
 
Ulishafika kuzimu??
A
 
Sasa kama majini wapo kitambo sana hapa duniani kulinganisha na binadam .......mbona wapo nyuma sana kiteknolojia au kazi yao ni kushangaa tu
 
Kwakweli😂😂nimecheka sana, ukute Koo yangu ni mizimuni huko halafu naenda kushinda Kwa walokole usiku na mchana na mapambio, vita haziishi...kumbe natakiwa nirudi nyumbani kesi iishe.
 
Ni kwa nini Waafrika wanatukuza mizimu ya kizungu kuliko ya kwao? Kuna ubora katika mizimu?
 
Majini wazuri wanamuabudu na kumtii Mungu wala hawashawishi wanaadamu wamkufuru Mungu.
Hakuna majini WAZURI bali wooote ni waovu.

YESU KRISTO aliwahi kuambiwa kuwa anatumia MKUU WA WAJINI kuyatoa MAJINI.

YESU KRISTO alijibu hivi… Mathayo 12: 25-27

25 Basi Yesu akijua mawazo yao, akawaambia, Kila ufalme ukifitinika juu ya nafsi yake, hufanyika ukiwa; tena mji au nyumba yo yote ikifitinika juu ya nafsi yake, haitasimama.

26 Na Shetani akimtoa Shetani, amefitinika juu ya nafsi yake; basi ufalme wake utasimamaje?

27 Na mimi nikitoa pepo kwa Beelzebuli, je! Wana wenu huwatoa kwa nani? Kwa sababu hiyo hao ndio watakaowahukumu.
____________________________
Kwa mujibu wa YESU KRISTO… MASHETANI au MAJINI yooote lao ni moja maana kama kundi moja lipo hivi na lingine lipo vile basi UFALME WAO hauwezi kusimama!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…