Niulize chochote kuhusu smartphones na mirrorless na DSLE Cameras

Niulize chochote kuhusu smartphones na mirrorless na DSLE Cameras

Nini maana ya Mirrorless na dslr ?
Mirrorless camera ni kamera ambayo mfumo wake wa upigaji picha kwenye upande wa sensor haina mfumo wa kuakisi Refelexmwanga kutoka kwenye picha inayochukuliwa ili ipelekwe kwenye sensor na picha kutengenezwa. Mfano mzuri ni kamera toka kampuni ya Fuji, Sony na baadhi toka kampuni za Nikon na Canon. Ni watengenezaji wakubwa wa hizi za Mirrorless camera.
Best-Mirrorless-Cameras.jpg
 
Nini maana ya dslr ?
DSLR NI Kifupi cha digital single-lens reflex. Mfumo wa uchukuaji picha ni kinyume cha Mirrorless ambapo ili picha inaswe na sensor ya kamera ina akisiwa toka kwenye kioo na ndipo hupelekwa kwenye sensor ili picha itengenezwe.
DSLR-Cross-Section.png

Kamera nyingi zenye huu mfumo ni za kampuni ya Canon, Nikon
 
Mkuu simu gani au toleo gani la Tecno ni best of all time mawili tafadhali hasa hasa kwenye ubora na uimara wa simu husika?

Sent from my TECNO KA7 using JamiiForums mobile app
 
Nikiona uzi wa namna hii ninakuwa na uhakika kabisa kuwa mtu alieanzisha ana ujuzi na mambo haya.

Ngoja nikae humu.
 
Kumekuwa kuna deals za smartphones kali kutoka used (Used from Dubai, Korea, Uk) simu kama samsung S7 edge utakuta inauzwa 240.......je ni deal nzuri kwa bei hiyo? na je zinakuwaga ni og au unahisi wanachakachua sana.?
 
Wino wa kwenye smartphone upo gramu ngapi mbona nimekaa na simu miaka miwili na haijawahi kuishiwa wino?

Je, tukikusanya wino wa simu milioni moja unaweza kujaza ndoo moja?
 
Kumekuwa kuna deals za smartphones kali kutoka used (Used from Dubai, Korea, Uk) simu kama samsung S7 edge utakuta inauzwa 240.......je ni deal nzuri kwa bei hiyo? na je zinakuwaga ni og au unahisi wanachakachua sana.?
Kwa sasa hizo simu used toka nje zimekamata sana soko. Mfano mzuri mimi natumia Sony XZ1. Kuna baadhi ya brand ni ngumu kuchakachua kama Sony, LG maana mchina hahusiki na kutoa copy sana.
Kwa brand kama Samsung ni rahisi kuchakachuliwa au kuuziwa simu ya mbongo mwenzako wa hapa hapa, labda upate Samsung ambayo ni customized kwa kampuni za simu za Korea na Japan kama docomo na kt.
Mfano mzuri:
kuna hii samsung galaxy feel nilinunua, zinakuwa na features tofauti sana na hizi ambazo zinatengenezwa china. kwa mfano china haweki features kama NFC.
1634715846426.jpeg
 
Wino wa kwenye smartphone upo gramu ngapi mbona nimekaa na simu miaka miwili na haijawahi kuishiwa wino?

Je, tukikusanya wino wa simu milioni moja unaweza kujaza ndoo moja?
Smartphone zinatumia Liquid Crystal Display screen ambapo pale kioo kinapopata majeraha huonekana kama ni wino, la hasha sio wino ni idadi ya pixel za kioo kilichopata jeraha.
 
Ushauri kqti ya samsung A12 na samsung A 21s hipi bora.nataka nichukue moja apo
Chief-Mkwawa
Mkuu nitakuelezea kutokana na baadhi ya vigezo kwa kupambanisha hziz simu mbili, wewe mwenyewe utaangalia kipi unachohitaji zaidi halafu utachagua aina ipi utainunu.

A12A21
Kutolewa 2020, June 26Kutolewa 2020, December 21
OS ANDROID 10OS ANDROID 10 unaweza ku-upgrade mpaka 11
Internal storage ni 32GB pekeeInternal storage ni 32GB 2GB RAM, 32GB 3GB RAM, 64GB 4GB RAM, 128GB 3GB RAM, 128GB 4GB RAM, 128GB 6GB RAM
Kamera ya mbele:13 MP, f/2.0, (wide), 1/3.1", 1.12µm

Kmaera ya nyuma: 16 MP, f/1.8, (wide), 1/3.06", 1.0µm, PDAF
8 MP, f/2.2, (ultrawide), 1/4.0", 1.12µm
2 MP, f/2.4, (macro)
2 MP, f/2.4, (depth)
kamera ya mbele: 8 MP, f/2.2

Kmaera ya Nyuma: 48 MP, f/2.0, 26mm (wide), AF
5 MP, f/2.2, 123˚ (ultrawide)
2 MP, f/2.4, (macro)
2 MP, f/2.4, (depth)
Battery:Li-Po 4000 mAhBattery:Li-Po 5000 mAh
Bei ya kiwandani:Tshs. 274295.00Bei ya kiwandani:Tshs. 366495.00
samsung-galaxy-a21-1.jpg
samsung-galaxy-a12-sm-a125-1.jpg

Hapo mkuu waweza chagua kwa tofauti hizo hapo juu unazoziona.
Vingine vinafanana, pia unaweza tembelea Compare Samsung Galaxy A21 vs. Samsung Galaxy A12 - GSMArena.com kwa maelezo zaidi
 
Internet tunayotumia inatoka wapi?
Internet ni mtandao wa kieletroniki unaounganishwa na mamilioni ya computer duniani ambayo hutumia protokali fulani ili kubadilishana taarifa mbalimbali. Mwanzo kabisa kianzilishi kilikuwa ARPANET ambao hawa walikua Wakala wa Miradi ya Utafiti wa Juu ndio waliofadhili zoezi la kubadilishana kwa taarifa.

Na Nani anayInternet ni
Hakuna mtu anayeimiliki, ila tunalipia gharama za kutumia kutokana na mitambo ambayo hutumika kusafirishia mtandao huo kama minara ambayo inamilikiwa na baadhi ya watu
 
Back
Top Bottom