Niulize chochote kuhusu smartphones na mirrorless na DSLE Cameras

Niulize chochote kuhusu smartphones na mirrorless na DSLE Cameras

swali langu kwa mleta mada, kipi hufanya computer itumie data kwa kiwango kikubwa kuliko smartphone
Computer hutumia data nyingi zaidi kwa sababu ya updates zinazokua zikiendela pale inapounganishwa na internet. Vitu kama Updates za window yenyewe, softwares kama office, antivirus na zinginezo.

Pia ukubwa wa kioo hasa pale unapo browse kwenye browser, taarifa zitakazo kuwa loaded ni kubwa zaidi kulinganisha na kioo cha simu.
 
na why smartphone iwe more than vibatan
Kwa issue ya smartphone vs vibatani.

Smartphones zinatumia network covarage kuanzia 2G mpaka 5G ambapo covarage kubwa ya network ni 3G na 4G kwa hapa nchini, wakati vibatani vingi vinatumia 2G (Edge) network na vichache vilivyotelew mwaka huu ni 3G.

Ukubwa wa matumizi upoje sasa? -

Smartphones zinauwezo mkubwa wa kuendesha apps in background ambazo zinatumia data bila ya wewe kufungua au kutumia wakati huo ambapo wewe unaitumia simu yako kwa mambo mengine ama hutumii kabisa endapo data imewashwa. Mfano unaweza washa data na punde ukaanza pata arafa(notifications) toka apps mbalimbali kwenye simu yako kama vile WhatsApp, Facebook, Stores n.k

Vibatani vilivyoundwa kwenye mfumo wake wa uendeshaji yani Operating System (OS) hairuhusu apps kutoa notification moja kwa moja mpaka uingie kwenye app husika. Pia mtandao wa 2G au Edge network ambao hauna kasi kubwa kama 3G,4G au 5G. Hivyo automatically ulaji wa MB 1 kwenye kibatani utakuwa mdogo sana kulinganisha na smartphone. KWA LUGHA NYEPESI SMARTPHONE NI SAWA NA TOYOTA V8 WAKATI KIBATANI NI TOYOTA PASSO.

Hata kwenye uharaka wa kufungua Data ni haraka zaidi kwenye Smartphone kuliko kibatani.
 
nifanyeje nipunguze matumizi ya data katka android phone while browsing not watching any video and namna ya kublock ads completely bila rooting.
Kama unatumia google chrome unaweza kuwasha Data Saver au Lite Mode ambazo hizi unazipata kwenye ili kupunguza matumizi ya data pale unapoitumia.

Ku-block ads kwenye google chrome nenda kwenye Setting>Advanced>>Site Setting>Ads bofya hapa utaona button bofya ku-block on site ads/misleading ads
 
DSLR NI Kifupi cha digital single-lens reflex. Mfumo wa uchukuaji picha ni kinyume cha Mirrorless ambapo ili picha inaswe na sensor ya kamera ina akisiwa toka kwenye kioo na ndipo hupelekwa kwenye sensor ili picha itengenezwe.
DSLR-Cross-Section.png

Kamera nyingi zenye huu mfumo ni za kampuni ya Canon, Nikon
Ipi nzuri kati ya hizo mbili?
 
Ipi nzuri kati ya hizo mbili?
Mirroless ni nzuri zaidi kuliko dslr kwa upande wa ubora wa picha ambapo hazina mechanical movement ambayo inaweza distort picha, ukubwa wa kamera kwa mirrorless ni mdogo zaidi kuliko dslr, na pia huchukua picha kwa haraka sana yani frame per second yake haina kizuizi kutokana na movement ya mirror haipo (mirrorless) ukilinganisha na kwenye dslr.
 
Mkuu unaweza ku Describe simu za Xiami.

Na Redmi ni hizo hizo ama...??

Naitaji kuzifaham ni General ukitofautisha na hizi simu zingine tunazo tumia.
Maana hizi simu zina Promo sana kuwa zina uwezo mkubwa tofauti na Gharama

Sent from my SM-A125F using JamiiForums mobile app
 
Naitaji kuzifaham ni General ukitofautisha na hizi simu zingine tunazo tumia.
Maana hizi simu zina Promo sana kuwa zina uwezo mkubwa tofauti na Gharama
Kuhusu promo hii kampuni wanafanya kujipenyeza ili kushika soko maana bado ni ngeni na haina miaka mingi sna kwenye soko.
kuhusu ubora kwa sasa hazitishi sana maana kampuni nyingi za simu zinatoa ubora wa hali ya juu kwenye soko la simu. Hivyo yote hayo ni kupambania mauzo ya kampuni ya Xiaomi lakini hakuna maajabu ukilinganisha na brands ya simu nyingine.
 
Natumia Samsung j6+ hivi karibuni nimepata shida upande app ya WhatsApp ikihitaji ni update lkn nikiwa playstore inaload hata nusu saa japokua network inasoma 4G ...

Nikirudisha tarehe nyuma mfano Sept 21 WhatsApp inakubali je nini tatizo ?

Pia nina tumia gbwhatsapp kwa namba nyingine je Kuna tatizo maana ni apk.
 
CHIEF MKWAWA na wadau wengine naomba ushauri wa hizj simu 3 zote bei zinakaribia

Ila nataka nichukue moja ipi Bora kigezo cha chaji naomba tusikiangalie

Nokia 1.4

Infinix smart 5

Na tecno spark 7

Picha za specifications zake hizo hapo down

Picha namba 1 ni Nokia 1.4

Namba 2 ni infinix smart 5

Na namba 3 ni spark 7

Naomba kiwasilisha
Screenshot_20211022-141332.jpg
Screenshot_20211022-141716.jpg
Screenshot_20211022-141756.jpg
 
Natumia Samsung j6+ hivi karibuni nimepata shida upande app ya WhatsApp ikihitaji ni update lkn nikiwa playstore inaload hata nusu saa japokua network inasoma 4G ...

Nikirudisha tarehe nyuma mfano Sept 21 WhatsApp inakubali je nini tatizo ?

Pia nina tumia gbwhatsapp kwa namba nyingine je Kuna tatizo maana ni apk.
Hiyo ishu ya whatsapp nishauri ufanye backup ya data zako pale inapokubali kufunguka, kisha unistall halafu download tena.

GBWhatsapp hamna tatizo. Endelea kutumia
 
Camera gani ya bei rahisi kmpuni ya nikoni kwa matumizi ya kupig picha
 
Mkuu nitakuelezea kutokana na baadhi ya vigezo kwa kupambanisha hziz simu mbili, wewe mwenyewe utaangalia kipi unachohitaji zaidi halafu utachagua aina ipi utainunu.

A12A21
Kutolewa 2020, June 26Kutolewa 2020, December 21
OS ANDROID 10OS ANDROID 10 unaweza ku-upgrade mpaka 11
Internal storage ni 32GB pekeeInternal storage ni 32GB 2GB RAM, 32GB 3GB RAM, 64GB 4GB RAM, 128GB 3GB RAM, 128GB 4GB RAM, 128GB 6GB RAM
Kamera ya mbele:13 MP, f/2.0, (wide), 1/3.1", 1.12µm

Kmaera ya nyuma: 16 MP, f/1.8, (wide), 1/3.06", 1.0µm, PDAF
8 MP, f/2.2, (ultrawide), 1/4.0", 1.12µm
2 MP, f/2.4, (macro)
2 MP, f/2.4, (depth)
kamera ya mbele: 8 MP, f/2.2

Kmaera ya Nyuma: 48 MP, f/2.0, 26mm (wide), AF
5 MP, f/2.2, 123˚ (ultrawide)
2 MP, f/2.4, (macro)
2 MP, f/2.4, (depth)
Battery:Li-Po 4000 mAhBattery:Li-Po 5000 mAh
Bei ya kiwandani:Tshs. 274295.00Bei ya kiwandani:Tshs. 366495.00
samsung-galaxy-a21-1.jpg
samsung-galaxy-a12-sm-a125-1.jpg

Hapo mkuu waweza chagua kwa tofauti hizo hapo juu unazoziona.
Vingine vinafanana, pia unaweza tembelea Compare Samsung Galaxy A21 vs. Samsung Galaxy A12 - GSMArena.com kwa maelezo zaidi
Mwonekano wa camera ya katikati siupendi bora iwe pembeni
 
Camera gani ya bei rahisi kmpuni ya nikoni kwa matumizi ya kupig picha
Inategemeana na soko unapochukulia. Ila matoleo haya utayapata kwa bei rahisi: Nikon D90, d3100, d3200, d3400, d3500
 
Back
Top Bottom