Niulize chochote kuhusu Subwoofer na Sounds system

Niulize chochote kuhusu Subwoofer na Sounds system

kelphin

JF-Expert Member
Joined
Dec 24, 2019
Posts
9,872
Reaction score
16,319
Ikiwa inakusumbua,ikiwa unataka kufahamu chochote kinachokutatiza.

Karibu
images.jpg


Nieleze kidogo kuhusu subwoofer
Je, unataka kununua, basi zingatia haya.

Zipo za aina mbili old model na digital. Siyo majina hapana ,yaani inaweza kua rising,seapiano,codjec,aborder au vyovyote Ila itakua digital au old model.

Hizo digital ni Aina ya subwoofer ambayo inamuundo wakisasa ,mala nyingi utakuta Ina (nob) kivingilisho Cha sauti kimoja tu.

Ila kinafanya multipurpose, ukibonyeza hyo hiyo nob unaweza ongeza sauti ,kuongeza bass, na mid.
kifupi mambo yote ni in one button.

Faida yake ni kuwa, aina ya power supply yake Ni ilitaka ifanane na ya home theater(Ila haijawahi[emoji2][emoji2inakua na umeme mnyoofu kidogo.

Zinakua na music mkubwa na mdundo zaidi ni digital,yaani yakisasa,
lakini pia display yake ni LCD haitumii umeme mwingi.

Je utaijuaje?
Nob ya kuongezea sauti ni moja tu na zaidi utakuta button za menu na input inategemeana). Ukiigeuza nyuma ina kiplastic kidogo kilichozungushwa nati, yaani ikiwa italeta shida fundi huku nyuma hafungui mfuniko wote wa nyuma, hufungua ki plastic tu hapo nyuma ndio kimebeba card zoote na subwoofer.

Hasara zake
  1. Ikitokea imeharibu card yake hauwez kubadilisha ,sababu ndani Ina circuit Kama ya phone mafundi weeengi hawana(hatuna) technology yakuitengeneza kwahyo unaenda dukani unanunua Tena kard na si chini ya 40000.
  2. Ila ukifika unaipachika tu huangaiki.
  3. Inahitaji utulie ili uioperate maana inatumia single nob.
  4. Speaker yake ya bass huwekwa ohms ndogo ili idunde sana kwahiyo usipende kuweka sauti kubwa Sana kwa muda mrefu.

Aina ya pili ndio zile old model
Hizo zinaitwa dunda udundavyo ni nzuri kwenye uzuri wake. Yenyewe ukiingalia utakuta Ina nob yaani vile vyakuongezea sauti zaidi ya kimoja. Yaani cha master volume, bass, tweeter na mic, na ukivizungusha vinafika mwisho.

Yenyewe ndani power supply yake ni ya kawaida, inatumia mtransformer wake na diodes za kawaida. kisha umeme huingia kwenye capacitor ndio unaanza kusambazwa ndani. Yaweza kuwa Seapiano, Codjec Aborder au vyovyote. Ukiigeuza nyuma mfuniko wote unafunguka wa nyuma.

Faida yake
  1. ikizingua unaiweza kuirekebisha kiurahisi tu
  2. Zinavumilia sana
  3. Hata muziki upo pia
  4. Rahisi kuitumia
Hasara zake
  1. Display yake ni VFD kama ni seapiano hapa mbele inakioo,inavyoimba Kuna vitu vinacheza cheza kwenye kioo(hii ni kwa baadhi ya subwoofer)
  2. Muonekano wake ni wakizamani ikilinganishwa na hizi mpya

Soma hi pia [emoji1427]
Ndani ya subwoofer panya hupenda kuishi humo, huzaliana na kuleta hitilafu kwa kukata nyaya na kula speaker.
Waya wa speaker una chumvi chumvi hivyo akiingia hauachi.

Simple way jinsi ya kudhibiti
Pale kwenye tobo kuna ki corn cha duara huwa wanakipachika unaweza kukitoa kwa kufuata mpangilio ufuatao:

  1. Chukua maji ya moto kidogo na kitambaa, kichovye kitambaa kwenye maji kisha kikande kuzunguka mduara kwa dakika tano.
  2. Kisha chukua kisu, tumia ncha yake kuingiza pembezoni mwa mduara bila kuikwajua. Huku ukiinua kidogo kidogo kuzunguka corn nzima,ukisha kitoa kitoboe vitundu vidogo kukizunguka upande wa ndani(sio Huku uliko Kanda kwa maji).
  3. Ukisha kitoa chukua waya mgumu usuke upande wa ndani kuzunguka uwazi wa duara wote mule ulimotoboa, kisuke hakikisha unaacha vyumba vidogovidogo kiasi kwamba kinaweza kupita kidore kidogo tu.
  4. Paka gundi upande wa ndani, huku ulikokua unakanda na maji kisha kibandike tena kama kilivyokuwa.

NB: Hii ni kwazile subwoofer kama pichani hapo juu, ambazo hutolea upepo pembeni kwenye kiduara. Wale zinazotolea mbele chini ni habari nyingine.

***
Kiasi chake mtanielewaView attachment 1560194View attachment 1560195

Some updates,
Je, music system yako haina bluetooth na unataka kuongezea? Easy sana na inawezekana pia, kwa mafundi ninaweza kuwaelekeza.

Lakini pia music system yako ulipenda itoe mp5, yaani picture, video inawezekana pia[emoji3][emoji3].
Hususani wale wenye TV za kizamani yaani unachomeka flash disk yako kwenye subwoofer, unapata mdundo alafu kuna cable itatoka kwenye subwoofer hadi kwenye TV yako.

Stay here.
More good things are here.
Welcome.

View attachment 1921368
View attachment 1921369
 
Nitaifix vipi mkuu
Inatakiwa ifunguliwe hadi kwenye amp circuit then kagua kama kuna kiungo kilichokauka na kupelekea mguu wa component kuwa haushikamani na risasi au umelega au umepwaya katikati ya risasi, kama kuna kitu kama hicho ujazilishie kwa risasi. Unapaswa kuwa na soldering iron na solder wire. Pia kagua nyaya zinazokwenda kuungana na spika kama zimeshikamana vizuri.
 
Ahsante mkuu,vipi unaweza kunipa mwanga kidogo ili hata nikipeleka kwa fundi niwe na idea kidogo maana nikienda kichwakichwa naweza kula za usoo

Sent from my 502SO using JamiiForums mobile app
1. Kabla ya kuituhumu subwoofer yako hakikisha Flash yako kama iko njema
2. Hakikisha muundo wa mafaili (file format)yaliyopo kwenye flash yako ndio yanayokubaliwa na subwoofer (yanatambuliwa na kuchezwa na subwoofer yako)
Kama vyote hivyo viko sawa basi
Hii ni kesi ya kwenye panel ya USB.
 
Mkuu miaka 5 nyuma nilinunua hiyo sub Ufa hapo chini, yaani ilikuwa safi mnooo ila vibaka wakaruka nayo daah nikasikitika sana maana kuitafuta sikuipata tena. Majuzi nikaona Instagram jamaa wanaojiita Electronic points wa Kariakoo wanayo. Hivi inaweza kuwa kama ile ya kwanza kweli??
Screenshot_20201211-144312.jpg
 
Inatakiwa ifunguliwe hadi kwenye amp circuit then kagua kama kuna kiungo kilichokauka na kupelekea mguu wa component kuwa haushikamani na risasi au umelega au umepwaya katikati ya risasi, kama kuna kitu kama hicho ujazilishie kwa risasi. Unapaswa kuwa na soldering iron na solder wire. Pia kagua nyaya zinazokwenda kuungana na spika kama zimeshikamana vizuri.

Good
 
Mkuu miaka 5 nyuma nilinunua hiyo sub Ufa hapo chini, yaani ilikuwa safi mnooo ila vibaka wakaruka nayo daah nikasikitika sana maana kuitafuta sikuipata tena. Majuzi nikaona Instagram jamaa wanaojiita Electronic points wa Kariakoo wanayo. Hivi inaweza kuwa kama ile ya kwanza kweli?? View attachment 1657081

Mkuu subwoofer nyingi sasahiv ni digital mode
Sio kama hizo za mwanzo
Zongtech wameacha kutengeneza oldmodel kwasababu kadhaa ikiwemo usasa na mauzo kiujumla
Unaweza ipata ila utaitafuta mno
Na ikiwa ipo basi ilikuwepo store
Ila zipo
 
Mkuu mimi yangu ni Geepas,inapiga mdundo tu lakini stereo hakuna mpala nichezeshe chezeshe nyaya kule nyuma nikiachia nayenyewe inaacha inapiga mdundo tu.

Nini tatizo hapo??
 
Mkuu mimi yangu ni Geepas,inapiga mdundo tu lakini stereo hakuna mpala nichezeshe chezeshe nyaya kule nyuma nikiachia nayenyewe inaacha inapiga mdundo tu.

Nini tatizo hapo??

Pole mkuu
Nyuma kule kuna connector za speaker output
Ikiwa terminal zimeachia basi hilo lazima zilikutokee
Kwahyo itafaa fundi achomelee kidogo hapo kuweka mkazo wa connector na circuit
 
Pole mkuu
Nyuma kule kuna connector za speaker output
Ikiwa terminal zimeachia basi hilo lazima zilikutokee
Kwahyo itafaa fundi achomelee kidogo hapo kuweka mkazo wa connector na circuit
Barikiwa mkuu,hata hivyo ni ya muda sana hii Geepas tangu 2008 mkuu nilinunua maonyesho ya 77 kwa gharama ya 70,000 tu.

Imekosa features za bluetooth hivi naweza kuzipachika humu kwenye hii old model system??
 
Barikiwa mkuu,hata hivyo ni ya muda sana hii Geepas tangu 2008 mkuu nilinunua maonyesho ya 77 kwa gharama ya 70,000 tu.

Imekosa features za bluetooth hivi naweza kuzipachika humu kwenye hii old model system??

Ndio kaka unaweka Bluetooth vizuri kabisa na remote kabisa
Na ikiwa hutumii flat tv unaweza kuweka mp5 hapo kwenye subwoofer
Kwahyo ukichomeka flash yako kwenye subwoofer unapata mdundo na picha kwenye tv yako[emoji41]
 
Ndio kaka unaweka Bluetooth vizuri kabisa na remote kabisa
Na ikiwa hutumii flat tv unaweza kuweka mp5 hapo kwenye subwoofer
Kwahyo ukichomeka flash yako kwenye subwoofer unapata mdundo na picha kwenye tv yako[emoji41]
Itabidi nifanye hivyo tu maana hii subwoofer nimepanga kutoiacha kamwe kwa kadri nilivyokaa nayo muda mrefu.
 
Back
Top Bottom