Niulize chochote kuhusu Subwoofer na Sounds system

Niulize chochote kuhusu Subwoofer na Sounds system

kelphin

JF-Expert Member
Joined
Dec 24, 2019
Posts
9,872
Reaction score
16,319
Ikiwa inakusumbua,ikiwa unataka kufahamu chochote kinachokutatiza.

Karibu
images.jpg


Nieleze kidogo kuhusu subwoofer
Je, unataka kununua, basi zingatia haya.

Zipo za aina mbili old model na digital. Siyo majina hapana ,yaani inaweza kua rising,seapiano,codjec,aborder au vyovyote Ila itakua digital au old model.

Hizo digital ni Aina ya subwoofer ambayo inamuundo wakisasa ,mala nyingi utakuta Ina (nob) kivingilisho Cha sauti kimoja tu.

Ila kinafanya multipurpose, ukibonyeza hyo hiyo nob unaweza ongeza sauti ,kuongeza bass, na mid.
kifupi mambo yote ni in one button.

Faida yake ni kuwa, aina ya power supply yake Ni ilitaka ifanane na ya home theater(Ila haijawahi[emoji2][emoji2inakua na umeme mnyoofu kidogo.

Zinakua na music mkubwa na mdundo zaidi ni digital,yaani yakisasa,
lakini pia display yake ni LCD haitumii umeme mwingi.

Je utaijuaje?
Nob ya kuongezea sauti ni moja tu na zaidi utakuta button za menu na input inategemeana). Ukiigeuza nyuma ina kiplastic kidogo kilichozungushwa nati, yaani ikiwa italeta shida fundi huku nyuma hafungui mfuniko wote wa nyuma, hufungua ki plastic tu hapo nyuma ndio kimebeba card zoote na subwoofer.

Hasara zake
  1. Ikitokea imeharibu card yake hauwez kubadilisha ,sababu ndani Ina circuit Kama ya phone mafundi weeengi hawana(hatuna) technology yakuitengeneza kwahyo unaenda dukani unanunua Tena kard na si chini ya 40000.
  2. Ila ukifika unaipachika tu huangaiki.
  3. Inahitaji utulie ili uioperate maana inatumia single nob.
  4. Speaker yake ya bass huwekwa ohms ndogo ili idunde sana kwahiyo usipende kuweka sauti kubwa Sana kwa muda mrefu.

Aina ya pili ndio zile old model
Hizo zinaitwa dunda udundavyo ni nzuri kwenye uzuri wake. Yenyewe ukiingalia utakuta Ina nob yaani vile vyakuongezea sauti zaidi ya kimoja. Yaani cha master volume, bass, tweeter na mic, na ukivizungusha vinafika mwisho.

Yenyewe ndani power supply yake ni ya kawaida, inatumia mtransformer wake na diodes za kawaida. kisha umeme huingia kwenye capacitor ndio unaanza kusambazwa ndani. Yaweza kuwa Seapiano, Codjec Aborder au vyovyote. Ukiigeuza nyuma mfuniko wote unafunguka wa nyuma.

Faida yake
  1. ikizingua unaiweza kuirekebisha kiurahisi tu
  2. Zinavumilia sana
  3. Hata muziki upo pia
  4. Rahisi kuitumia
Hasara zake
  1. Display yake ni VFD kama ni seapiano hapa mbele inakioo,inavyoimba Kuna vitu vinacheza cheza kwenye kioo(hii ni kwa baadhi ya subwoofer)
  2. Muonekano wake ni wakizamani ikilinganishwa na hizi mpya

Soma hi pia [emoji1427]
Ndani ya subwoofer panya hupenda kuishi humo, huzaliana na kuleta hitilafu kwa kukata nyaya na kula speaker.
Waya wa speaker una chumvi chumvi hivyo akiingia hauachi.

Simple way jinsi ya kudhibiti
Pale kwenye tobo kuna ki corn cha duara huwa wanakipachika unaweza kukitoa kwa kufuata mpangilio ufuatao:

  1. Chukua maji ya moto kidogo na kitambaa, kichovye kitambaa kwenye maji kisha kikande kuzunguka mduara kwa dakika tano.
  2. Kisha chukua kisu, tumia ncha yake kuingiza pembezoni mwa mduara bila kuikwajua. Huku ukiinua kidogo kidogo kuzunguka corn nzima,ukisha kitoa kitoboe vitundu vidogo kukizunguka upande wa ndani(sio Huku uliko Kanda kwa maji).
  3. Ukisha kitoa chukua waya mgumu usuke upande wa ndani kuzunguka uwazi wa duara wote mule ulimotoboa, kisuke hakikisha unaacha vyumba vidogovidogo kiasi kwamba kinaweza kupita kidore kidogo tu.
  4. Paka gundi upande wa ndani, huku ulikokua unakanda na maji kisha kibandike tena kama kilivyokuwa.

NB: Hii ni kwazile subwoofer kama pichani hapo juu, ambazo hutolea upepo pembeni kwenye kiduara. Wale zinazotolea mbele chini ni habari nyingine.

***
Kiasi chake mtanielewaView attachment 1560194View attachment 1560195

Some updates,
Je, music system yako haina bluetooth na unataka kuongezea? Easy sana na inawezekana pia, kwa mafundi ninaweza kuwaelekeza.

Lakini pia music system yako ulipenda itoe mp5, yaani picture, video inawezekana pia[emoji3][emoji3].
Hususani wale wenye TV za kizamani yaani unachomeka flash disk yako kwenye subwoofer, unapata mdundo alafu kuna cable itatoka kwenye subwoofer hadi kwenye TV yako.

Stay here.
More good things are here.
Welcome.

View attachment 1921368
View attachment 1921369
 
Bass ya kawaida? Kwenye makaratasi (specs) labda.

Nenda YouTube silikiza reviews zinasema nini kuhusu BASS yake na pia nenda amazon soma reviews za walionunua uone wanaongelea nini kuhusu BASS yake halafu uje hapa tuendelee kuongea.

Kiuhalisia watumiaji na reviewers huwa wanasema the Bass is too much, na hizi speakers zina option ya kupunguza Bass kama mtu anaona bass is too much for him..

I own them, so ninaongelea kitu ninachokifahamu.
yawezekana hta mtu wa sayona nae akakuambia anachokisikia ni too much bass

anyway kila mtu aamini kimfaacho.
 
yawezekana hta mtu wa sayona nae akakuambia anachokisikia ni too much bass

anyway kila mtu aamini kimfaacho.
Mkuu , hapa tunazungumzia Klipsch, an American Speaker Brand, one of the biggest manufacturers wa audio gears duniani, sio michina ya Sea piano wala kodtec.

Nimekuambia Nenda online kaangalie reviews na comments kuhusu BASS ya hizi speakers (kutoka kwa watu waliozitumia huko duniani), umeenda au unanibishia tu?

NB: Mimi ninazo hizi speakers home kwangu hapa Bongo, so ninajua ninachokizungumza.
 
nihangaike kupata deep bass kwa mamilion ya fedha wakat zipo better and affordable options

kuna subwoofer za inchi 8 zimeandikwa black decker aloo zinatema bass vibaya

ukifika moshi mjini stend kubwa kuna kighorofa kuna pub kuna subwoofer hpo zimefungwa ile deep bass sijawah isikia popote ukipita lami unasikia kabisa muungurumo wa hatari hyo ndo mambo sasa.
Yaleyale ya "nihangaike kununua Land Cruizer ya mamilioni ya fedha wakati zipo Vitz ambazo ni affordable options"

Mzee baba, tutafute hela tuache hizi sababu-sababu.
 
Mkuu , hapa tunazungumzia Klipsch, an American Speaker Brand, one of the biggest manufacturers wa audio gears duniani, sio michina ya Sea piano wala kodtec.

Nimekuambia Nenda online kaangalie reviews na comments kuhusu BASS ya hizi speakers (kutoka kwa watu waliozitumia huko duniani), umeenda au unanibishia tu?

NB: Mimi ninazo hizi speakers home kwangu hapa Bongo, so ninajua ninachokizungumza.
kumbe mnabishana kuhusu keepers of sound "klipsch"
Hayo madude similiki ila ni habari nyingine. towers tu pekee unaonglea mil4+😂😂🙌🙌
 
kumbe mnabishana kuhusu keepers of sound "klipsch"
Hayo madude similiki ila ni habari nyingine. towers tu pekee unaonglea mil4+[emoji23][emoji23][emoji119][emoji119]
ni kweli jamaa wako vizuri sanaaa kwnye huo upande

ila sio kwamba hawa wengine hamna kabisa especially linapokuja suala la budgetary mechanism

sasa hvi watu wenye pub na bar Hawangahiki sana na P.A system

wanacustomize tu car audio systems na sound inakuwa yakibabe sanaaa tena ni affordable zaidi.
 
ni kweli jamaa wako vizuri sanaaa kwnye huo upande

ila sio kwamba hawa wengine hamna kabisa especially linapokuja suala la budgetary mechanism

sasa hvi watu wenye pub na bar Hawangahiki sana na P.A system

wanacustomize tu car audio systems na sound inakuwa yakibabe sanaaa tena ni affordable zaidi.
Wanacustomize sio kama hawapendi mziki mzuri, tatizo ni mawe.
 
ni kweli jamaa wako vizuri sanaaa kwnye huo upande

ila sio kwamba hawa wengine hamna kabisa especially linapokuja suala la budgetary mechanism

sasa hvi watu wenye pub na bar Hawangahiki sana na P.A system

wanacustomize tu car audio systems na sound inakuwa yakibabe sanaaa tena ni affordable zaidi.
kama ambavyo mimi nimeamua kuteñgeneza speaker zangu mwenyewe.
maana nawaza nikanunue kitu sawa na bei ya gari bongo. bei + usafiri. maana towers ni nzito.

na ukitafuta za mtumba hapa bongo nyingi zimechoka na bado bei ni mkasi wanaanzia laki 5.
 
Anachokifanya RReigns na huyu wa Nairobi tofauti ni nini? Yeye kakusanya katengeneza tower zake, ukazisigina hapa hapa kwamba hazina deep bass.
umesoma hzo specs kwanza


tembelea kwanza page yko huko insta.

halafu nilishasema inategemea na ww unavyotafsir deep bass, kwangu naamin hzo hazitonitosha kma kipengele ni deep bass.
 
Back
Top Bottom