Niulize chochote kuhusu Subwoofer na Sounds system

kelphin

JF-Expert Member
Joined
Dec 24, 2019
Posts
9,872
Reaction score
16,319
Ikiwa inakusumbua,ikiwa unataka kufahamu chochote kinachokutatiza.

Karibu

Nieleze kidogo kuhusu subwoofer
Je, unataka kununua, basi zingatia haya.

Zipo za aina mbili old model na digital. Siyo majina hapana ,yaani inaweza kua rising,seapiano,codjec,aborder au vyovyote Ila itakua digital au old model.

Hizo digital ni Aina ya subwoofer ambayo inamuundo wakisasa ,mala nyingi utakuta Ina (nob) kivingilisho Cha sauti kimoja tu.

Ila kinafanya multipurpose, ukibonyeza hyo hiyo nob unaweza ongeza sauti ,kuongeza bass, na mid.
kifupi mambo yote ni in one button.

Faida yake ni kuwa, aina ya power supply yake Ni ilitaka ifanane na ya home theater(Ila haijawahi[emoji2][emoji2inakua na umeme mnyoofu kidogo.

Zinakua na music mkubwa na mdundo zaidi ni digital,yaani yakisasa,
lakini pia display yake ni LCD haitumii umeme mwingi.

Je utaijuaje?
Nob ya kuongezea sauti ni moja tu na zaidi utakuta button za menu na input inategemeana). Ukiigeuza nyuma ina kiplastic kidogo kilichozungushwa nati, yaani ikiwa italeta shida fundi huku nyuma hafungui mfuniko wote wa nyuma, hufungua ki plastic tu hapo nyuma ndio kimebeba card zoote na subwoofer.

Hasara zake
  1. Ikitokea imeharibu card yake hauwez kubadilisha ,sababu ndani Ina circuit Kama ya phone mafundi weeengi hawana(hatuna) technology yakuitengeneza kwahyo unaenda dukani unanunua Tena kard na si chini ya 40000.
  2. Ila ukifika unaipachika tu huangaiki.
  3. Inahitaji utulie ili uioperate maana inatumia single nob.
  4. Speaker yake ya bass huwekwa ohms ndogo ili idunde sana kwahiyo usipende kuweka sauti kubwa Sana kwa muda mrefu.

Aina ya pili ndio zile old model
Hizo zinaitwa dunda udundavyo ni nzuri kwenye uzuri wake. Yenyewe ukiingalia utakuta Ina nob yaani vile vyakuongezea sauti zaidi ya kimoja. Yaani cha master volume, bass, tweeter na mic, na ukivizungusha vinafika mwisho.

Yenyewe ndani power supply yake ni ya kawaida, inatumia mtransformer wake na diodes za kawaida. kisha umeme huingia kwenye capacitor ndio unaanza kusambazwa ndani. Yaweza kuwa Seapiano, Codjec Aborder au vyovyote. Ukiigeuza nyuma mfuniko wote unafunguka wa nyuma.

Faida yake
  1. ikizingua unaiweza kuirekebisha kiurahisi tu
  2. Zinavumilia sana
  3. Hata muziki upo pia
  4. Rahisi kuitumia
Hasara zake
  1. Display yake ni VFD kama ni seapiano hapa mbele inakioo,inavyoimba Kuna vitu vinacheza cheza kwenye kioo(hii ni kwa baadhi ya subwoofer)
  2. Muonekano wake ni wakizamani ikilinganishwa na hizi mpya

Soma hi pia [emoji1427]
Ndani ya subwoofer panya hupenda kuishi humo, huzaliana na kuleta hitilafu kwa kukata nyaya na kula speaker.
Waya wa speaker una chumvi chumvi hivyo akiingia hauachi.

Simple way jinsi ya kudhibiti
Pale kwenye tobo kuna ki corn cha duara huwa wanakipachika unaweza kukitoa kwa kufuata mpangilio ufuatao:

  1. Chukua maji ya moto kidogo na kitambaa, kichovye kitambaa kwenye maji kisha kikande kuzunguka mduara kwa dakika tano.
  2. Kisha chukua kisu, tumia ncha yake kuingiza pembezoni mwa mduara bila kuikwajua. Huku ukiinua kidogo kidogo kuzunguka corn nzima,ukisha kitoa kitoboe vitundu vidogo kukizunguka upande wa ndani(sio Huku uliko Kanda kwa maji).
  3. Ukisha kitoa chukua waya mgumu usuke upande wa ndani kuzunguka uwazi wa duara wote mule ulimotoboa, kisuke hakikisha unaacha vyumba vidogovidogo kiasi kwamba kinaweza kupita kidore kidogo tu.
  4. Paka gundi upande wa ndani, huku ulikokua unakanda na maji kisha kibandike tena kama kilivyokuwa.

NB: Hii ni kwazile subwoofer kama pichani hapo juu, ambazo hutolea upepo pembeni kwenye kiduara. Wale zinazotolea mbele chini ni habari nyingine.

***
Kiasi chake mtanielewaView attachment 1560194View attachment 1560195

Some updates,
Je, music system yako haina bluetooth na unataka kuongezea? Easy sana na inawezekana pia, kwa mafundi ninaweza kuwaelekeza.

Lakini pia music system yako ulipenda itoe mp5, yaani picture, video inawezekana pia[emoji3][emoji3].
Hususani wale wenye TV za kizamani yaani unachomeka flash disk yako kwenye subwoofer, unapata mdundo alafu kuna cable itatoka kwenye subwoofer hadi kwenye TV yako.

Stay here.
More good things are here.
Welcome.

View attachment 1921368
View attachment 1921369
 

Mkuu sikua nmeiona hi
Kwahyo hapo box moja itabeba speaker5 jumla[emoji848][emoji848]
Any hapo lazima ziungwe series tu maan ukisema ziende parallel zitagoma
Kwahyo tuseme mid bass 4+4 =8ohm ambayo ni sawa
Kisha mmid ya kawaida zikiwa hivyo pia 4+4 ambayo itakua 8
Ukija kuzi parallel itarud 4 ambayo definitely ni fresh
Hiyo h-f isijupe shida kabisa kwakua inapita kwenye capacitors
Lakini ikiwa itatokea ukazikosa(sababu hua zinakua hazipatikani pia) basi utachukua hizo hizo 4ohms lakin ndani uta series na resistor ya 2.2 au 4ohms ili ifidie hiyo gape

Ingia google andika 4ohms resistor utaziona
Kwahyo zitaungwa series na speaker ili kufidia ile ohms4 inayopelea
Kwakua amplify inachohesabu ni ohms pekee
Usiumize kichwa mambo yanawezekana in easy way
 
Hivi hili neno bridgeable linamaanishaga nini kwnye amplifier?

@korokwincho
Mkuu nikujibu kwa kutumia mfano!
Kwa mfano wew si unamikono miwili
Kila mkono una uwezo wake wakufanya kazi
Ukifanyiwa bridge ni kua wanaukata mkono mmoja ili ule unaobaki utoe nguvu mala mbili ya ile ya awali
Mfano wa pili
Kuna scania 2 unatakazivute mizigo mmoja mkubwa
Uki bridge wana unachukua mashinne ya huku unaipa kwenye ile nyingine ili iwe powerful kuvuta vema mzigo huo

Kwenye amplify kuna kitu kinaitwa channel
Kikawaida zinakua 2
Kwahyo kama zipo mbili na una speaker moja yenye powe una bridge channel ili itoke moja yenye power

Umepata mwanga kidogo?
 
Hivi hili neno bridgeable linamaanishaga nini kwnye amplifier?

Lakini kabla hujachomeka speaker lazima uiambie kwanza amply kama unaibridge kwakuselect selector
Ukiweka speaker in blidge kabla yakuselect hapo tena ni majanga
 
Nataka home theatre au sound bar nzuri nikiwa ndani nachek movie nijihisi niko cinema theatre
 
Mkuu nielekeze kuhusu dolby

Dolby ni mfumo wa sauti na mwanga katika usikivu makini na safi
Yaani ikiwa unataka kutengeneza movie yako unaweza kutumia mfumo wao kwaajiri yakupata sound nzuri na makini isio kela
Ndio maan ikiwa unatumia cd za kingwendu kwenye home theater utasikia speaker mbili pekee
Kwakua hizo cd hazinamfumo wa 5.1 from dolby
Lakini pia
Unaweza install program ya dolby kwenye pc ili isaidie ku ongeZa sounds improvement


Umeelewa kidogo?
 
Reactions: Lee
Nimelewaa vizuri...ata movie nying za sasa zina huo mfumo
 

Nafikiri hukunielewa au lbda upitie tena hiyo reply.
Kumbuka tutatumia crossover kudevide aina za sound. Yaani speaker moja itoe midrange, twitter moja itoe full range na speaker mbili zitoe midbass. Hapa jumla ni drive 4.
Sasa sidhani kama zote zitaweza kuwekwa kwenye series. Ila hizi mbili yaani midbass kwa kuwa zote zitatoa sauti moja naweza kuziweka kwenye mfumo wa series. Ndio maana nikasema kwa kufikiri kwangu sina budi kutafuta midbass za 8ohms. Ili nikiweka kwenye series itakuwa 16ohms then narudi kuunga kawaida kumbuka inatka kwenye crossover hapa naunga tena midrange ya 8ohms so kimahesabu yenu itapungua tena kuwa 8ohms halafu namaliza na fullrange(twitter) hapa sasa ndio total floorstanding inakuwa na 4ohms. (Hiyo ishu ya kufidia naweza kuifanya labda ili walau full niirudishe speaker nzima kusomwa ohms 6.)
Ndio maana nikasema labda na ww nikuachie unipangie hapo je inakubali vyema kama nilivyofikiri.
(Drive zote itabidi nitafute za 8ohms)
Nahitaji midbass mbili za 8ohms, midrange moja ya 8ohms na full range(twitter) moja ya 8 au 4ohms ikae kwenye box speaker moja.
 
Ooohhh nimekupata mkuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…