Niulize chochote kuhusu Subwoofer na Sounds system

Niulize chochote kuhusu Subwoofer na Sounds system

kelphin

JF-Expert Member
Joined
Dec 24, 2019
Posts
9,872
Reaction score
16,319
Ikiwa inakusumbua,ikiwa unataka kufahamu chochote kinachokutatiza.

Karibu
images.jpg


Nieleze kidogo kuhusu subwoofer
Je, unataka kununua, basi zingatia haya.

Zipo za aina mbili old model na digital. Siyo majina hapana ,yaani inaweza kua rising,seapiano,codjec,aborder au vyovyote Ila itakua digital au old model.

Hizo digital ni Aina ya subwoofer ambayo inamuundo wakisasa ,mala nyingi utakuta Ina (nob) kivingilisho Cha sauti kimoja tu.

Ila kinafanya multipurpose, ukibonyeza hyo hiyo nob unaweza ongeza sauti ,kuongeza bass, na mid.
kifupi mambo yote ni in one button.

Faida yake ni kuwa, aina ya power supply yake Ni ilitaka ifanane na ya home theater(Ila haijawahi[emoji2][emoji2inakua na umeme mnyoofu kidogo.

Zinakua na music mkubwa na mdundo zaidi ni digital,yaani yakisasa,
lakini pia display yake ni LCD haitumii umeme mwingi.

Je utaijuaje?
Nob ya kuongezea sauti ni moja tu na zaidi utakuta button za menu na input inategemeana). Ukiigeuza nyuma ina kiplastic kidogo kilichozungushwa nati, yaani ikiwa italeta shida fundi huku nyuma hafungui mfuniko wote wa nyuma, hufungua ki plastic tu hapo nyuma ndio kimebeba card zoote na subwoofer.

Hasara zake
  1. Ikitokea imeharibu card yake hauwez kubadilisha ,sababu ndani Ina circuit Kama ya phone mafundi weeengi hawana(hatuna) technology yakuitengeneza kwahyo unaenda dukani unanunua Tena kard na si chini ya 40000.
  2. Ila ukifika unaipachika tu huangaiki.
  3. Inahitaji utulie ili uioperate maana inatumia single nob.
  4. Speaker yake ya bass huwekwa ohms ndogo ili idunde sana kwahiyo usipende kuweka sauti kubwa Sana kwa muda mrefu.

Aina ya pili ndio zile old model
Hizo zinaitwa dunda udundavyo ni nzuri kwenye uzuri wake. Yenyewe ukiingalia utakuta Ina nob yaani vile vyakuongezea sauti zaidi ya kimoja. Yaani cha master volume, bass, tweeter na mic, na ukivizungusha vinafika mwisho.

Yenyewe ndani power supply yake ni ya kawaida, inatumia mtransformer wake na diodes za kawaida. kisha umeme huingia kwenye capacitor ndio unaanza kusambazwa ndani. Yaweza kuwa Seapiano, Codjec Aborder au vyovyote. Ukiigeuza nyuma mfuniko wote unafunguka wa nyuma.

Faida yake
  1. ikizingua unaiweza kuirekebisha kiurahisi tu
  2. Zinavumilia sana
  3. Hata muziki upo pia
  4. Rahisi kuitumia
Hasara zake
  1. Display yake ni VFD kama ni seapiano hapa mbele inakioo,inavyoimba Kuna vitu vinacheza cheza kwenye kioo(hii ni kwa baadhi ya subwoofer)
  2. Muonekano wake ni wakizamani ikilinganishwa na hizi mpya

Soma hi pia [emoji1427]
Ndani ya subwoofer panya hupenda kuishi humo, huzaliana na kuleta hitilafu kwa kukata nyaya na kula speaker.
Waya wa speaker una chumvi chumvi hivyo akiingia hauachi.

Simple way jinsi ya kudhibiti
Pale kwenye tobo kuna ki corn cha duara huwa wanakipachika unaweza kukitoa kwa kufuata mpangilio ufuatao:

  1. Chukua maji ya moto kidogo na kitambaa, kichovye kitambaa kwenye maji kisha kikande kuzunguka mduara kwa dakika tano.
  2. Kisha chukua kisu, tumia ncha yake kuingiza pembezoni mwa mduara bila kuikwajua. Huku ukiinua kidogo kidogo kuzunguka corn nzima,ukisha kitoa kitoboe vitundu vidogo kukizunguka upande wa ndani(sio Huku uliko Kanda kwa maji).
  3. Ukisha kitoa chukua waya mgumu usuke upande wa ndani kuzunguka uwazi wa duara wote mule ulimotoboa, kisuke hakikisha unaacha vyumba vidogovidogo kiasi kwamba kinaweza kupita kidore kidogo tu.
  4. Paka gundi upande wa ndani, huku ulikokua unakanda na maji kisha kibandike tena kama kilivyokuwa.

NB: Hii ni kwazile subwoofer kama pichani hapo juu, ambazo hutolea upepo pembeni kwenye kiduara. Wale zinazotolea mbele chini ni habari nyingine.

***
Kiasi chake mtanielewaView attachment 1560194View attachment 1560195

Some updates,
Je, music system yako haina bluetooth na unataka kuongezea? Easy sana na inawezekana pia, kwa mafundi ninaweza kuwaelekeza.

Lakini pia music system yako ulipenda itoe mp5, yaani picture, video inawezekana pia[emoji3][emoji3].
Hususani wale wenye TV za kizamani yaani unachomeka flash disk yako kwenye subwoofer, unapata mdundo alafu kuna cable itatoka kwenye subwoofer hadi kwenye TV yako.

Stay here.
More good things are here.
Welcome.

View attachment 1921368
View attachment 1921369
 
Ziada nilijaribu kutafuta speakers kwa bongo nzuri kupata inakuwa shida nyingi ni za gari. Ila nikakuta hizi ambazo hutumika kwenye sea piano za kichina moja ni 25000. Watt 80-100 nchi 8. Ila nikaja gundua kuwa ohms nyingi ni 2. Zingeweza nifaa kwa kazi yangu ila changamoto ni hapo kwenye ohms. Ila kwa kuwa umeniambia zipo za ohms 4,6 na 8 pia, ngoja niendelee kucheki.

Nilizoziona ni hizo ambazo zinakuja empty kwa kureplace kwa wale ambao labda ziliaribika. Mpya ni 25000, bei yake si mbaya. Vipi nikipata za ohms 4,6 au 8 si zitanifaa? Nahitaji nne tu kwa ajili ya Front R na Front L (floorstanding).

Mkuu zunguka kwa mafundi tv na redio utazipata kama hizo unazozitaka
Ila zile za nch8 hua ni kwajiri ya low freq sidhan kama utapata unachokitaka
Zipo hizo unazozitaka kwa mafundi humo
 
Mkuu zunguka kwa mafundi tv na redio utazipata kama hizo unazozitaka
Ila zile za nch8 hua ni kwajiri ya low freq sidhan kama utapata unachokitaka
Zipo hizo unazozitaka kwa mafundi humo
Ok, ila kwa mafundi si used? Me nataka mpya.
Low frequency hasa itakuwa poa maana kumbuka pia nataka pia kuwa na za high frequency.
 
Zipo za aina mbili
Active na passive
Active ipo mfano wa DVD players inakuna na tuning nob kadhh mbele na ili ifanye kazi inahitaji umeme
Ila passive crossover ndio hizo unazozisemea
Na kila moja inafanya kwa nafasi yake
Ikiwa utaitoa lazima madhala yatokee hasa hiyo passive
Passive ww si unaweza kutengeneza?
 
Crossover ni device ambayo inagawanisha signals.
Ikumbukwe mziki unapotengenezwa studio hua ni 2.0channel
Yaan hua ni stereo kama ule unaosikiliza ukivaa earphone
Ila sasa wewe unataka mziki usikikike ki tofauti yaani speaker moja i dunde
Moja iimbe mid nyingine tweeter Kwahyo crossover itakuchukua hizo signal za stereo kisha yenyewe itazitengeneza zitoke high mid na bass
Ni vyema sana kua nayo kwa sound kali
Kabisa,
Hapa nataka upande wa Speaker kubwa za mbele, mbili zidunde moja iimbe mid na nyingine twitter. Kwa kila moja. So, ina maana nahitaji crossover ya 3-way?

Surround na center nataka moja iimbe mid na twitter kwa kila moja. So hapa nahitaji 2-way crossover?

Amplifier ina chanel 6. Chanell moja ni passive subwoofer. So, sub nitaunda tu box kama lilivyo bila crossover maana hii haina mgawanyo?

Ndani ya box wengine huweka cotton au sufi. Hii ina umuhimu kiasi gani?
 
Kabisa,
Hapa nataka upande wa Speaker kubwa za mbele, mbili zidunde moja iimbe mid na nyingine twitter. Kwa kila moja. So, ina maana nahitaji crossover ya 3-way?

Surround na center nataka moja iimbe mid na twitter kwa kila moja. So hapa nahitaji 2-way crossover?

Amplifier ina chanel 6. Chanell moja ni passive subwoofer. So, sub nitaunda tu box kama lilivyo bila crossover maana hii haina mgawanyo?

Ndani ya box wengine huweka cotton au sufi. Hii ina umuhimu kiasi gani?

Yess utahitaji 3way ili igawanye hizo freq kwenye music system yako kuna sehem ya woofer?
Cotton na sufi ni kwaajiri yakupunguza mwangwi
Lakini kwenye bass huongeza low freq pia
 
Back
Top Bottom