Niulize chochote kuhusu Subwoofer na Sounds system

Niulize chochote kuhusu Subwoofer na Sounds system

kelphin

JF-Expert Member
Joined
Dec 24, 2019
Posts
9,872
Reaction score
16,319
Ikiwa inakusumbua,ikiwa unataka kufahamu chochote kinachokutatiza.

Karibu
images.jpg

Nieleze kidogo kuhusu subwoofer
Je, unataka kununua, basi zingatia haya.

Zipo za aina mbili old model na digital. Siyo majina hapana ,yaani inaweza kua rising,seapiano,codjec,aborder au vyovyote Ila itakua digital au old model.

Hizo digital ni Aina ya subwoofer ambayo inamuundo wakisasa ,mala nyingi utakuta Ina (nob) kivingilisho Cha sauti kimoja tu.

Ila kinafanya multipurpose, ukibonyeza hyo hiyo nob unaweza ongeza sauti ,kuongeza bass, na mid.
kifupi mambo yote ni in one button.

Faida yake ni kuwa, aina ya power supply yake Ni ilitaka ifanane na ya home theater(Ila haijawahi[emoji2][emoji2inakua na umeme mnyoofu kidogo.

Zinakua na music mkubwa na mdundo zaidi ni digital,yaani yakisasa,
lakini pia display yake ni LCD haitumii umeme mwingi.

Je utaijuaje?
Nob ya kuongezea sauti ni moja tu na zaidi utakuta button za menu na input inategemeana). Ukiigeuza nyuma ina kiplastic kidogo kilichozungushwa nati, yaani ikiwa italeta shida fundi huku nyuma hafungui mfuniko wote wa nyuma, hufungua ki plastic tu hapo nyuma ndio kimebeba card zoote na subwoofer.

Hasara zake
  1. Ikitokea imeharibu card yake hauwez kubadilisha ,sababu ndani Ina circuit Kama ya phone mafundi weeengi hawana(hatuna) technology yakuitengeneza kwahyo unaenda dukani unanunua Tena kard na si chini ya 40000.
  2. Ila ukifika unaipachika tu huangaiki.
  3. Inahitaji utulie ili uioperate maana inatumia single nob.
  4. Speaker yake ya bass huwekwa ohms ndogo ili idunde sana kwahiyo usipende kuweka sauti kubwa Sana kwa muda mrefu.

Aina ya pili ndio zile old model
Hizo zinaitwa dunda udundavyo ni nzuri kwenye uzuri wake. Yenyewe ukiingalia utakuta Ina nob yaani vile vyakuongezea sauti zaidi ya kimoja. Yaani cha master volume, bass, tweeter na mic, na ukivizungusha vinafika mwisho.

Yenyewe ndani power supply yake ni ya kawaida, inatumia mtransformer wake na diodes za kawaida. kisha umeme huingia kwenye capacitor ndio unaanza kusambazwa ndani. Yaweza kuwa Seapiano, Codjec Aborder au vyovyote. Ukiigeuza nyuma mfuniko wote unafunguka wa nyuma.

Faida yake
  1. ikizingua unaiweza kuirekebisha kiurahisi tu
  2. Zinavumilia sana
  3. Hata muziki upo pia
  4. Rahisi kuitumia
Hasara zake
  1. Display yake ni VFD kama ni seapiano hapa mbele inakioo,inavyoimba Kuna vitu vinacheza cheza kwenye kioo(hii ni kwa baadhi ya subwoofer)
  2. Muonekano wake ni wakizamani ikilinganishwa na hizi mpya

Soma hi pia [emoji1427]
Ndani ya subwoofer panya hupenda kuishi humo, huzaliana na kuleta hitilafu kwa kukata nyaya na kula speaker.
Waya wa speaker una chumvi chumvi hivyo akiingia hauachi.

Simple way jinsi ya kudhibiti
Pale kwenye tobo kuna ki corn cha duara huwa wanakipachika unaweza kukitoa kwa kufuata mpangilio ufuatao:

  1. Chukua maji ya moto kidogo na kitambaa, kichovye kitambaa kwenye maji kisha kikande kuzunguka mduara kwa dakika tano.
  2. Kisha chukua kisu, tumia ncha yake kuingiza pembezoni mwa mduara bila kuikwajua. Huku ukiinua kidogo kidogo kuzunguka corn nzima,ukisha kitoa kitoboe vitundu vidogo kukizunguka upande wa ndani(sio Huku uliko Kanda kwa maji).
  3. Ukisha kitoa chukua waya mgumu usuke upande wa ndani kuzunguka uwazi wa duara wote mule ulimotoboa, kisuke hakikisha unaacha vyumba vidogovidogo kiasi kwamba kinaweza kupita kidore kidogo tu.
  4. Paka gundi upande wa ndani, huku ulikokua unakanda na maji kisha kibandike tena kama kilivyokuwa.

NB: Hii ni kwazile subwoofer kama pichani hapo juu, ambazo hutolea upepo pembeni kwenye kiduara. Wale zinazotolea mbele chini ni habari nyingine.

***
Kiasi chake mtanielewaView attachment 1560194View attachment 1560195

Some updates,
Je, music system yako haina bluetooth na unataka kuongezea? Easy sana na inawezekana pia, kwa mafundi ninaweza kuwaelekeza.

Lakini pia music system yako ulipenda itoe mp5, yaani picture, video inawezekana pia[emoji3][emoji3].
Hususani wale wenye TV za kizamani yaani unachomeka flash disk yako kwenye subwoofer, unapata mdundo alafu kuna cable itatoka kwenye subwoofer hadi kwenye TV yako.

Stay here.
More good things are here.
Welcome.

View attachment 1921368
View attachment 1921369
 
[emoji23][emoji23][emoji23] mkuu punguza hasira [emoji23]

Anyway nakujibu moja moja
Hasira kivipi mkuu.

Me miziki ya kichina naitumia ni vile umaskini, sijawahi ielewa. Nilikuta mtu ana surround sound kama pichani hapo. Aisee kwa chizi mziki yeyote lazima udate.
 
Midrange n speaker ambazo zinaweza kucheza kati ya freq 250-2000 hivi
Lakini full range ni tweeter speakers
Ikumbukwe speaker zote lazima kuwe na coil ndani lakin utofauti unakuja kwenye karatas na spider ya speaker
Ikiwa karatasi haitakua na mpira pembezoni speaker hiyo itakua fullrange na ukiilizimisha kupiga midbass itakatika pembeni
Kwahyo midrange ni speaker normally ambayo inaweza cheza low freq at yhe same time ikafanya full pia ikitegemea setting ya crossover ila fullrang ni full pekee
Ila midbass ni speaker ambazo zinaweza kucheza both
Zenyewe zinakua na mpira pembezoni
Na spider yake inakua inamatuta yakaribu
Hivyo inawwza kucheza low freq na isipate shida yoyote
Kwahyo
Fullrange inakupa tweeter kari pekeea na inakua na ki vorn hivi
Midrange inakua kati inaweza kucheza low ila sio kavu sana
Ila midbass inakuj na mpira kabisa kua inaweza dunda na isilete shida
Ikiwa speaker ni midrange ukaipa freq ya mid bass basi mayokeo yake itaimba ila itapangua coil

Nakuhusu kuijua ni kipitia printed paper lazima mtengenezaji akuambie hiyo ni mahususi kwa kazi gani
Ila ukiwa mzoefu unaweza angalia spider na ile karatasi ya juu tu
 
Naomba unifafanulie kuhusu hapa.

Midrange
Fullrange
Midbass.

Najuaje kuwa hii speaker ni midrange,fullrange au midbass.

Sub za kichina nyingi ni ohms 2 watts 80 - 100 tu kwa sub na zile chanel mbili ni ohms 4 tu kwa kila moja. Kwanini wanatumia sana 2ohms?

Amplifier nyingi zimeandikwa tumia 4 - 16 ohms.
Kama nataka kuunda mziki wangu binafsi kati ya 4 ohms na 8 ohms unashauri nitumie speaker ya ohms ngapi?
Nataka niwe na floorstanding yenye driver tatu. Midrange 2, full range 1, twitter 1.
Kila driver (midrange) ina watt 100. Je floor standing moja itakuwa na jumla ya watt ngapi au inabaki kuwa watt 100?

How about crossover, ni muhimu kuitumia? Mfano kwa floor standing hapo nitahitaji cossover ya njia ngapi?

Center chanel nahitaji full range mbili twitter 1.
Surround speakers(bookshelf) full range 1, twitter 1 kwa kila moja.
Nazo bado ni muhimu kutumia crossover.

Mwisho kuna vitu gani muhimu napaswa kuzingatia?View attachment 1841876

Hapana subwoofer zipo na aina nyingi
Nyingi zake ni 8ohms
4ohms na 2ohms
Ila kaka haaaweki hivyo kwa kupenda tu kuweka kuna specification zinazowaongoza kufanya hivyo
Ndani ya subwoofer kuna amplify
Amplify inapotengenezwa hutumia either ic,transistors sasa kama utatumia ic kila ic inakua na sheria zake na ukikiuka utapata moshiii[emoji23]
Mfano mdogo sana suka amp ya tda 2030 kisha ipe 25v afu weka hivo 2ohms afu uone moshi
Kwahyo ikiwa utasuka ya ic kila ic inakuja na matakwa yeke
Ivyo ni wew tu kuchagua
Nkuambie tu kua subwoofer zinazotumia transistor mala nyingi inakua inataka utumie 4ohms
Ikiwa inatumia ic hapo ndio mziki unapoanzia kwakua kila ic inakua na guide zake
Na wanakuambia pale kwenye maelezo yao watengenezaje
Pia kuna vitu vinaitwa bridge kwenye amp
Kwahyo kifupi hawatumii tu speaker kwa kupenda Hapana kuna specifications zinafuatwa
 
Naomba unifafanulie kuhusu hapa.

Midrange
Fullrange
Midbass.

Najuaje kuwa hii speaker ni midrange,fullrange au midbass.

Sub za kichina nyingi ni ohms 2 watts 80 - 100 tu kwa sub na zile chanel mbili ni ohms 4 tu kwa kila moja. Kwanini wanatumia sana 2ohms?

Amplifier nyingi zimeandikwa tumia 4 - 16 ohms.
Kama nataka kuunda mziki wangu binafsi kati ya 4 ohms na 8 ohms unashauri nitumie speaker ya ohms ngapi?
Nataka niwe na floorstanding yenye driver tatu. Midrange 2, full range 1, twitter 1.
Kila driver (midrange) ina watt 100. Je floor standing moja itakuwa na jumla ya watt ngapi au inabaki kuwa watt 100?

How about crossover, ni muhimu kuitumia? Mfano kwa floor standing hapo nitahitaji cossover ya njia ngapi?

Center chanel nahitaji full range mbili twitter 1.
Surround speakers(bookshelf) full range 1, twitter 1 kwa kila moja.
Nazo bado ni muhimu kutumia crossover.

Mwisho kuna vitu gani muhimu napaswa kuzingatia?View attachment 1841876

Kuhusu watts hapo sijaelewa vyema naomba uulize vema zaidi

Ikiwa unataka kusuka amplify sio kama wew ndio utachagua ohms hapana!!!
Ila aina ya amp utakayoisuka ndio itakupeleka kwenye aina fulan ya speaker
Kuna amp zinataka 2,4,8,16
Ila nikuambie tu
Ikiwa amplify itataka uweke 4ohms wew ukaweka 8-16 utakua umezidishavhivyo sauti haitakua kubwa
Ila amplify haiwezi kuchemka
Ila ikiwa umeweka 2ohms sehemu ya 8ohms[emoji23][emoji23] utapat sound kubwa inayokaribiana kabisa na moshi
 
Crossover ni device ambayo inagawanisha signals.
Ikumbukwe mziki unapotengenezwa studio hua ni 2.0channel
Yaan hua ni stereo kama ule unaosikiliza ukivaa earphone
Ila sasa wewe unataka mziki usikikike ki tofauti yaani speaker moja i dunde
Moja iimbe mid nyingine tweeter Kwahyo crossover itakuchukua hizo signal za stereo kisha yenyewe itazitengeneza zitoke high mid na bass
Ni vyema sana kua nayo kwa sound kali
 
Naomba unifafanulie kuhusu hapa.

Midrange
Fullrange
Midbass.

Najuaje kuwa hii speaker ni midrange,fullrange au midbass.

Sub za kichina nyingi ni ohms 2 watts 80 - 100 tu kwa sub na zile chanel mbili ni ohms 4 tu kwa kila moja. Kwanini wanatumia sana 2ohms?

Amplifier nyingi zimeandikwa tumia 4 - 16 ohms.
Kama nataka kuunda mziki wangu binafsi kati ya 4 ohms na 8 ohms unashauri nitumie speaker ya ohms ngapi?
Nataka niwe na floorstanding yenye driver tatu. Midrange 2, full range 1, twitter 1.
Kila driver (midrange) ina watt 100. Je floor standing moja itakuwa na jumla ya watt ngapi au inabaki kuwa watt 100?

How about crossover, ni muhimu kuitumia? Mfano kwa floor standing hapo nitahitaji cossover ya njia ngapi?

Center chanel nahitaji full range mbili twitter 1.
Surround speakers(bookshelf) full range 1, twitter 1 kwa kila moja.
Nazo bado ni muhimu kutumia crossover.

Mwisho kuna vitu gani muhimu napaswa kuzingatia?View attachment 1841876

@RReigns mkuu wapi bado?
 
Hasira kivipi mkuu.

Me miziki ya kichina naitumia ni vile umaskini, sijawahi ielewa. Nilikuta mtu ana surround sound kama pichani hapo. Aisee kwa chizi mziki yeyote lazima udate.

Unaweza kusuka amp mkuu?
 
Kuhusu watts hapo sijaelewa vyema naomba uulize vema zaidi

Ikiwa unataka kusuka amplify sio kama wew ndio utachagua ohms hapana!!!
Ila aina ya amp utakayoisuka ndio itakupeleka kwenye aina fulan ya speaker
Kuna amp zinataka 2,4,8,16
Ila nikuambie tu
Ikiwa amplify itataka uweke 4ohms wew ukaweka 8-16 utakua umezidishavhivyo sauti haitakua kubwa
Ila amplify haiwezi kuchemka
Ila ikiwa umeweka 2ohms sehemu ya 8ohms[emoji23][emoji23] utapat sound kubwa inayokaribiana kabisa na moshi
Nina midrnge au midbass mbili nimezifunga kwenye box moja na full range 1
Mid bass watt 100 kila moja na labda full range watt 50.
Hapa hii floorstanding inasomeka watt ngapi? Shida yangu iwe kama hivi. kumbuka amplifier yangu imenipa kiwango cha watt kwa main speakers(Front Right and left) nichopaswa kutumia. so sitaki kucheza mbali na masherti niliyopewa wakati naunda.
1625424930488.jpg
 
Nina midrnge au midbass mbili nimezifunga kwenye box moja na full range 1
Mid bass watt 100 kila moja na labda full range watt 50.
Hapa hii floorstanding inasomeka watt ngapi? Shida yangu iwe kama hivi. kumbuka amplifier yangu imenipa kiwango cha watt kwa main speakers(Front Right and left) nichopaswa kutumia. so sitaki kucheza mbali na masherti niliyopewa wakati naunda.View attachment 1841951

Nina midrnge au midbass nimezifunga kwenye box moja na full range 1
Mid bass watt 100 kila moja na labda full range watt 50.
Hapa hii floorstanding inasomeka watt ngapi? Shida yangu iwe kama hivi. kumbuka amplifier yangu imenipa kiwango cha watt kwa main speakers(Front Right and left) nichopaswa kutumia. so sitaki kucheza mbali na masherti niliyopewa wakati naunda.View attachment 1841951

Mkuu kwakua waya wa hizo speaker ni mmja tu Kwahyo hizo speaker zinakua parallel Kwahyo watts zitajuishwa kwa hyo hapo utakua na watts 150 kwakua zipo kwenye njia moja ya sauti
 
Ziada nilijaribu kutafuta speakers kwa bongo nzuri kupata inakuwa shida nyingi ni za gari. Ila nikakuta hizi ambazo hutumika kwenye sea piano za kichina moja ni 25000. Watt 80-100 nchi 8. Ila nikaja gundua kuwa ohms nyingi ni 2. Zingeweza nifaa kwa kazi yangu ila changamoto ni hapo kwenye ohms. Ila kwa kuwa umeniambia zipo za ohms 4,6 na 8 pia, ngoja niendelee kucheki.

Nilizoziona ni hizo ambazo zinakuja empty kwa kureplace kwa wale ambao labda ziliaribika. Mpya ni 25000, bei yake si mbaya. Vipi nikipata za ohms 4,6 au 8 si zitanifaa? Nahitaji nne tu kwa ajili ya Front R na Front L (floorstanding).
 
Crossover kile kisakiti kitumikacho kugawanya njia ndani ya speaker kuwa hii iende kwenye twitter hii iende kwenye midrange na hii labda iende kwenye midbass. Au hata ukiunga kienyeji haina shida?

Zipo za aina mbili
Active na passive
Active ipo mfano wa DVD players inakuna na tuning nob kadhh mbele na ili ifanye kazi inahitaji umeme
Ila passive crossover ndio hizo unazozisemea
Na kila moja inafanya kwa nafasi yake
Ikiwa utaitoa lazima madhala yatokee hasa hiyo passive
 
Back
Top Bottom