Niulize chochote kuhusu Subwoofer na Sounds system

Niulize chochote kuhusu Subwoofer na Sounds system

kelphin

JF-Expert Member
Joined
Dec 24, 2019
Posts
9,872
Reaction score
16,319
Ikiwa inakusumbua,ikiwa unataka kufahamu chochote kinachokutatiza.

Karibu
images.jpg

Nieleze kidogo kuhusu subwoofer
Je, unataka kununua, basi zingatia haya.

Zipo za aina mbili old model na digital. Siyo majina hapana ,yaani inaweza kua rising,seapiano,codjec,aborder au vyovyote Ila itakua digital au old model.

Hizo digital ni Aina ya subwoofer ambayo inamuundo wakisasa ,mala nyingi utakuta Ina (nob) kivingilisho Cha sauti kimoja tu.

Ila kinafanya multipurpose, ukibonyeza hyo hiyo nob unaweza ongeza sauti ,kuongeza bass, na mid.
kifupi mambo yote ni in one button.

Faida yake ni kuwa, aina ya power supply yake Ni ilitaka ifanane na ya home theater(Ila haijawahi[emoji2][emoji2inakua na umeme mnyoofu kidogo.

Zinakua na music mkubwa na mdundo zaidi ni digital,yaani yakisasa,
lakini pia display yake ni LCD haitumii umeme mwingi.

Je utaijuaje?
Nob ya kuongezea sauti ni moja tu na zaidi utakuta button za menu na input inategemeana). Ukiigeuza nyuma ina kiplastic kidogo kilichozungushwa nati, yaani ikiwa italeta shida fundi huku nyuma hafungui mfuniko wote wa nyuma, hufungua ki plastic tu hapo nyuma ndio kimebeba card zoote na subwoofer.

Hasara zake
  1. Ikitokea imeharibu card yake hauwez kubadilisha ,sababu ndani Ina circuit Kama ya phone mafundi weeengi hawana(hatuna) technology yakuitengeneza kwahyo unaenda dukani unanunua Tena kard na si chini ya 40000.
  2. Ila ukifika unaipachika tu huangaiki.
  3. Inahitaji utulie ili uioperate maana inatumia single nob.
  4. Speaker yake ya bass huwekwa ohms ndogo ili idunde sana kwahiyo usipende kuweka sauti kubwa Sana kwa muda mrefu.

Aina ya pili ndio zile old model
Hizo zinaitwa dunda udundavyo ni nzuri kwenye uzuri wake. Yenyewe ukiingalia utakuta Ina nob yaani vile vyakuongezea sauti zaidi ya kimoja. Yaani cha master volume, bass, tweeter na mic, na ukivizungusha vinafika mwisho.

Yenyewe ndani power supply yake ni ya kawaida, inatumia mtransformer wake na diodes za kawaida. kisha umeme huingia kwenye capacitor ndio unaanza kusambazwa ndani. Yaweza kuwa Seapiano, Codjec Aborder au vyovyote. Ukiigeuza nyuma mfuniko wote unafunguka wa nyuma.

Faida yake
  1. ikizingua unaiweza kuirekebisha kiurahisi tu
  2. Zinavumilia sana
  3. Hata muziki upo pia
  4. Rahisi kuitumia
Hasara zake
  1. Display yake ni VFD kama ni seapiano hapa mbele inakioo,inavyoimba Kuna vitu vinacheza cheza kwenye kioo(hii ni kwa baadhi ya subwoofer)
  2. Muonekano wake ni wakizamani ikilinganishwa na hizi mpya

Soma hi pia [emoji1427]
Ndani ya subwoofer panya hupenda kuishi humo, huzaliana na kuleta hitilafu kwa kukata nyaya na kula speaker.
Waya wa speaker una chumvi chumvi hivyo akiingia hauachi.

Simple way jinsi ya kudhibiti
Pale kwenye tobo kuna ki corn cha duara huwa wanakipachika unaweza kukitoa kwa kufuata mpangilio ufuatao:

  1. Chukua maji ya moto kidogo na kitambaa, kichovye kitambaa kwenye maji kisha kikande kuzunguka mduara kwa dakika tano.
  2. Kisha chukua kisu, tumia ncha yake kuingiza pembezoni mwa mduara bila kuikwajua. Huku ukiinua kidogo kidogo kuzunguka corn nzima,ukisha kitoa kitoboe vitundu vidogo kukizunguka upande wa ndani(sio Huku uliko Kanda kwa maji).
  3. Ukisha kitoa chukua waya mgumu usuke upande wa ndani kuzunguka uwazi wa duara wote mule ulimotoboa, kisuke hakikisha unaacha vyumba vidogovidogo kiasi kwamba kinaweza kupita kidore kidogo tu.
  4. Paka gundi upande wa ndani, huku ulikokua unakanda na maji kisha kibandike tena kama kilivyokuwa.

NB: Hii ni kwazile subwoofer kama pichani hapo juu, ambazo hutolea upepo pembeni kwenye kiduara. Wale zinazotolea mbele chini ni habari nyingine.

***
Kiasi chake mtanielewaView attachment 1560194View attachment 1560195

Some updates,
Je, music system yako haina bluetooth na unataka kuongezea? Easy sana na inawezekana pia, kwa mafundi ninaweza kuwaelekeza.

Lakini pia music system yako ulipenda itoe mp5, yaani picture, video inawezekana pia[emoji3][emoji3].
Hususani wale wenye TV za kizamani yaani unachomeka flash disk yako kwenye subwoofer, unapata mdundo alafu kuna cable itatoka kwenye subwoofer hadi kwenye TV yako.

Stay here.
More good things are here.
Welcome.

View attachment 1921368
View attachment 1921369
 
Ndiyo ni kitu kidogo Sana Sema ukiwa mtu WA clear audio ndo Utahis ila ni kwenye Bluetooth tu ila average person hawez kugundua hili tatizo maana ni mpaka uisogelee hyo spika ndo utaisikia. Ila vingine vipo sawa
Itakuwa ni defect tu toka kiwandani which means ukibadilisha ungeweza pata isio na shida hio kabisa!

Bass yake ni deep sana nafikiri ni 20kHZ and below na inapiga woofer range notes za 35-45kHZ nafikiri ndio maana waka mount side speakers zile kama woofers!
 
Tatizo Hawana Tena hii Wana ndogo yake ambayo ukiangalia kwa muonekano zinafanana japo hyo ndogo ni 200w na pia box lake ni dogo. Nikikutajia kwa model ndo utanielewa Kuna kt2812 na kt2913. Ila wakiwa wanakuuziwa wanakuambia kt2812 hazina utofaut ila utofaut upo nahis ni masuala ya kodi na kufix price ndo yamewafanya wapunguze ukubwa na power but bei ibak the same
 
Na sio boomy. I napiga deep bass vzr ambapo sjaona kwenye hz Sony au panasonic ht zinauwezo huo labda jbl sound bar ndo nlishaona inauwezo WA hii bass. Ilikuwa ni jbl 5.1 soundbar ambayo spika za surround zinachomoka ndo bass yake na yenyew sio mchezo na ni sound bar
Yeah Sony na Panasonic nimetumia sana naijua ila still hawakamati hio range ya bass!

Siku nilipokuwa napost humu watu waliniona kama nazingua ila kimsingi wengi hawajaskia bass yake ilivyo tight! Nikawaambia tu piteni msikilize muone uhalisia.
 
Kwa mtu anayejua mzik na bass hyo ya kodtec hawez kuiacha ama kuidharau maana weng huwa Wana home theater na sio za maana ni hz dz 350 650 950 za Sony ambazo mzik ni mzur ila still ni entry music. Kuna Sony dav n9200 Ile ni home theater Sema bei yake ni ndefu ni 2M. Ila Tena bora na home theater. Kuna hz sound bar Tena kama za Sony ndo hamna ktu kwenye bass Ata na sound ya kawaida bora Ata hisense kidogo anajitahid. Ila jbl original Ile ni soundbar
 
Yeah Sony kwenye soundbar ni utopolo tu aisee! Nimeskiliza ile ya 600 watts nikajiskia kutapika! Mara 100 lile li hometheatre tu la dz650.

Ile N9200 sijapata kuisikiliza kabisa ila wanadai ni ya moto sana. JBL pia sikusikiliza ile yenye watts za maana ila wanaisifia
 
Tatizo Hawana Tena hii Wana ndogo yake ambayo ukiangalia kwa muonekano zinafanana japo hyo ndogo ni 200w na pia box lake ni dogo. Nikikutajia kwa model ndo utanielewa Kuna kt2812 na kt2913. Ila wakiwa wanakuuziwa wanakuambia kt2812 hazina utofaut ila utofaut upo nahis ni masuala ya kodi na kufix price ndo yamewafanya wapunguze ukubwa na power but bei ibak the same
Hii ndogo yake ndio kt2812 sema nayo sio haba inagonga kichizi
 
Mkuu Nina kodtec Ile kubwa ipo vzr Sema nkiweka Bluetooth speaker moja ya mid unakuwa na kanoise so unakuwa haiimbii clear kama right mid. Ila nkiweka flash au line in hyo noise huisikii kwenye hyo mid. Model yake ni kt2913 nliipendaga kwa sababu ya bass yake ipo deep Ata kuzid my hm theater ila Bluetooth ndo inaniangusha tu. Na kingine naweza nikaunganishaje nikatumia kwenye home theater bass

Pol sana mkuu
Kwenye ic ya Bluetooth inawezekana njia moja haitoki vema
Na je umejaribu kutumia device tofauti n hiyo simu yako na bado ikaleta shida?
Hapo kwenye home theatre sijaelewa
 
Mkuu mm nina home theater Lakin nlikutana na kodtec linapiga bass nzur nkajikuta natoa hela mfukoni nanunua. Kwenye bass hamna subwoofer inaikuta hata hz home theater dz za Sony haxiingii maana I napiga bass kama Ile ya gar na ni 300watt.

Mkuu usikivu wa mziki unachangiwa na vitu vingi
1 power supply
2 amplifier
3 operation amplifier
4 speaker
5box design
Hay mambo yoote yanahesabu na namn yake
Inawezekana mtu akafeli kimojawapo ikawa n noma
 
Wakubwa mambo vipi.

Samahani naomba kuuliza kama kuna list ya the best sound bars, and sub woofers to buy.

Na pia naomba kuuliza kama sound bar inaweza kuwa mbadala wa home theatre au la.

Asante
Soundbar kama una afford tafuta jbl Sema upatikanaj wake nao ni kikwazo maana weng wanaleza hzi za hisense na Sony na LG ambazo ni za kawaida tu
 
Wewe sina shaka mkuu utakuwa unajua maana ya mziki mzuri! Maana mie nilipata experience nzuri sana hasa ya bass ambayo sikutegemea yani kama kuna subwoofer ya kichina inaweza kuwa na mziki mzuri namna ile! Nilishasikiliza miziki mingi mikubwa subwoofers ila ule ulikuwa na extra punch

Subwoofer nyingi za mchina zina boomy bass (bass lililochanganyika na midrange) sio deep bass (bass kavu) halafu husikii ile range ya woofer bass notes ambayo unaipata kwenye zile hi-fi systems!

Hivi mkuu unajua ili upate bass kavu current ya power supply inabid iwe juu sana?
Sasa ili u construct more current unahitaji transformer hizi za duara
Sasa akikuwekea hizo hiyo subwoofer atakuuzia shingapi?
 
Aweke tu sababu hata hio Kodtec inauzwa laki 4 ni sababu ya huo mziki wake mzuri!
 
Back
Top Bottom