Niulize chochote kuhusu Subwoofer na Sounds system

Niulize chochote kuhusu Subwoofer na Sounds system

kelphin

JF-Expert Member
Joined
Dec 24, 2019
Posts
9,872
Reaction score
16,319
Ikiwa inakusumbua,ikiwa unataka kufahamu chochote kinachokutatiza.

Karibu
images.jpg


Nieleze kidogo kuhusu subwoofer
Je, unataka kununua, basi zingatia haya.

Zipo za aina mbili old model na digital. Siyo majina hapana ,yaani inaweza kua rising,seapiano,codjec,aborder au vyovyote Ila itakua digital au old model.

Hizo digital ni Aina ya subwoofer ambayo inamuundo wakisasa ,mala nyingi utakuta Ina (nob) kivingilisho Cha sauti kimoja tu.

Ila kinafanya multipurpose, ukibonyeza hyo hiyo nob unaweza ongeza sauti ,kuongeza bass, na mid.
kifupi mambo yote ni in one button.

Faida yake ni kuwa, aina ya power supply yake Ni ilitaka ifanane na ya home theater(Ila haijawahi[emoji2][emoji2inakua na umeme mnyoofu kidogo.

Zinakua na music mkubwa na mdundo zaidi ni digital,yaani yakisasa,
lakini pia display yake ni LCD haitumii umeme mwingi.

Je utaijuaje?
Nob ya kuongezea sauti ni moja tu na zaidi utakuta button za menu na input inategemeana). Ukiigeuza nyuma ina kiplastic kidogo kilichozungushwa nati, yaani ikiwa italeta shida fundi huku nyuma hafungui mfuniko wote wa nyuma, hufungua ki plastic tu hapo nyuma ndio kimebeba card zoote na subwoofer.

Hasara zake
  1. Ikitokea imeharibu card yake hauwez kubadilisha ,sababu ndani Ina circuit Kama ya phone mafundi weeengi hawana(hatuna) technology yakuitengeneza kwahyo unaenda dukani unanunua Tena kard na si chini ya 40000.
  2. Ila ukifika unaipachika tu huangaiki.
  3. Inahitaji utulie ili uioperate maana inatumia single nob.
  4. Speaker yake ya bass huwekwa ohms ndogo ili idunde sana kwahiyo usipende kuweka sauti kubwa Sana kwa muda mrefu.

Aina ya pili ndio zile old model
Hizo zinaitwa dunda udundavyo ni nzuri kwenye uzuri wake. Yenyewe ukiingalia utakuta Ina nob yaani vile vyakuongezea sauti zaidi ya kimoja. Yaani cha master volume, bass, tweeter na mic, na ukivizungusha vinafika mwisho.

Yenyewe ndani power supply yake ni ya kawaida, inatumia mtransformer wake na diodes za kawaida. kisha umeme huingia kwenye capacitor ndio unaanza kusambazwa ndani. Yaweza kuwa Seapiano, Codjec Aborder au vyovyote. Ukiigeuza nyuma mfuniko wote unafunguka wa nyuma.

Faida yake
  1. ikizingua unaiweza kuirekebisha kiurahisi tu
  2. Zinavumilia sana
  3. Hata muziki upo pia
  4. Rahisi kuitumia
Hasara zake
  1. Display yake ni VFD kama ni seapiano hapa mbele inakioo,inavyoimba Kuna vitu vinacheza cheza kwenye kioo(hii ni kwa baadhi ya subwoofer)
  2. Muonekano wake ni wakizamani ikilinganishwa na hizi mpya

Soma hi pia [emoji1427]
Ndani ya subwoofer panya hupenda kuishi humo, huzaliana na kuleta hitilafu kwa kukata nyaya na kula speaker.
Waya wa speaker una chumvi chumvi hivyo akiingia hauachi.

Simple way jinsi ya kudhibiti
Pale kwenye tobo kuna ki corn cha duara huwa wanakipachika unaweza kukitoa kwa kufuata mpangilio ufuatao:

  1. Chukua maji ya moto kidogo na kitambaa, kichovye kitambaa kwenye maji kisha kikande kuzunguka mduara kwa dakika tano.
  2. Kisha chukua kisu, tumia ncha yake kuingiza pembezoni mwa mduara bila kuikwajua. Huku ukiinua kidogo kidogo kuzunguka corn nzima,ukisha kitoa kitoboe vitundu vidogo kukizunguka upande wa ndani(sio Huku uliko Kanda kwa maji).
  3. Ukisha kitoa chukua waya mgumu usuke upande wa ndani kuzunguka uwazi wa duara wote mule ulimotoboa, kisuke hakikisha unaacha vyumba vidogovidogo kiasi kwamba kinaweza kupita kidore kidogo tu.
  4. Paka gundi upande wa ndani, huku ulikokua unakanda na maji kisha kibandike tena kama kilivyokuwa.

NB: Hii ni kwazile subwoofer kama pichani hapo juu, ambazo hutolea upepo pembeni kwenye kiduara. Wale zinazotolea mbele chini ni habari nyingine.

***
Kiasi chake mtanielewaView attachment 1560194View attachment 1560195

Some updates,
Je, music system yako haina bluetooth na unataka kuongezea? Easy sana na inawezekana pia, kwa mafundi ninaweza kuwaelekeza.

Lakini pia music system yako ulipenda itoe mp5, yaani picture, video inawezekana pia[emoji3][emoji3].
Hususani wale wenye TV za kizamani yaani unachomeka flash disk yako kwenye subwoofer, unapata mdundo alafu kuna cable itatoka kwenye subwoofer hadi kwenye TV yako.

Stay here.
More good things are here.
Welcome.

View attachment 1921368
View attachment 1921369
 
Mkuu kinachokusukuma kununua music system ni watts? Bas itakusumbua
Sababu watts mala nyingi kwenye subwoofer wanadanganya pia sababu ni printed document tu
Je hyo home theater ni ipi
Na subwoofer n ip?
Home theatre ni Sony, sabufa ni sea peano.
We unanishauri vipi? Niangalie vitu gani vya msingi? Nishauri plz!
 
Home theatre ni Sony, sabufa ni sea peano.
We unanishauri vipi? Niangalie vitu gani vya msingi? Nishauri plz!

Mkuu uwezo wako tu
Ila home theatre hua hazisumbui sana kama subwoofer ikiwa hautaikorofisha mwenyewe
Na pindi ikiharibika urekebishaji wake ni adimu sana
Ila subwoofer ziko kommon sana kiasi kwamba zinaweza kurekebishika zikisumbua!
Ki muonekano wa kupendeza na kupamba nyumba bas home theatre inakua pow zaidi
Ki muziki inategemeana true watts ya hizo music system
Kwenye bei home theatre ina ghalama zaid ikitegemana na aina na ubora bia
 
Mkuu uwezo wako tu
Ila home theatre hua hazisumbui sana kama subwoofer ikiwa hautaikorofisha mwenyewe
Na pindi ikiharibika urekebishaji wake ni adimu sana
Ila subwoofer ziko kommon sana kiasi kwamba zinaweza kurekebishika zikisumbua!
Ki muonekano wa kupendeza na kupamba nyumba bas home theatre inakua pow zaidi
Ki muziki inategemeana true watts ya hizo music system
Kwenye bei home theatre ina ghalama zaid ikitegemana na aina na ubora bia
Fresh mkuu. Niko kujifunza vitu hadimu.
 
Kwani ni kweli sabufa tu ndiko wanadanganya watts? Je, Home theatre hawadanganyi Watts?
Kudanganya huko kukoje? Kwa mfano:
Sabufa ikiwa na 500W ina maana inaweza kuwa zaidi ya hapo au chini ya hapo?

Really home theatre zilikua zamani pekee
Sasahiv nyingi pia wameshazichakachua mkuu
Labda upate from trusted companies
Ila zakichina wamezichakachua nying mno
Watts wanaandika ili kuuza pengine
Ila kuna ile truepower ambayo inakuwepo mkuu
Subwoofer hani ina 500watts mkuu ya seapiano
 
Really home theatre zilikua zamani pekee
Sasahiv nyingi pia wameshazichakachua mkuu
Labda upate from trusted companies
Ila zakichina wamezichakachua nying mno
Watts wanaandika ili kuuza pengine
Ila kuna ile truepower ambayo inakuwepo mkuu
Subwoofer hani ina 500watts mkuu ya seapiano
Basi sawa!
 
Kuna mtu kanikumbusha hi

Kati ya vitu vinavoongoza kuharibu subwoofer nyingi za watu ni speaker
Unakuta mtu alikua na subwoofer mwanzo labda ikafa akabaki na zile speaker
Alipokuja kununua redio nyingine akataka kutumia speaker zote
Lakini kumbe basi kadri unavyoongeza spika nyingine kuna mahesab unaharibu
Ikumbukwe kua redio zite ndani zina amplifaya ambayo inaendesha hizo spika
Kwahyo basi hizo amply zinakiwango chake cha ohms inayoitajika
Nyingi hua kati ya 3-4-8ohms
Na kuna mifumo miwili ya kunganisha speaker
Moja inaitwa parallel kama inavyoonekan hapachini
Na nyingine inaitwa series(hi ni ngumu kama sio fundi)kikawaida ukiwa nyumbn utachukua waya wa spika ya pili utaunga kama ilivyoungwa ile yakwanza kwa kuzibana waya zote pamoja

Hiyo ni hatar kwasababu ki mahesabu spika zikiungwa hivyo hushusha ohms yaza hiyo spika

Kwahyo kama redio inataka utumie 4ohms ile iliyokuja nayo
Wewe ukaweka yakwako nyingine ya 4ohms pia hapo utakua unapiga kwa 2ohms ambayo kifupi ni hatar kwa redio yako
Ingawa na sauti itakua kubwa zaidi
IMG_3726.jpg

Ya pili inaitwa series kama tunavyoona hapo chini
Hi ni ngumu[emoji23][emoji23][emoji23] na ninauhakika hua hamuungi
Hi hupunguza sauti ya redio piaila ni nzuri ikiwa unataka kuongezea speak zako binafsi.
IMG_3725.jpg
 
Back
Top Bottom