Niulize chochote kuhusu Subwoofer na Sounds system

Niulize chochote kuhusu Subwoofer na Sounds system

kelphin

JF-Expert Member
Joined
Dec 24, 2019
Posts
9,872
Reaction score
16,319
Ikiwa inakusumbua,ikiwa unataka kufahamu chochote kinachokutatiza.

Karibu
images.jpg


Nieleze kidogo kuhusu subwoofer
Je, unataka kununua, basi zingatia haya.

Zipo za aina mbili old model na digital. Siyo majina hapana ,yaani inaweza kua rising,seapiano,codjec,aborder au vyovyote Ila itakua digital au old model.

Hizo digital ni Aina ya subwoofer ambayo inamuundo wakisasa ,mala nyingi utakuta Ina (nob) kivingilisho Cha sauti kimoja tu.

Ila kinafanya multipurpose, ukibonyeza hyo hiyo nob unaweza ongeza sauti ,kuongeza bass, na mid.
kifupi mambo yote ni in one button.

Faida yake ni kuwa, aina ya power supply yake Ni ilitaka ifanane na ya home theater(Ila haijawahi[emoji2][emoji2inakua na umeme mnyoofu kidogo.

Zinakua na music mkubwa na mdundo zaidi ni digital,yaani yakisasa,
lakini pia display yake ni LCD haitumii umeme mwingi.

Je utaijuaje?
Nob ya kuongezea sauti ni moja tu na zaidi utakuta button za menu na input inategemeana). Ukiigeuza nyuma ina kiplastic kidogo kilichozungushwa nati, yaani ikiwa italeta shida fundi huku nyuma hafungui mfuniko wote wa nyuma, hufungua ki plastic tu hapo nyuma ndio kimebeba card zoote na subwoofer.

Hasara zake
  1. Ikitokea imeharibu card yake hauwez kubadilisha ,sababu ndani Ina circuit Kama ya phone mafundi weeengi hawana(hatuna) technology yakuitengeneza kwahyo unaenda dukani unanunua Tena kard na si chini ya 40000.
  2. Ila ukifika unaipachika tu huangaiki.
  3. Inahitaji utulie ili uioperate maana inatumia single nob.
  4. Speaker yake ya bass huwekwa ohms ndogo ili idunde sana kwahiyo usipende kuweka sauti kubwa Sana kwa muda mrefu.

Aina ya pili ndio zile old model
Hizo zinaitwa dunda udundavyo ni nzuri kwenye uzuri wake. Yenyewe ukiingalia utakuta Ina nob yaani vile vyakuongezea sauti zaidi ya kimoja. Yaani cha master volume, bass, tweeter na mic, na ukivizungusha vinafika mwisho.

Yenyewe ndani power supply yake ni ya kawaida, inatumia mtransformer wake na diodes za kawaida. kisha umeme huingia kwenye capacitor ndio unaanza kusambazwa ndani. Yaweza kuwa Seapiano, Codjec Aborder au vyovyote. Ukiigeuza nyuma mfuniko wote unafunguka wa nyuma.

Faida yake
  1. ikizingua unaiweza kuirekebisha kiurahisi tu
  2. Zinavumilia sana
  3. Hata muziki upo pia
  4. Rahisi kuitumia
Hasara zake
  1. Display yake ni VFD kama ni seapiano hapa mbele inakioo,inavyoimba Kuna vitu vinacheza cheza kwenye kioo(hii ni kwa baadhi ya subwoofer)
  2. Muonekano wake ni wakizamani ikilinganishwa na hizi mpya

Soma hi pia [emoji1427]
Ndani ya subwoofer panya hupenda kuishi humo, huzaliana na kuleta hitilafu kwa kukata nyaya na kula speaker.
Waya wa speaker una chumvi chumvi hivyo akiingia hauachi.

Simple way jinsi ya kudhibiti
Pale kwenye tobo kuna ki corn cha duara huwa wanakipachika unaweza kukitoa kwa kufuata mpangilio ufuatao:

  1. Chukua maji ya moto kidogo na kitambaa, kichovye kitambaa kwenye maji kisha kikande kuzunguka mduara kwa dakika tano.
  2. Kisha chukua kisu, tumia ncha yake kuingiza pembezoni mwa mduara bila kuikwajua. Huku ukiinua kidogo kidogo kuzunguka corn nzima,ukisha kitoa kitoboe vitundu vidogo kukizunguka upande wa ndani(sio Huku uliko Kanda kwa maji).
  3. Ukisha kitoa chukua waya mgumu usuke upande wa ndani kuzunguka uwazi wa duara wote mule ulimotoboa, kisuke hakikisha unaacha vyumba vidogovidogo kiasi kwamba kinaweza kupita kidore kidogo tu.
  4. Paka gundi upande wa ndani, huku ulikokua unakanda na maji kisha kibandike tena kama kilivyokuwa.

NB: Hii ni kwazile subwoofer kama pichani hapo juu, ambazo hutolea upepo pembeni kwenye kiduara. Wale zinazotolea mbele chini ni habari nyingine.

***
Kiasi chake mtanielewaView attachment 1560194View attachment 1560195

Some updates,
Je, music system yako haina bluetooth na unataka kuongezea? Easy sana na inawezekana pia, kwa mafundi ninaweza kuwaelekeza.

Lakini pia music system yako ulipenda itoe mp5, yaani picture, video inawezekana pia[emoji3][emoji3].
Hususani wale wenye TV za kizamani yaani unachomeka flash disk yako kwenye subwoofer, unapata mdundo alafu kuna cable itatoka kwenye subwoofer hadi kwenye TV yako.

Stay here.
More good things are here.
Welcome.

View attachment 1921368
View attachment 1921369
 
2.1 au 5.1?
By the way nliwah kusema humu kua mziki unaundwa kwa kuunganisha vitu vingi
Hivyo kimoja kati yake kikienda tofauti basi lazima kuna kitu kinapungua!
Mfano amp kubwa ila speaker ndogo,au speaker kubwa amp ndogo,au box design na operation amplifier pia
Hivyo hiyo yakwako iko planned mkuu
2.1 mkuu
 
niulizie sony str dn1060 au str dn1080 naipata kwa ngapi,second hand, sio mupya, baana bei za wale jamaa wa kenya electrohub ni ndefu sana
He can get 1060 at 60k and 1080 at 75k.

He can also get Sony str-dn850 at 48k

Hayo ndo majibu ya mdau aliyeko Nairobi.

Sent from my SM-N916S using JamiiForums mobile app
 
Yes, box set up tu. Floor standing speaker huwa zimebeba zote horn, mid range na woofer. Sema kutokana design na diameter za woofer speaker pale front utaona tu horn, mid ranges speakers. Woofer mara nyingi kwa sababu ya diameter kubwa huwa zinafungwa sided position za box,

Unaweza ona floor standing mbili tu nyembamba na kimuuonekano unaona horn, mid ranges tu. Ila hiyo nusu ya chini ndio kuna woofer speaker. na haionekani kwa mmuonekano wa box upande wa mbele ni either imekuwa installed ubavuni au ndani kwa ndani na ina puliza kelele zake upande wa chini au pembeni mwa box za floor standing speaker na zinafoka kibabe sana.

Ila kuna set up nyingine kama hiyo picha ya tatu, channel 7.2 (subwoofer 3) ina main woofer box moja na 2 main floor standing speakers ambazo na zenyewe zinapika stereo, mid range na base pia. Hata ukiondoa main woofer bado low frequency ya kuridhisha unaipata pia.

Kwenye hili la P.A / home music system wenzetu wapo mbali sana. Kuna mitandao nimepita yaani kukuta kinu kinauzwa $35,000, $70,000, $90,000 ni kawaida sana. Sema tu sijabahatika kusikiliza huo muziki wa kwenye kinu hata cha $35,000 tu. [emoji38][emoji38][emoji38]

download%20(3).jpg
images%20(7).jpg
download%20(5).jpg
images%20(10).jpg

View attachment 2169527
 
Naomba kujua nina sabufa, lakini remote haina ushirikiano na display, nikiijaribu remote kuiangalia kwenye camera ya simu inatoa mionzi lkn ukiibonyeza kwenye sabufa hairespond.

Pole huenda IRD ya subwoofer haipokei
Au inapokea ila processor inazingua
Kama n ird unaweza kurekebisha ila kam n processor ni shida kidogo
 
Yes, box set up tu. Floor standing speaker huwa zimebeba zote horn, mid range na woofer. Sema kutokana design na diameter za woofer speaker pale front utaona tu horn, mid ranges speakers. Woofer mara nyingi kwa sababu ya diameter kubwa huwa zinafungwa sided position za box,

Unaweza ona floor standing mbili tu nyembamba na kimuuonekano unaona horn, mid ranges tu. Ila hiyo nusu ya chini ndio kuna woofer speaker. na haionekani kwa mmuonekano wa box upande wa mbele ni either imekuwa installed ubavuni au ndani kwa ndani na ina puliza kelele zake upande wa chini au pembeni mwa box za floor standing speaker na zinafoka kibabe sana.

Ila kuna set up nyingine kama hiyo picha ya tatu, channel 7.2 (subwoofer 3) ina main woofer box moja na 2 main floor standing speakers ambazo na zenyewe zinapika stereo, mid range na base pia. Hata ukiondoa main woofer bado low frequency ya kuridhisha unaipata pia.

Kwenye hili la P.A / home music system wenzetu wapo mbali sana. Kuna mitandao nimepita yaani kukuta kinu kinauzwa $35,000, $70,000, $90,000 ni kawaida sana. Sema tu sijabahatika kusikiliza huo muziki wa kwenye kinu hata cha $35,000 tu. [emoji38][emoji38][emoji38]

View attachment 2169405View attachment 2169407View attachment 2169414View attachment 2169415
View attachment 2169527

Maelezo mazuri na yaliyojaa mkuu
 
Mkuu yangu hizi Seapiano za digital,sku hizi imeanza tatizo unaweza ukawasha inapga bila bass kabsa ila kuna muda ukiwasha inapga vizuri..wakat mwingne kama haipig bass inabid nizime na kuwasha upya inapga vzur shida Itakuwa nn aisee?

Either cables
I mea wire system haiko sawa kuna mahara panaachia na kushika
Au ni soldering kuna mahara inashika na kuachia

Fanya hivi...ikiwa inaimba bila bass fany km unasukuma bass kuingia ndani hiv uone km itaendelea
 
Back
Top Bottom