Niulize chochote kuhusu Subwoofer na Sounds system

Niulize chochote kuhusu Subwoofer na Sounds system

kelphin

JF-Expert Member
Joined
Dec 24, 2019
Posts
9,872
Reaction score
16,319
Ikiwa inakusumbua,ikiwa unataka kufahamu chochote kinachokutatiza.

Karibu
images.jpg

Nieleze kidogo kuhusu subwoofer
Je, unataka kununua, basi zingatia haya.

Zipo za aina mbili old model na digital. Siyo majina hapana ,yaani inaweza kua rising,seapiano,codjec,aborder au vyovyote Ila itakua digital au old model.

Hizo digital ni Aina ya subwoofer ambayo inamuundo wakisasa ,mala nyingi utakuta Ina (nob) kivingilisho Cha sauti kimoja tu.

Ila kinafanya multipurpose, ukibonyeza hyo hiyo nob unaweza ongeza sauti ,kuongeza bass, na mid.
kifupi mambo yote ni in one button.

Faida yake ni kuwa, aina ya power supply yake Ni ilitaka ifanane na ya home theater(Ila haijawahi[emoji2][emoji2inakua na umeme mnyoofu kidogo.

Zinakua na music mkubwa na mdundo zaidi ni digital,yaani yakisasa,
lakini pia display yake ni LCD haitumii umeme mwingi.

Je utaijuaje?
Nob ya kuongezea sauti ni moja tu na zaidi utakuta button za menu na input inategemeana). Ukiigeuza nyuma ina kiplastic kidogo kilichozungushwa nati, yaani ikiwa italeta shida fundi huku nyuma hafungui mfuniko wote wa nyuma, hufungua ki plastic tu hapo nyuma ndio kimebeba card zoote na subwoofer.

Hasara zake
  1. Ikitokea imeharibu card yake hauwez kubadilisha ,sababu ndani Ina circuit Kama ya phone mafundi weeengi hawana(hatuna) technology yakuitengeneza kwahyo unaenda dukani unanunua Tena kard na si chini ya 40000.
  2. Ila ukifika unaipachika tu huangaiki.
  3. Inahitaji utulie ili uioperate maana inatumia single nob.
  4. Speaker yake ya bass huwekwa ohms ndogo ili idunde sana kwahiyo usipende kuweka sauti kubwa Sana kwa muda mrefu.

Aina ya pili ndio zile old model
Hizo zinaitwa dunda udundavyo ni nzuri kwenye uzuri wake. Yenyewe ukiingalia utakuta Ina nob yaani vile vyakuongezea sauti zaidi ya kimoja. Yaani cha master volume, bass, tweeter na mic, na ukivizungusha vinafika mwisho.

Yenyewe ndani power supply yake ni ya kawaida, inatumia mtransformer wake na diodes za kawaida. kisha umeme huingia kwenye capacitor ndio unaanza kusambazwa ndani. Yaweza kuwa Seapiano, Codjec Aborder au vyovyote. Ukiigeuza nyuma mfuniko wote unafunguka wa nyuma.

Faida yake
  1. ikizingua unaiweza kuirekebisha kiurahisi tu
  2. Zinavumilia sana
  3. Hata muziki upo pia
  4. Rahisi kuitumia
Hasara zake
  1. Display yake ni VFD kama ni seapiano hapa mbele inakioo,inavyoimba Kuna vitu vinacheza cheza kwenye kioo(hii ni kwa baadhi ya subwoofer)
  2. Muonekano wake ni wakizamani ikilinganishwa na hizi mpya

Soma hi pia [emoji1427]
Ndani ya subwoofer panya hupenda kuishi humo, huzaliana na kuleta hitilafu kwa kukata nyaya na kula speaker.
Waya wa speaker una chumvi chumvi hivyo akiingia hauachi.

Simple way jinsi ya kudhibiti
Pale kwenye tobo kuna ki corn cha duara huwa wanakipachika unaweza kukitoa kwa kufuata mpangilio ufuatao:

  1. Chukua maji ya moto kidogo na kitambaa, kichovye kitambaa kwenye maji kisha kikande kuzunguka mduara kwa dakika tano.
  2. Kisha chukua kisu, tumia ncha yake kuingiza pembezoni mwa mduara bila kuikwajua. Huku ukiinua kidogo kidogo kuzunguka corn nzima,ukisha kitoa kitoboe vitundu vidogo kukizunguka upande wa ndani(sio Huku uliko Kanda kwa maji).
  3. Ukisha kitoa chukua waya mgumu usuke upande wa ndani kuzunguka uwazi wa duara wote mule ulimotoboa, kisuke hakikisha unaacha vyumba vidogovidogo kiasi kwamba kinaweza kupita kidore kidogo tu.
  4. Paka gundi upande wa ndani, huku ulikokua unakanda na maji kisha kibandike tena kama kilivyokuwa.

NB: Hii ni kwazile subwoofer kama pichani hapo juu, ambazo hutolea upepo pembeni kwenye kiduara. Wale zinazotolea mbele chini ni habari nyingine.

***
Kiasi chake mtanielewaView attachment 1560194View attachment 1560195

Some updates,
Je, music system yako haina bluetooth na unataka kuongezea? Easy sana na inawezekana pia, kwa mafundi ninaweza kuwaelekeza.

Lakini pia music system yako ulipenda itoe mp5, yaani picture, video inawezekana pia[emoji3][emoji3].
Hususani wale wenye TV za kizamani yaani unachomeka flash disk yako kwenye subwoofer, unapata mdundo alafu kuna cable itatoka kwenye subwoofer hadi kwenye TV yako.

Stay here.
More good things are here.
Welcome.

View attachment 1921368
View attachment 1921369
 
Hio ni woofer kwa ajili ya mid range na ki twita chake bado huwezi pata mingurumo ya aina yake hapo hata ingekuwa 100watts per channel
radio za zamani zile hi-fi ziliwezaje kutoa deepbass? chukua Aiwa moja hivi sasahv huwezi linganisha na mchina yeyote.
Na hapo ni speaker mbili tu tena zenye ukubwa kama bookshelf speaker.😂🙌
 
Ndio maana nikasema hio kodtec 5.1 ya kiwaki. Ile 2.1 ndio nyokow na muamuzi wa mwisho ni sikio lako mzee. Waliosikiliza wanaelewa zaidi nini namaanisha.
Sasa mkuu, japo hiyo kodteq sijaisikiliza, ila ukishasema 5.1 maana yake hapo huzungumzii tena Stereo(Hifi) System, unazungumzia Homethearte. Na ni Homethearte ya mchina.

Na homethearters hazikutengenezwa kwa ajili ya kukupa ile real feel ya Music, hata home theaterte zenye majina makubwa duniani bado hazikupi that real Music( I stand to be corrected).

Kama tunazungumzia real Music system, sidhani kama hapo kwenye kodtec 5.1 kuna serious Music, labda hiyo 2.1
 
radio za zamani zile hi-fi ziliwezaje kutoa deepbass? chukua Aiwa moja hivi sasahv huwezi linganisha na mchina yeyote.
Na hapo ni speaker mbili tu tena zenye ukubwa kama bookshelf speaker.😂🙌
Zile redio zilidizainiwa with high precision in sound production. Best sounding machine katika kila idara ndio ilikuwa lengo kuu. Ukikutana na Sony LBT series, Kenwood, Aiwa, Pioneer, Akai.

Sio siri vinu vilikuwa vinamwaga sound sio kitoto, kila kitu kwenye balance yake. Bass inasikika vizuri, mids zimematch na highs. Unaweza ukawa ndani ukawa unaskia mziki wa kawaida tu ila ukitoka nje sasa unasikia vishindo yani mziki mziki haswa.

Sometimes nawaza nahisi hata Mmarekani kumtwanga mjapani mibomu ya Nuclear alijua mjapan alikuwa mtamu sana wa Technology na alikuwa anatoa kazi safi mno. Alitaka amdhoofishe tu.
 
vinu vipo baba ila vimeboreshwa

macintos, yamaha, Onkyo nk wanatoa pia sterio intergrated amplifier ila sasa zina bei balaa.

yaani bei kama ya hii unapata toyota vtz bongo.

sasa uwe na hiyo halafu uwe na floor standing mbili za maana
 
Hahahahah hela za kununua vits ununue redio ndani labda kama mke huna😂😂😂!

Utakula vichambo hadi utarudisha redio dukani.
 
Hahahahah hela za kununua vits ununue redio ndani labda kama mke huna😂😂😂!

Utakula vichambo hadi utarudisha redio dukani.
Sasa wenzetu unakuta wana Av receiver, kwa ajili ya surround sound na Video. ana powerd amplifier ana equalizer na ana intergrated amplifier kweye setup moja.🙌😂😂
 
Hahahahah hela za kununua vits ununue redio ndani labda kama mke huna😂😂😂!

Utakula vichambo hadi utarudisha redio dukani.
Mbeleni natàka kuwa na theater ya nyumbani kwangu yaani humu nafunga sound proof kabisa. Nikitaka kusikiliza mziki, kucheza game kiwatch movie basi unazama humo humgasi mtu.
 
Hio
Sasa wenzetu unakuta wana Av receiver, kwa ajili ya surround sound na Video. ana powerd amplifier ana equalizer na ana intergrated amplifier kweye setup moja.🙌😂😂
Redio ya design hio alikuwa nayo uncle wangu mmoja ile ilikuwa ni hatari. Hizo deck zimepangwa kwenye kabati lake kabisa.😂😂😂!!!
 
Mbeleni natàka kuwa na theater ya nyumbani kwangu yaani humu nafunga sound proof kabisa. Nikitaka kusikiliza mziki, kucheza game kiwatch movie basi unazama humo humgasi mtu.
Hahahahah unasikiliza kinu ndani kwa ndani 😂😂
 
wabongo wengi hawajui mziki na
ukimwambia mtu mziki mzuri ni gharama na haupatikani ndani ya box moja hawakuelewi.
umeona chuma hicho cha Wicalu,mtafute akusukie dundo
 
Attachments

  • Screenshot_2022-09-03-19-52-08-59_1c337646f29875672b5a61192b9010f9.jpg
    Screenshot_2022-09-03-19-52-08-59_1c337646f29875672b5a61192b9010f9.jpg
    135.9 KB · Views: 30
Back
Top Bottom