Niulize chochote kuhusu Subwoofer na Sounds system

Niulize chochote kuhusu Subwoofer na Sounds system

kelphin

JF-Expert Member
Joined
Dec 24, 2019
Posts
9,872
Reaction score
16,319
Ikiwa inakusumbua,ikiwa unataka kufahamu chochote kinachokutatiza.

Karibu
images.jpg


Nieleze kidogo kuhusu subwoofer
Je, unataka kununua, basi zingatia haya.

Zipo za aina mbili old model na digital. Siyo majina hapana ,yaani inaweza kua rising,seapiano,codjec,aborder au vyovyote Ila itakua digital au old model.

Hizo digital ni Aina ya subwoofer ambayo inamuundo wakisasa ,mala nyingi utakuta Ina (nob) kivingilisho Cha sauti kimoja tu.

Ila kinafanya multipurpose, ukibonyeza hyo hiyo nob unaweza ongeza sauti ,kuongeza bass, na mid.
kifupi mambo yote ni in one button.

Faida yake ni kuwa, aina ya power supply yake Ni ilitaka ifanane na ya home theater(Ila haijawahi[emoji2][emoji2inakua na umeme mnyoofu kidogo.

Zinakua na music mkubwa na mdundo zaidi ni digital,yaani yakisasa,
lakini pia display yake ni LCD haitumii umeme mwingi.

Je utaijuaje?
Nob ya kuongezea sauti ni moja tu na zaidi utakuta button za menu na input inategemeana). Ukiigeuza nyuma ina kiplastic kidogo kilichozungushwa nati, yaani ikiwa italeta shida fundi huku nyuma hafungui mfuniko wote wa nyuma, hufungua ki plastic tu hapo nyuma ndio kimebeba card zoote na subwoofer.

Hasara zake
  1. Ikitokea imeharibu card yake hauwez kubadilisha ,sababu ndani Ina circuit Kama ya phone mafundi weeengi hawana(hatuna) technology yakuitengeneza kwahyo unaenda dukani unanunua Tena kard na si chini ya 40000.
  2. Ila ukifika unaipachika tu huangaiki.
  3. Inahitaji utulie ili uioperate maana inatumia single nob.
  4. Speaker yake ya bass huwekwa ohms ndogo ili idunde sana kwahiyo usipende kuweka sauti kubwa Sana kwa muda mrefu.

Aina ya pili ndio zile old model
Hizo zinaitwa dunda udundavyo ni nzuri kwenye uzuri wake. Yenyewe ukiingalia utakuta Ina nob yaani vile vyakuongezea sauti zaidi ya kimoja. Yaani cha master volume, bass, tweeter na mic, na ukivizungusha vinafika mwisho.

Yenyewe ndani power supply yake ni ya kawaida, inatumia mtransformer wake na diodes za kawaida. kisha umeme huingia kwenye capacitor ndio unaanza kusambazwa ndani. Yaweza kuwa Seapiano, Codjec Aborder au vyovyote. Ukiigeuza nyuma mfuniko wote unafunguka wa nyuma.

Faida yake
  1. ikizingua unaiweza kuirekebisha kiurahisi tu
  2. Zinavumilia sana
  3. Hata muziki upo pia
  4. Rahisi kuitumia
Hasara zake
  1. Display yake ni VFD kama ni seapiano hapa mbele inakioo,inavyoimba Kuna vitu vinacheza cheza kwenye kioo(hii ni kwa baadhi ya subwoofer)
  2. Muonekano wake ni wakizamani ikilinganishwa na hizi mpya

Soma hi pia [emoji1427]
Ndani ya subwoofer panya hupenda kuishi humo, huzaliana na kuleta hitilafu kwa kukata nyaya na kula speaker.
Waya wa speaker una chumvi chumvi hivyo akiingia hauachi.

Simple way jinsi ya kudhibiti
Pale kwenye tobo kuna ki corn cha duara huwa wanakipachika unaweza kukitoa kwa kufuata mpangilio ufuatao:

  1. Chukua maji ya moto kidogo na kitambaa, kichovye kitambaa kwenye maji kisha kikande kuzunguka mduara kwa dakika tano.
  2. Kisha chukua kisu, tumia ncha yake kuingiza pembezoni mwa mduara bila kuikwajua. Huku ukiinua kidogo kidogo kuzunguka corn nzima,ukisha kitoa kitoboe vitundu vidogo kukizunguka upande wa ndani(sio Huku uliko Kanda kwa maji).
  3. Ukisha kitoa chukua waya mgumu usuke upande wa ndani kuzunguka uwazi wa duara wote mule ulimotoboa, kisuke hakikisha unaacha vyumba vidogovidogo kiasi kwamba kinaweza kupita kidore kidogo tu.
  4. Paka gundi upande wa ndani, huku ulikokua unakanda na maji kisha kibandike tena kama kilivyokuwa.

NB: Hii ni kwazile subwoofer kama pichani hapo juu, ambazo hutolea upepo pembeni kwenye kiduara. Wale zinazotolea mbele chini ni habari nyingine.

***
Kiasi chake mtanielewaView attachment 1560194View attachment 1560195

Some updates,
Je, music system yako haina bluetooth na unataka kuongezea? Easy sana na inawezekana pia, kwa mafundi ninaweza kuwaelekeza.

Lakini pia music system yako ulipenda itoe mp5, yaani picture, video inawezekana pia[emoji3][emoji3].
Hususani wale wenye TV za kizamani yaani unachomeka flash disk yako kwenye subwoofer, unapata mdundo alafu kuna cable itatoka kwenye subwoofer hadi kwenye TV yako.

Stay here.
More good things are here.
Welcome.

View attachment 1921368
View attachment 1921369
 
Equlizer?
Preamplifier mkuu. Hii huwa inatumika pamoja na power amplifier. Pre amplifier inakuwa na Volume knob, inakuwa na selector/sources mfano cd, tuner, dvd etc. Nyuma unaweza chomeka cables mbalimbali toka kwenye tv, cd, tuner etc.

Zinakuwa amplified kidogo kabla ya kuruhusiwa kwenda kwenye power amplifier/hii haina sehemu ya kuongeza volume wala kuchagua source.

Kwenye picha hapo, ya juu yenye knob ya sauti ndo preamplifier na hiyo ya hini ndo power amplifier
View attachment 2545279View attachment 2545280
 
Imagine kuna power amplifier ziko stable at 2.7 Ohms
Hi Ni matakwa ya mtengenezaji

Hata wewe ukitaka amplifier sa hivi let's say 20w nitahitaji kujua Ni 20w kwenye impedance ngap kawaida Ni 4ohms ila naweza tengeneza ikatoa hata 20w at 2ohms kamili bila shida yoyote

Ziko power amp za watts hata elf nne na Zina perform vizuri at 2ohms load
 
Preamplifier mkuu. Hii huwa inatumika pamoja na power amplifier. Pre amplifier inakuwa na Volume knob, inakuwa na selector/sources mfano cd, tuner, dvd etc. Nyuma unaweza chomeka cables mbalimbali toka kwenye tv, cd, tuner etc.

Zinakuwa amplified kidogo kabla ya kuruhusiwa kwenda kwenye power amplifier/hii haina sehemu ya kuongeza volume wala kuchagua source.

Kwenye picha hapo, ya juu yenye knob ya sauti ndo preamplifier na hiyo ya hini ndo power amplifier
View attachment 2545279View attachment 2545280

The same mkuu
Mixser,equlizer,active crossover zote ni operation amplifier (op amp) au pre amp
Sema design ndio tofauti ikilingana na matakwa ya mtumiaji
Hicho unachokitaka wewe ni sawa na tukaita mixser sababu ina kusanya signal zote na kutoa kwa njia mbili(stereo) ili ishuke kwenye amp

Nadhan ni namna ya matamshi na maana yake.
 
Hi Ni matakwa ya mtengenezaji

Hata wewe ukitaka amplifier sa hivi let's say 20w nitahitaji kujua Ni 20w kwenye impedance ngap kawaida Ni 4ohms ila naweza tengeneza ikatoa hata 20w at 2ohms kamili bila shida yoyote

Ziko power amp za watts hata elf nne na Zina perform vizuri at 2ohms load

Leo nmefungua sundar speker moja hivi ambayo ni powered
Inaingiza volts 24 za SMPS Ila inapiga mziki hatari

Kila mtu na namna yake yakubuni ic zake
Anachoniudhi wachina hizo ic wanaziweka kwa mtindo wa chawa!
 
Zinapiga
Ziko fresh ila sio best sana kusikiliza sauti kubwa kwa muda mrefu sana

Had leo sijui why wachina waliamua kuzipa 2ohm bass speaker
Ni sahihi hio spika Ina watts sawa na ya ile ya 8ohms

Tofauti Ni impedance

Je kwanini wametumia 2ohms speaker

Jibu Ni kwamba wametumia TPA3116D2 iko bridged for a total output of 100w at 2ohms


Hio ic inaweza toa max 100w at 2ohms kuweka spika ya ohms 4 ama 8 huwezi pata watts nyingi spika itapiga normal


Tafuta graph ya tpa3116D2 uone watts zake at different voltage na load tofauti tofauti
 
wanasema ohms zinapukuwa ndogo sauti inakuwa kubwa ila ubora wa sauti unakuwa mbaya.
yaani mfano speaker ya ohms 2 ikipokea watt 80 sauti inakuwa kubwa zaidi ila haina ubora.

ila speaker inapendekezwa ohms nzuri ni 6 au 8
zaidi 8.
ili sauti kuwa ya ubora mzuri japo ukifingulia hadi mwisho sauti haiwi kubwa sawa na ile ya ohms 2.

je ni kweli?
Technology ipo mbali Sana some class of amplifier zinaweza perform vizuri even at 1ohms
 
View attachment 2522183
Katika maswali niliyoulizwa sana ni je inawezekana kutumia sound system za magari nyumbani?
Wengi wakisikia zile bass za kwenye magari wanatamani kama wangetumia au wangeisikia seating room au getto
Ila je inawezekana?
Kwasababu subwoofer/home theater zilizo nyingi hazifikii ile bass!
Nianze kwa kusema hivi
Mziki una mambo mengi
Unapoona ile sound inakita vile basi jua ni kutokana na muunganiko wa vitu vingi!
Na muunganiko huo ndio system ya mziki
Ubora wa vifaa hivyo ndio ubora wa sound hiyo na usikivu mzuri
Lakini kuna kitu kimoja ambacho ndio kikwazo namba moja ambacho kinasababisha kufanya ugumu kutumia sound system hizo nyumbani
Umeme wa nyumbani ni 220v-240v hivi ila current yake ni kama 13 hiv per single phase
Ila umeme wa kwenye gari ni 12v tu ila current yake ni 40+ampere

Current inayotembea kwenye waya ndio muhimu kwasababu current ndio UMEME WENYEWE!
Chaja ya kisimbuzi cha AzamTV hua ni 12v
Sawa na 12v za betri ya gari
Ila utofauti ni output current ya hivi vitu viwili

Je hizi busta utaziwasha na nini? Ok tuseme uweke transformer ili ipunguze voltage then ugeuze ac hizo kwenda dc hi ni rahisi na inawezekana ila je hiyo transformer yako itakupa 40+ current? Definitely inawezekana kuwa ngumu kidogo
Ndio maana inawezekana kua vigumu kidogo kutumia system hizi kwenye nyumbaniView attachment 2522201
View attachment 2522202
[emoji1369] hiyo ni equlizer + crossover ya ku tume mziki
Can you imagine sound ipite hapo ndio iende kwenye amplifier zako unadhani usikivu wake utakuaje?View attachment 2522206
Finally check spika kama hizi
Zinataka power ya maana ku drive
Zinatak mashine zenye afya na umeme wa uhakika
Unless utakua haujafanya kitu na hutapata unachokitaka
Mziki wa gari majumbani na sehemu pa vinywaji chakula nk nimefunga Sana

Ni rahisi Sana funga mziki wa gari nyumbani au popote penye 220VAC


Current unayosema 40A je umezidisha na 12v ukajua Ni watts ngapi?


Huwezi sema 12v 40A Ni kubwa kuliko 50v 20A


Umeme wa majumbani Ni mwingi Sana na sio Ampere 13 Ni umeme mwingi Sana ndo Mana watu wanafunga dual 18inch bass spika na mids zake Ni wewe tu kwenye gari huwezi hata uwe na inverter kubwa kiasi gani ..altenator haiwezi fua umeme huo thou Kuna after market zinaweza fua Hadi 200A

Turudi kwnye mziki wa gari

Amplifier ya gari inahitaji 12vdc -14.6VDC as input japo amplifier hazitumii volt hizo ,, zinaenda ongezwa ndani kwnye dc to DC converter


Unachohitaji Ni power supply inayotoa 12v na current ya kutosha kwa hio boschmann kwa nyumbani normal 30A is enough power supply zimejaa tele 20,30,50,80A zipo Bei Hadi laki plus
 
Hi Ni matakwa ya mtengenezaji

Hata wewe ukitaka amplifier sa hivi let's say 20w nitahitaji kujua Ni 20w kwenye impedance ngap kawaida Ni 4ohms ila naweza tengeneza ikatoa hata 20w at 2ohms kamili bila shida yoyote

Ziko power amp za watts hata elf nne na Zina perform vizuri at 2ohms load
Unachosema ni kweli, manufacturers do that. Ila unapozungumzia stable at 2 ohm, unazungumzia speakers zikiwa full range?.

Hivi unajua kwamba amplifier/avr nyingi haziwezi kuwa stable for long kwa load ya 2 ohm?.

Speakers zinaweza kuwa rated mfano 100 watts @8 ohms, japo huwa zina swing kulingana na load inayokuwa directed kwenye speaker. Hii inaweza dip mpaka 4 ohms kwa muda mfupi na ikapanda mpaka labda 16 ohms kulingana na load.

Unajua kwamba the low the impedance of the speakers, the harder the amplifier works?. Tuanzie hapo kwanza.

Achana na hizi HTIB (Home Theatre In Box) ambazo unakuta ina vispeaker hata 5 na Subwoofer moja. Hizi vispeaker vyake vingi ni 3ohms .
 
Back
Top Bottom