Niulize chochote kuhusu Taifa la Burundi

Niulize chochote kuhusu Taifa la Burundi

Juzi kuna jamaa anasema laki 1 ya Burundi ni amepewa elfu 30 ya Tanzania yaan hela ya Burundi ina nguvu kuliko ya kwetu?

Google is free usidanganywe kizoba kwa mambo unayoweza kuverify kirahisi. Currency strength isn't everything jielimisheni watanganyika.

Hata
Screenshot_20250130_172234_Google.jpg
 
JF imeruhusu hata ninyi Vilaza muwe mnaandika ili sisi wenye akili TUWAKOSOE. SASA ELEZEA 330 INAINGIAJE MARA 4 KWENYE 1000?😁 ULIDHANI HUMU MMEJAA NYIE TU DIVISION 5.
Huko mbali sana mpe zile kubwa za mls 500 umuulize kama nazo zinaingia 4 kwenye lita 1?
 
usibishane na mtu ambae yuko border. leo kuna mtu kaniambiea hivyo hivyo 10,000 ths ni 30,000 Bif. wabongo mbona mnapenda ubishi??

Ukiwa zwazwa utaamini. Hata mimi niko boarder, wewe umeambiwa mimi nipo Manyovu, Kigoma boarder sijasimuliwa.

Mtu akiwa USA akikwamba $1 ni 50k TSH inawezekana utaamini pia.
 
Ukiwa zwazwa utaamini. Hata mimi niko boarder, wewe umeambiwa mimi nipo Manyovu, Kigoma boarder sijasimuliwa.

Mtu akiwa USA akikwamba $1 ni 50k TSH inawezekana utaamini pia.
Ona sasa ulivyo na akili za kuokoteza. we mbugira leo nilikuwa napanga mikakati ya Huko na mtu nilie kuewa nawasiliana nae yuko huko ndio kanipa taarifa za exchange rate za huko. msitegemee kushikiwa akili kea kila jambo yaani mnaamini sana google
 
Ukiwa zwazwa utaamini. Hata mimi niko boarder, wewe umeambiwa mimi nipo Manyovu, Kigoma boarder sijasimuliwa.

Mtu akiwa USA akikwamba $1 ni 50k TSH inawezekana utaamini pia.
Hili jamaa lobishi sana Linapenda ligi za kipuuzi afu sasa linakisifiaga sijui liko USA
 
Niulize historia, fursa, diplomasia, n. K nitakujibu
Inasemakana Taifa la Burundi ndo nchi masikini zaidi duniani.

Ukitaka uone shida za watu fika Burundi, kule ndo Kuna masikini na shida hasa, watu hawana nguo, viatu, watoto hawasoni, pesa ngumu n. K

Burundi Kuna makabila makuu 3 amba ni Wahutu ambao ndo wengi, Watusi na Watwa

Lugha kubwa Burundi ni Kirundi na Kiswahili huko mjini Bujumbura

Majengo na miundo mbinu Burundi ni duni mno, rami ipo maeneo macheche, magari sio mengi

Sokoni au gulioni watu wanaokula tu, wanalewa pombe za kienyeji, n.k ni umasikini sana

Mji mkuu wa Burundi ni Gitega yaani Kwa Hapa kwetu ni kama Dodoma. Huko ndo kuna ofsi za serikali ila ukiambiwa kuwa hii ndo Dodoma ya Burundi utashangaa yaani ni kama kijijini huko

Bunjumbura ndo mji wenye harakati nyingi, ndo mji wa Biashara Kwa Hapa Tanzania ndo kama Dar es salaam lakini inalingana na Bagamoyo mjini au pale Kibaha.

Hapo starehe zipo, bia kubwa inabeba Lita 1 inaitwa primus, hizo safari lager zenu zinaingia mara 4

Fursa za biashara kule ni mazao, kununua mazao Burundi ni bei nafuu na kuja kuuza huku
Au kupeleka mavazi

Warundi ni watu wema na waoga Kwa Watanzania, ukienda Mtanzania wanakuheshimu mno,
Ila uasi mtaani upo sana, kutekwa mchana sokoni na kuibiwa au kuuwawa ni jambo la kawaida.
Kuna tofauti gani kati ya Wahutu wa Burundi na wale wa Rwanda? Je ni kabila moja? Kama ni kabila moja mbona wanaongea lugha tofauti?
 
1 waliogawa mipaka ni wazungu
Tanganyika koloni la German na Kigoma ikiwa Tanganyika
Rwanda koloni la France
Burundi koloni la German
Kwaiyo hakuna nchi iliyojitengeneza ni wakoloni huko mkutanoni Berlin 1884

Utaratibu wa barabarani kwao ni keep right huku Tanzania ni keep left, kusema la ukweli sijui sababu nini
Utaratibu wa barabara kuendesha upande upi tumerithi kutoka kwa mabwana zetu waliotutawala. Nikiingia Burundi au nikitoka huko huwa napenda sana eneo la interchange mipakani.
 
Inasemekana hawa waha waliojaa hapa Dar wengi wao ni waburundi hili Lina kaukweli wowote?
Ni kweli Hawa wanaouza Madafu wengi ni warundi wanatokea Burundi hata kiswahili ni cha kuunga UNGA sema wanajiita ni watu wa kigoma..


Sijui kwanini serikali haiko macho.
 
Inafahamika kuwa waha wanatoka mkoa wa Kigoma.
1. Ni nini kinawatofautisha waha na warundi au wanyarwanda?
2. Kwa nini mkoa wa Kigoma haukuunda nchi yao kama Rwanda na Burundi licha ya kuwa na eneo lake, lugha na utamaduni?.
3. Kwa nini Burundi wanaendeshea magari yao kulia kwa barabara wakati dereva akiketi na usukani kushoto?
Kigoma hawatoki tu Waha acheni kudanganywa.

Kuna Wabembe hili ni kabila kubwa sana kigoma ulizia.


Kuna wamanyema Hawa ndio wakina ( Mama yake Diamond, juma kaseja, Seleman matola ) ... Wamejaa ujiji. Ni nadra sana kukuta Waha ujiji.


Kuna watongwe n.k
 
Ukiwa zwazwa utaamini. Hata mimi niko boarder, wewe umeambiwa mimi nipo Manyovu, Kigoma boarder sijasimuliwa.

Mtu akiwa USA akikwamba $1 ni 50k TSH inawezekana utaamini pia.
Acha ubishi ndugu yangu Mimi nilikuwa Bujumbura hivi karibuni


100,000 ya Tanzania unapewa 270,000 ya Burundi. Ila bei za vitu Burundi ziko juu hiyo heka Yao inaisha kama upepo.



Taarifa zingine za mitandaoni hazina uhalisia kwenye maisha halisi.
 
Back
Top Bottom