Niulize jambo lolote kuhusu mziki wa Mchiriku/Mnanda

Niulize jambo lolote kuhusu mziki wa Mchiriku/Mnanda

Namichiga

JF-Expert Member
Joined
Jun 1, 2017
Posts
356
Reaction score
526
Wana jamvi,mimi ni mdau mkubwa wa mziki wa mchiriku/mnanda. Mziki ambao ulitawala na kujizolea umaarufu mkubwa kwenye miaka ya 90 hadi 2000,binafsi nimekulia kwenye jamii yenye kuhusudu mziki huo na hivyo kifuani kwangu nina hazina ya kutosha kuhusu mziki huo hatua kwa hatua tangu ulipotokea hadi ulipokuja kuanguka baada Serikali kuingilia kati kutokana na matendo yaliyokua yakifanywa na mashabiki na wapenzi.

Isitoshe nimefanya documentary yangu binafsi kwa kuwatembelea na kuwahoji waliokua/na waliopo kwenye fani hiyo na hivyo kujikusanyia hazina ya kutosha kuhusu mziki huu.

Karibuni wapenzi wa mziki huu tubadilishane mawazo.
 
Huu mziki una uzuri wake kuliko hata hii singeli ya sikuhizi iliyojaa matusi,mnanda una ujumbe pia una vibe,jagwa music walitisha sana na nyimbo zao kama mwana wa kitwana,rest in peace jack simela,mleta mada juma mpongo yupo hai?
 
Juma Mpogo ni marehemu,amefariki muda kidogo.Lakini bado wapo walio hai ambao wanaindeleza bendi ya Seven survivor japo kwa kusuasua.
 
nasikia mlikua kila mkienda kupiga mziki mtaa huo lazima waibiwe
Ni kweli,na jambo hilo ndio lililopelekea hadi serikali kuingilia kati na kuupiga marufuku mziki huu.Japokua ujumbe wake ni mzuri tena uliowagusa watu wa maisha ya chini lakini mashabiki wake walikua ni wahuni mno,ilifikia mahala ukialika mnanda nyumbani kwako na shughuli ikaisha salama basi jua una bahati!.
 
Huo mziki ni kutoka jamii ya wazaramo?
Ki uhalisia huu mziki hauna kabila maalum,in short ni mziki wa watoto wa mjini.Sababu mnanda wakati unashika hatamu enzi ya bendi kama Hisani Gari kubwa,Uraibu,Tokyo ngoma,Kombora Music na nyinginezo,zilikua na watu waliochanganyika kutoka makabira tofauti jijini Dar es salaam.
 
Enzi hizo wakipita mtaani hawa wa mnanda, lazima watoto wapotee walikuwa wanawafuata popote wanapoenda,mwishoni mwa miaka ya 90 manzese darajani,midizini,kwa Bibi nyau, uzuri daah maisha yanaenda kasi
Wakati huo wajanja wa mziki huu wapo Mwananyamala,yaani mziki huu ulivyo una tune zake.Wilaya nzima ya Kinondoni na baadhi ya maeneo ya wilaya Ilala wa tune (mapigo) na bendi zao nyingi ni za Mwananyamala Kama vile,Hisani Gari Kubwa,Jagwa,Tumaini Jabali,Chaukucha na Wanyamwezi.
 
Kuna kundi moja maskani yao ilikua pale mwembe yanga uwanjani lilikua linaitwa Farmer Gusta..lilikua atari sana likiongozwa na marehem Kipaka..[emoji445]tulikua maskani,maskani Farmer Gusta,kukaa kidogo kaja mtu,kaja anatuuliza,kipaka kafa saa ngapi,sio yeye peke yake eee ,yeye ametangulia aaa[emoji445]

Sungu sungu hakulinda baba Asha aa,na ndani hakulala baba Asha aa..[emoji445][emoji445][emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji16]
 
Yaah hao ni Atomic Music chini ya mafundi kama akina Omary Omary,Saidi Ndiga,Mwamkoto Ngoma,Nanga boy Simela(Wema Said Nanga) na wengineo.Hiyo Kipaka nyimbo inaitwa Kipaka Memory,wakati hiyo baba Asha in muendelezo kuanzia baba Asha no.1,2,3 na 4.
 
Ashaaaa niambie ukweli kama hunitaki usinitapeli... ilikua balaaa

kondakta kaja juu akasema haiwezekani kupanda bure imeruhusiwa jeshi la polisi..
mnanda [emoji119][emoji119][emoji119] sema tu hawauelewi

Btw Asha imeimbwa na jack simela au
 
Back
Top Bottom