Niulize jambo lolote kuhusu mziki wa Mchiriku/Mnanda

Niulize jambo lolote kuhusu mziki wa Mchiriku/Mnanda

Wakati huo wajanja wa mziki huu wapo Mwananyamala,yaani mziki huu ulivyo una tune zake.Wilaya nzima ya Kinondoni na baadhi ya maeneo ya wilaya Ilala wa tune (mapigo) na bendi zao nyingi ni za Mwananyamala Kama vile,Hisani Gari Kubwa,Jagwa,Tumaini Jabali,Chaukucha na Wanyamwezi.
chaukucha family, watoto wadogo waliokomaa vichwa 😂 🔥 🔥
 
".......Kama miudaaaa,Kama midaladala yooote anaendesha mdogo wake kachalaaaaa......" huu ulikuwa wimbo gani?..

Enzi hizo tunaishi Temeke Mikoroshini maeneo ya Sandali kuna mahali panaitwa Tops mpaka leo kuna mateja, ndio mitaa unawakuta kina Omary Omary, Charles Tondo, Saidi Ndiga

Nakumbuka Saidi Ndiga alizinguana na anko wangu, basi walileteana mikwara baadae wakaishia kutaniana.

Anyway, hii ndude ilikuwa na vibe fulani hivi mtaani, ile mtu anaimbaaaa halafu ikichanganya unasikia kinanda tuu, hapo masela wanaruka kama wanacheza reggae.

Ujumbe,Vibes, ni muziki wenye mashabiki wengi wahuni ila hakuwa matusi kama miziki ya siku.


Ngoma yangu ya muda wote na hata sasa ninayo kwa simu ni ile, Kivuruge
"......mtazameni kivuruge alivyonyorodoka...., sasa umebaki tuu miguu kama fito.....

Kuna mtu zikinisikiaga nasikiliza zinakuwa hazinielewi kabisaa [emoji23]
hiyo kivuruge kama unayo nipe
 
Hamna mziki naukubali kama mchiriku Nawakubali sana seven survival japo sijui hata nazipataje nyimbo zao.Efm wakati inaanza ilikuwa ni mchiriku mwanzo mwenga japo na wenyewe naona wamefifia kuupromote sasa wanakumbatia masingeli ambayo hayana hata maana
zipo YouTube
 
Hii imenifanya nidukue zaidi kuhusu mchiriku
Kumbe vijana wapya walipeperusha bendera
Tokea enzi za shule na ndomu kwa sana baada ya hapo sikufatilia kabisa mchiriku
Huyu Kijana Mungu amlaze pema peponi
Aliyaweza sana tena

Dah nakubali sana
 
YouTube nao wababaishaji. Yani mpaka leo wameshishindwa kutuwekea ule wimbo wa mchu
Screenshot_20250605-125810_WhatsApp.jpg
ngwa hachagui gereza wa Omary Omary. Au wewe unao mkuu?
Jamaa yupo online mcheki
 
Mimi ni mpz mkubwa wa Jagwa,ila jana usiku E FM walikuwa wanapiga ngoma za Chaukucha family kumbe nao ni wakali aisee,kuna ngoma moja wanasema dogo Jack Simela kuwa anafanya mchezo wa kurudi nyuma,iko pow sana,sijui inaitwaje
huo wimbo unaousema ni huu
Screenshot_20250605-183958_Internet.jpg
 
Ni aina ya mziki ambao unavutia masikioni mwa watu kasikilize hii wametutoka muimbaji juma mpogo
 
Nautafuta wimbo wa wametoka mbali nadhani ni jagwa wameimba na wimbo mwingine unaimbwa "tabia zako na vitendo vyako vmenichosha ewe mke wangu tulia mama wa watoto maisha haya magumu" nadhan unaitwa tulia mama watoto.
 
Back
Top Bottom