Namichiga
JF-Expert Member
- Jun 1, 2017
- 356
- 526
- Thread starter
- #161
Mkama Shapu huyu alikua ni askari polisi aliewahi kufanya kazi mitaa ya Temeke na baadae kituo cha Msimbazi kama sikosei,huyu alikua ni mdau mkubwa wa mziki wa mchiriku kwa wakati huo na bendi ya mwanzo maarufu kuipa saport ni bendi ya Night Star iliyokuwa chini ya Haidari Kesi.Mkama Shapu mdau mkubwa wa mchuliku.. Kile kikundi chake cha Mchiliku kilitwaje?
Hisani ngoma ilikiwa na mwimbaji wake wa kike, Aligongwa na gari asubuhi mitaa ya Faya, Kutokana na ile ajali wakatunga nyimbo uke mwimbo nimeusahau jina.. Unaitwaje? Kama uko nao tuwekee hapa...
Hussein Mwinyi sasa Rais Zanzibar alikuwa mdau mkubwa wa Hisani ngoma (Mchiliku) unakumbuka aliwahi kutungiwa nyimbo? Mbali na ule ya aliyotungiwa Baba yake Mzee Mwinyi kipindi Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania...
Mkuu huu mziki ni full masela.. Old is Nile..
Kuhusu bendi ya Hisani Gari kubwa iliyokuwa na maskani yake pale Mwananyamala Ujiji na ukaribu na familia ya Mwinyi hilo sina uhakika nalo sana, bali ninachokumbuka ni kuwa Hisani wao katika albam yao ya kwanza Hisani Garikubwa Vol.1 iliyotoka 1986 walimtunguia wimbo walioupa jina la #Ally Mwinyi(Nahodha wetu hodari) sababu nyakati hizo ndio katoka kuchukua hatamu za uongozi wa nchi mwaka 85.
Na kuhusu hili la msanii wao wa kike kufariki kwa ajali ya gari pale faya wacha nilifanyie kazi,sababu nina connection ya kutosha ya baadhi ya wasanii wa iliyokua bendi hiyo ambao bado wako hai,mfano aliewahi kuwa mpiga ngoma(Kulwa) ambae kwa sasa natambulika kama Sheshi Jr aliyo