Komeo Lachuma
JF-Expert Member
- Oct 31, 2014
- 7,926
- 17,030
Huu ulikuwa wimbo gani? Wa nani?Bwana kicheko sina ubaya nae
Bwana sidibe sina ubaya naye
Bwana mfaume sina ubaya
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Huu ulikuwa wimbo gani? Wa nani?Bwana kicheko sina ubaya nae
Bwana sidibe sina ubaya naye
Bwana mfaume sina ubaya
Mbona dar nyota nyimbo zinafanana na gari kubwa, Nani alikuwa anaigaHizo ni zama za chakacha,za bendi kama Dar nyota,Night Star ya akina Haidary Kessy na nyinginezo.Hizi hupatikanaji wake umekua ni watabu sana,lakini wacha nikupekulie maabara.
Dar Nyota ya akina Selemani Misasa ndio band ya kwanza kurecord albam ya Mchiriku mwaka 1993,japo zipo band zilizotangulia kuanzishwa kuliko wao kama vile Night Star na Hisani Gari Kubwa (Meli ya sumu). Kuhusu kufana mapigo kati ya Dar Nyota na Hisani hebu jaribu kutafiti tena juu ya hili,kwani kisanturi ya mapigo Dar Nyota wanafafana na Night Star ya akina Mkama shapu,kwani walikuwa wanatumia vifaa vinavyofanana kama vile vinanda vya upepo (kuvuta) na magita.Mbona dar nyota nyimbo zinafanana na gari kubwa, Nani alikuwa anaiga
Halafu mbona wanaimba kama taarabu flani.
Unazo zile nyimbo za Haidary kessy za miaka ile 1992/93?Wadau na wapenzi wote wa mziki wa Mchiriku,kwa yeyote mwenye kutaka nyimbo yoyote aipendayo ya mchiriku (mnanda) kutoka band yoyote ile,basi anicheck kwa no. 0713963812 ili nimtumie what's up.Ahsanteni.
Nyimbo za mchiriku huwa ndefu na zinachukua nafasi kubwa mfano wa taarabu. lakini kuna namna ya kupunguza ukubwa wa mb na kuzi upload tafadhali fanya hivyo ili utupatie burudani.Kwenye jukwaa hili nashindwa kuziwasilisha sababu zinavuka ujazo wa mb zinazokubalika kulingana na miongozo.
Hilo unalolisema natamani nilijue,lakini je haiathiri ubora wa nyimbo?,kwa maana ya kucheza zikiwa na low quality?.Nyimbo za mchiriku huwa ndefu na zinachukua nafasi kubwa mfano wa taarabu. lakini kuna namna ya kupunguza ukubwa wa mb na kuzi upload tafadhali fanya hivyo ili utupatie burudani.
Kaka Mtambo kutoka Ruangwa ametajwa sana na Juma Mpogo kwenye nyimbo inayoitwa #Usije Mjini iliyopo kwenye Seven Survivor Vol.21.Huyu ni mdau na mpenzi tu wa mziki wa mchiriku hususani band ya Seven Survivor (Juma Mpogo).Mtu huyu alipata connection ya kufahamika na wasanii wa Seven kupitia mtu anaeitwa Pylot Ngulamba ambaye yeye ni msanii wa band hiyo pia (Yeye alikuwa Rapper).Kaka mtambo luangwa ndo nani jombi,mana nimemsikia sana kwenye ngoma za mpogo
Mkuu huu uzi nimeuona leo, mimi ni mpenzi sana wa Mchiriku, na haswa hawa jamaa wa Jagwa... nimefurahi, hongera sana. Hivi mfano nataka kuwaona Jagwa waki perform naweza kuwapata wapi?Huo wimbo wenyewe ni Hisani Gari kubwa(Meli ya sumu),binafsi nina hazina ya kutosha kwenye maabara yangu ya Mchiriku/Mnanda/Limba.So kila mtu akitaja yake uzi utajaa manyimbo tu,ww nifuate dm nikutumie wangu.
Daah, mzee unanifurahisha sanaKamongo Manjalino,huni ni miongoni mwa maprofesheno wa Jagwa Music,yeye alikua anagusa kinanda(njia).
Wana jamvi,mimi ni mdau mkubwa wa mziki wa mchiriku/mnanda. Mziki ambao ulitawala na kujizolea umaarufu mkubwa kwenye miaka ya 90 hadi 2000,binafsi nimekulia kwenye jamii yenye kuhusudu mziki huo na hivyo kifuani kwangu nina hazina ya kutosha kuhusu mziki huo hatua kwa hatua tangu ulipotokea hadi ulipokuja kuanguka baada Serikali kuingilia kati kutokana na matendo yaliyokua yakifanywa na mashabiki na wapenzi.
Isitoshe nimefanya documentary yangu binafsi kwa kuwatembelea na kuwahoji waliokua/na waliopo kwenye fani hiyo na hivyo kujikusanyia hazina ya kutosha kuhusu mziki huu.
Karibuni wapenzi wa mziki huu tubadilishane mawazo.
Dah umenikumbusha mbali Sana habari za mkama sharpHii band ya Night Star, muanzilishi alikua ni Koplo Mkama Sharp,huyu alikua ni askari polisi alietikisa na kuogopwa na wakuda miaka hiyo ya 90' akiwa pale kituo cha Msimbazi.Huyu jamaa alikua hakosi kwenye shoo za band ya Mchiriku ya Red Star maeneo ya Ilala.
Baadae ndio akahamasika na kuwang'oa Magwiji wa band hiyo ya Red Star akina Mkama shapu, Halfan wa Mizoga na wengineo na kwenda kuanzisha Night Star iliyokuja kupata umaarufu mkubwa.