Niulize jambo lolote kuhusu mziki wa Mchiriku/Mnanda

Niulize jambo lolote kuhusu mziki wa Mchiriku/Mnanda

Hizo ni zama za chakacha,za bendi kama Dar nyota,Night Star ya akina Haidary Kessy na nyinginezo.Hizi hupatikanaji wake umekua ni watabu sana,lakini wacha nikupekulie maabara.
Mbona dar nyota nyimbo zinafanana na gari kubwa, Nani alikuwa anaiga
Halafu mbona wanaimba kama taarabu flani.
 
Mbona dar nyota nyimbo zinafanana na gari kubwa, Nani alikuwa anaiga
Halafu mbona wanaimba kama taarabu flani.
Dar Nyota ya akina Selemani Misasa ndio band ya kwanza kurecord albam ya Mchiriku mwaka 1993,japo zipo band zilizotangulia kuanzishwa kuliko wao kama vile Night Star na Hisani Gari Kubwa (Meli ya sumu). Kuhusu kufana mapigo kati ya Dar Nyota na Hisani hebu jaribu kutafiti tena juu ya hili,kwani kisanturi ya mapigo Dar Nyota wanafafana na Night Star ya akina Mkama shapu,kwani walikuwa wanatumia vifaa vinavyofanana kama vile vinanda vya upepo (kuvuta) na magita.

Hisani gari Kubwa kimapigo ilifanana sana na Tumaini Jabali (wasanii wengi walikua ni wa Hisani hiyo hiyo)na wahasimu wao band ya Fadhila kutoka Mabibo
 
Wadau na wapenzi wote wa mziki wa Mchiriku,kwa yeyote mwenye kutaka nyimbo yoyote aipendayo ya mchiriku (mnanda) kutoka band yoyote ile,basi anicheck kwa no. 0713963812 ili nimtumie what's up.Ahsanteni.
Unazo zile nyimbo za Haidary kessy za miaka ile 1992/93?
 
Kwenye jukwaa hili nashindwa kuziwasilisha sababu zinavuka ujazo wa mb zinazokubalika kulingana na miongozo.
 
Hii band ya Night Star, muanzilishi alikua ni Koplo Mkama Sharp,huyu alikua ni askari polisi alietikisa na kuogopwa na wakuda miaka hiyo ya 90' akiwa pale kituo cha Msimbazi.Huyu jamaa alikua hakosi kwenye shoo za band ya Mchiriku ya Red Star maeneo ya Ilala.

Baadae ndio akahamasika na kuwang'oa Magwiji wa band hiyo ya Red Star akina Mkama shapu, Halfan wa Mizoga na wengineo na kwenda kuanzisha Night Star iliyokuja kupata umaarufu mkubwa.
 
Huyo ni Mfaume (Thompson), Muimbaji nguli wa band ya Hisani gari kubwa.Kwa sasa ni mgonjwa yupo kwao hapo Mwananyamala.
IMG-20211009-WA0002.jpg
 
Attachments

  • VID-20211009-WA0009.mp4
    4.6 MB
Na huyo ni Haidary Kessy, muimbaji nguli wa band ya Night Star.Kwa sasa yupo kwa mwanae huko Buza.
IMG-20200929-WA0000.jpg
 
Kaka mtambo luangwa ndo nani jombi,mana nimemsikia sana kwenye ngoma za mpogo
 
Kwenye jukwaa hili nashindwa kuziwasilisha sababu zinavuka ujazo wa mb zinazokubalika kulingana na miongozo.
Nyimbo za mchiriku huwa ndefu na zinachukua nafasi kubwa mfano wa taarabu. lakini kuna namna ya kupunguza ukubwa wa mb na kuzi upload tafadhali fanya hivyo ili utupatie burudani.
 
Nyimbo za mchiriku huwa ndefu na zinachukua nafasi kubwa mfano wa taarabu. lakini kuna namna ya kupunguza ukubwa wa mb na kuzi upload tafadhali fanya hivyo ili utupatie burudani.
Hilo unalolisema natamani nilijue,lakini je haiathiri ubora wa nyimbo?,kwa maana ya kucheza zikiwa na low quality?.
 
Kaka mtambo luangwa ndo nani jombi,mana nimemsikia sana kwenye ngoma za mpogo
Kaka Mtambo kutoka Ruangwa ametajwa sana na Juma Mpogo kwenye nyimbo inayoitwa #Usije Mjini iliyopo kwenye Seven Survivor Vol.21.Huyu ni mdau na mpenzi tu wa mziki wa mchiriku hususani band ya Seven Survivor (Juma Mpogo).Mtu huyu alipata connection ya kufahamika na wasanii wa Seven kupitia mtu anaeitwa Pylot Ngulamba ambaye yeye ni msanii wa band hiyo pia (Yeye alikuwa Rapper).

Pylot Ngulamba nje na shughuli zake za usanii alikua ni dereva pia, hivyo juna nyakati alikua anaendesha basi la Wifi Coach lililokua linakwenda huko Ruangwa,na huo ndio ikawa mwanzo wa watu wa Ruangwa kuwa na ukaribu wa kutosha na Seven Survivor na hatimaye kutajwa kwenye nyimbo zao.
 
Huo wimbo wenyewe ni Hisani Gari kubwa(Meli ya sumu),binafsi nina hazina ya kutosha kwenye maabara yangu ya Mchiriku/Mnanda/Limba.So kila mtu akitaja yake uzi utajaa manyimbo tu,ww nifuate dm nikutumie wangu.
Mkuu huu uzi nimeuona leo, mimi ni mpenzi sana wa Mchiriku, na haswa hawa jamaa wa Jagwa... nimefurahi, hongera sana. Hivi mfano nataka kuwaona Jagwa waki perform naweza kuwapata wapi?
 
Wana jamvi,mimi ni mdau mkubwa wa mziki wa mchiriku/mnanda. Mziki ambao ulitawala na kujizolea umaarufu mkubwa kwenye miaka ya 90 hadi 2000,binafsi nimekulia kwenye jamii yenye kuhusudu mziki huo na hivyo kifuani kwangu nina hazina ya kutosha kuhusu mziki huo hatua kwa hatua tangu ulipotokea hadi ulipokuja kuanguka baada Serikali kuingilia kati kutokana na matendo yaliyokua yakifanywa na mashabiki na wapenzi.

Isitoshe nimefanya documentary yangu binafsi kwa kuwatembelea na kuwahoji waliokua/na waliopo kwenye fani hiyo na hivyo kujikusanyia hazina ya kutosha kuhusu mziki huu.

Karibuni wapenzi wa mziki huu tubadilishane mawazo.

Mkuu hebu naomba niambie Oscar Mkoba alikuwa nani? Nona Jagwa walimtungia wimbo kabisa nadhani uko katika Albamu ya Liwalo na Liwe.
 
Hii band ya Night Star, muanzilishi alikua ni Koplo Mkama Sharp,huyu alikua ni askari polisi alietikisa na kuogopwa na wakuda miaka hiyo ya 90' akiwa pale kituo cha Msimbazi.Huyu jamaa alikua hakosi kwenye shoo za band ya Mchiriku ya Red Star maeneo ya Ilala.

Baadae ndio akahamasika na kuwang'oa Magwiji wa band hiyo ya Red Star akina Mkama shapu, Halfan wa Mizoga na wengineo na kwenda kuanzisha Night Star iliyokuja kupata umaarufu mkubwa.
Dah umenikumbusha mbali Sana habari za mkama sharp

Alikuwa kituo Cha pollisi mzimbaz pale jamaa alikuwa n kwikwi kwa hapa dsm

Ukienda taifa uwanjan utamkuta anapanga watu folen ya kuingia ndan hatumii nguvu na watu wanamuogopa

Alikuwa anatembea na bastola zake kiunoni kila upande na zinaonekana

Nyakat nyingine alaikuwa anatembea juu ya faras na watoto tukikuwa tunamfuata nyuma enz hizo

Kubwa Zaid jamaa alikuwa n promota was ngumi miaka hyo nakumbuka Sana maeneo ya DDC alikokuwa anaandaa mapambano yake

RIP MKAMA SHAP

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom