Niulize jambo lolote kuhusu mziki wa Mchiriku/Mnanda

Niulize jambo lolote kuhusu mziki wa Mchiriku/Mnanda

Huo wimbo wenyewe ni Hisani Gari kubwa(Meli ya sumu),binafsi nina hazina ya kutosha kwenye maabara yangu ya Mchiriku/Mnanda/Limba.So kila mtu akitaja yake uzi utajaa manyimbo tu,ww nifuate dm nikutumie wangu.
Broh kujaza uzi sio tatizo. Weka nyimbo tuburudike. Namkubaligi sana Lupozi (R. I. P)
 
Kuna wimbo nausikiliza efm hapa,wanaimba hivi:
Wewe,wenzako wanakutafuna
Wewe,sio kama ushahidi sina
Wewe,mchezo wa kurudi kinyuma nyuma.
Unajiita simela,huku elimu hauna
Hata hilo gazeti,linakushinda kusoma,
Huo usimela gani,huku mapene hauna
Au usimela wako,kurudi kinyuma nyuma.
Nautafuta huu wimbo nadhani wameimba Chaukucha family,sijui unaitwaje.
 
Na kuna wimbo pia wanaimba hivi.

Sisi tunaokwambia,tupo kwenye fani
Sasa mwenzangu na mie upo mashakani
Hao raia mtaani hawana utani
Tena wanaua hawana imani.
Huu nao nadhani wameimba Chaukucha family ila sijui unaitwaje,nauhitaji
 
Enz hizo maeneo ya TAA NYEKUNDU hadi SANDALI njoo farmer gusta hatari tupu

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
Kuna nyingine wanakwambia
Tulikuwa tumekaa maskani
Maskani famagusta
Mara washkaj wanatuambia
Kicheko katutoka
Sie yeye peke yake.
Nyingine ilikuwa
Atakufanyia hila
Na rumande akuweke
Uijutie duniaaaa
Kila shetani na mbuyu wake.
 
Kuna nyingine wanakwambia
Tulikuwa tumekaa maskani
Maskani famagusta
Mara washkaj wanatuambia
Kicheko katutoka
Sie yeye peke yake.
Nyingine ilikuwa
Atakufanyia hila
Na rumande akuweke
Uijutie duniaaaa
Kila shetani na mbuyu wake.
Hiyo nyimbo imeimbwa na bend ya Atomic Music"Sauti ya utawala",inaitwa Kipaka memory.Its a true story about Kipaka's death.
 
Na kuna wimbo pia wanaimba hivi.

Sisi tunaokwambia,tupo kwenye fani
Sasa mwenzangu na mie upo mashakani
Hao raia mtaani hawana utani
Tena wanaua hawana imani.
Huu nao nadhani wameimba Chaukucha family ila sijui unaitwaje,nauhitaji
Mziki wa mnanda nao una vijembe na michambo ya kiaina,kule Mwananyamala (Kinondoni tune)kuna zama vilitawala vijembe hususani kati ya bendi ya Jagwa"Dege la jeshi" na Chaukucha Family(Watoto wadogo waliokomaa vichwa).Navyo vilizidi kuchagiza burudani kwa wapenzi wa mziki huu.
 
Huyo hapo ni mkongwe wa muziki wa mchiriku(zama za chakacha),Haidary Kessy kutoka bendi ya Night Star.
IMG-20200929-WA0000.jpg
 
Huyu ni striker Mhina kutoka Miami Voice Yankees,moja kati ya wakongwe wa mziki wa mchiriku kanda ya Temeke( Temeke tune).
IMG_20210525_105018_427.jpg
 
Huyo hapo ni mtu wa kuitwa Hassan Kindende,moja kati ya mafundi wa kugusa njia lakini wasiopata umaarufu wa kivile kanda yaTemeke.
IMG-20201024-WA0005.jpg
 
Atomic Advantage Music,bend iliyoachwa na super star wa kwanza kupata jina kubwa wilaya ya Temeke Omary Omary(double Ommy) wakikinukisha kitaa.
IMG-20201024-WA0004.jpg
 
mkuu namichiga unaijua story ya boniface machupa aliyeimbiwa na jagwapole jenerali by baba j(r.i.p)
 
mkuu namichiga unaijua story ya boniface machupa aliyeimbiwa na jagwapole jenerali by baba j(r.i.p)
Story kuhusu Boniface Machupa alieimbwa na Legendary wa mziki wa mchiriku kutoka bend ya Jagwa marehemu baba J kiukweli sina,lakini labda unitume(as a mdau)ili nimtrack na kumjua vyakutosha ili nikujuze.Kwa kuwa mkononi nina connection ya kutosha ya wasanii na wadau wa kutosha wa mchiriku kutoka Mwananyamala(Kinondoni tune).
 
poa mkuu, ukipata utujuze pamoja!
 
Mziki wa mnanda nao una vijembe na michambo ya kiaina,kule Mwananyamala (Kinondoni tune)kuna zama vilitawala vijembe hususani kati ya bendi ya Jagwa"Dege la jeshi" na Chaukucha Family(Watoto wadogo waliokomaa vichwa).Navyo vilizidi kuchagiza burudani kwa wapenzi wa mziki huu.
Mkuu ahsante kwa ufafanuzi wako,ila mimi nakutuma naomba nitafutie hizo nyimbo nilizoomba hapo juu,alafu mwanzo hawa Efm walikuwa wanapiga mnanda ijumaa na jmos kuanzia saa tano usiku mpaka saa saba usiku,lakin siku hizi wanapiga kuanzia tano kamili mpaka tano na nusu wamemaliza.wanatunyima uhondo

Sent from my Infinix X5515 using JamiiForums mobile app
 
Mkuu Namichiga , natafuta saaaana wimbo mmoja unaimba "..narudi nyumbani Chalinze".

-Kaveli-
 
"Narudi nyumbani Chalinze" huu wimbo waliimba kundi gani? Nautafuta sana.

-Kaveli-
 
Back
Top Bottom