Niulize jambo lolote kuhusu mziki wa Mchiriku/Mnanda

Niulize jambo lolote kuhusu mziki wa Mchiriku/Mnanda

Nitakufanyia mpango,hizo nyimbo wenyewe ni Atomic Music(Omary Omary)na zipo namba 1-4,na mjumbe alikuwa anaitwa Mzee Nanga.Huyo Nanga yy alikua ni rapper kwenye bendi hiyo na baadae alihama na kuamia Seven Survivor ya Juma Mpogo.
Nanga Boy Simela,Chichi Baunsa,Midoke
 
Wana jamvi,mimi ni mdau mkubwa wa mziki wa mchiriku/mnanda. Mziki ambao ulitawala na kujizolea umaarufu mkubwa kwenye miaka ya 90 hadi 2000,binafsi nimekulia kwenye jamii yenye kuhusudu mziki huo na hivyo kifuani kwangu nina hazina ya kutosha kuhusu mziki huo hatua kwa hatua tangu ulipotokea hadi ulipokuja kuanguka baada Serikali kuingilia kati kutokana na matendo yaliyokua yakifanywa na mashabiki na wapenzi.

Isitoshe nimefanya documentary yangu binafsi kwa kuwatembelea na kuwahoji waliokua/na waliopo kwenye fani hiyo na hivyo kujikusanyia hazina ya kutosha kuhusu mziki huu.

Karibuni wapenzi wa mziki huu tubadilishane mawazo.
Topaz walifia wapi?
 
Watu bado wapo ila saport ilikua chini tu,kuna watu kama akina Mwina,Mudy Jongo, Division Hadji,Amani Stereo,Mudy black,Mudy wa Shamba,Amadi Kiedu,Ally Chande "Dog",akina Machupa kule Bagamoyo na watu lundo tu.Lakini tushukuru E-Fm wameanza kuusaport.
Naona umewataja wakali wote wa Seven Survivor wakina Mudy Jongo,Aman Stereo, Division Haji,Mudy Black,Mudy wa Shamba, Amad Kiedu na Ally Chande. Bado wanalisongesha pale alipoachia Jenerali Lupozi
 
hahahaahahahh hapo Farmer Gusta enzi hizoo palikua na kibustani cha michongoma kabisaa pale ambapo leo hii pana jumba la kutupia taka
wanikumbusha watoto wa Mzee Mangusiroo, kina Kabwe na nduguye Kipaka,
enzi za Double Ommy na Atomic music
mikoroshini ilikua motooooo
Hivi Kabwe bado yupo hai?
 
Ilikuwa vibes la ukweli kuanzia pande za Puma hadi Famagusta.
 
Hapo Tops kulikua na wahuni wakutosha na ndio ilisababisha zile maskani ( garden ) kupigwa marufuku maana ilikua ganja ganjani unga ngada kwa kwenda mbele.kulikua na vile vikundi vya komando yosso kama wale panya road.Usisahau wale wahuni wa pale mwembeyanga Farmer Gusta
Halafu kipindi hicho kila kijiwe/maskani inajiona Wajanja zaidi kuliko maskani nyingine,kuanzia Famagusta, Tops,Puma, Ajax, Target, Manova, Place,Kiembe.
 
Kwanini kwenye ngoma ya mnanda wanapendelea kuvaa sharti na busta nyeupe na Sisi na viatu vyeupe??
Wadau kwanza naomba mniwie radhi kwa kutotoa saport kwenye uzi huu kutokana na sababu zilizo nje ya uwezo wangu,lakini yote kwa yote nimerudi na nitajibu kila swali.

Katika mziki wa mnanda ( mchiriku) hakuna vazi rasmi la kuainisha mziku huu,yaani kuanzia wanamuziki wenyewe,wapenzi hadi mashabiki.Ila basi,kwa vile mziki huu asili yake ni tabaka la watu wa maisha ya chini(hali za kawaida kimaisha) basi wadau wote wa mziki huu wamejenga mfumo wa kujitambulisha kwamba wao pia hawako nyuma katika mifumo ya kimaisha hususani fashion au mitindo ya kimavazi,hali hiyo imepelekea kubuni mitindo ya mavazi yenye kuwatambulisha kwamba wao ni wabishi wa kitaa ili kulinda ngome yao!!.

Vazi kuu ni raba mtoni kutoka makampuni makubwa kama vile Asics Gel,New Ballance, Reebok,Nike Air,Adidas,Puma,na viatu vigumu (stone boots) tena zikiwa namba ndefu.Pia kwenye nguo basi Jeans huchukua nafasi kubwa na mavazi ya juu ni mchanganyiko.

Hii yote ni kujaribu kuilinda ngome yao kwamba wewe ikiwa umezaliwa kwenye kada fulani ya kimaisha basi maisha ya mfumo huo huyawezi
 
Kabila Moja na Majaliwa.
Yawezekena ikawa kweli lakini yapo mashaka,Majaliwa kwa maana ya waziri mkuu ni Mmwera kutoka wilaya ya Ruangwa,lakini mpogo ni mtu wa kitoka Kijiji cha Kivinja wilaya ya Kibiti mkoa wa pwani(Wandengereko),na sababu ya seven kupata connection na kufahamika na watu wa Ruangwa ni Pylot Nguramba ambae yeye ni dereva wa mabasi ya huko hususani WiFi coach.Hivyo hilo la Juma Mpogo kuwa Mmwera inawezekana lakini
 
Juma Mpogo japokuwa kafariki ila mpaka sasa hakuna wakumfikia.
Usemacho ni kweli,lakini kwa vile halikuwahi kufanyika pambano la kitaifa la mziki wa mnanda basi itoshe kusema mnanda hauna bingwa!.

Kwanini?,kwanza kwenye mziki wa mnanda kuna kitu kikuu kinaitwa #Tune(mapigo au miondoko),kuna mziki wa Kinondoni,bendi kama Hisan Gari kubwa,Tumaini Jabali,Fadhira,Jagwa,Chaukucha,na hata Wanyamwezi familly,wao wana mapigo yao na mashabiki wao kindakindaki.

Na kuna mziki wa Temeke,bendi kama Seven Survivor,Atomic,Topaz,Kombora,Buti Kubwa,Miami Yankees,Kijumuia New kiwembe na hata Uraibu.Hivyo basi kila mpenzi wa muziki huu ana mapenzi binafsi kutoka kwenye band husika.

Hivyo hatuwezi kuitimisha kwamba fulani alikua bora kuliko mwengine ilihali halikuwahi kufanyika shindano na kila mmoja ana band yake .
 
Juma Mpogo japokuwa kafariki ila mpaka sasa hakuna wakumfikia.
Usemacho ni kweli,lakini kwa vile halikuwahi kufanyika pambano la kitaifa la mziki wa mnanda basi itoshe kusema mnanda hauna bingwa!.

Kwanini?,kwanza kwenye mziki wa mnanda kuna kitu kikuu kinaitwa #Tune(mapigo au miondoko),kuna mziki wa Kinondoni,bendi kama Hisan Gari kubwa,Tumaini Jabali,Fadhira,Jagwa,Chaukucha,na hata Wanyamwezi familly,wao wana mapigo yao na mashabiki wao kindakindaki.

Na kuna mziki wa Temeke,bendi kama Seven Survivor,Atomic,Topaz,Kombora,Buti Kubwa,Miami Yankees,Kijumuia New kiwembe na hata Uraibu.Hivyo basi kila mpenzi wa muziki huu ana mapenzi binafsi kutoka kwenye band husika.

Hivyo hatuwezi kuitimisha kwamba fulani alikua bora kuliko mwengine ilihali halikuwahi kufanyika shindano na kila mmoja ana band yake
 
Back
Top Bottom