Iko hivi Mwandende,mziki wa mnanda hapo mwanzo kabisa ulikua unatambulika kama chakacha.Katika awamu hiyo ya chakacha mziki huu ulikua na mandhari ya ubasha na ushoga,na hata upigaji wao ulikua wa santuri ya miondoko raini na vifaa kama magitaa viliusika na madensa wake au wachezaji waliitwa mafaruku.Hapo unaweza kuziona bendi maarufu kama vile Dar Nyota na Night Star ya akina Haidary Kessy.
Lakini baadae mziki huu ulipiga hatua na kupokelewa na watoto wa uswahili,ambao wao kwanza hawakua na vifaa vya kisasa na lakini pia walitaka mziki wenye mandhari ya kuchezeka kisela na kuruka kiuswahili na si kusikiliza na kunengua mauno.Ndipo hapo mziki huu inaingia hatua ya pili kwani unabadilika mandhari na upigaji na kuitwa Mchiriku,hapa bendi maarufu iliyotamba sana ni Hisani Gari Kubwa(Meli ya sumu)wahuni kutoka Mwananyamala kwa Manjunju.
Lakini kadri muda ulivyosonga ndipo makundi zaidi yakawa yanaibuka na ubunifu ukawa unaongezeka na upigaji pia,hapa ndio mziki unaingia hatua nyingine na kuingia kwenye mnanda.Hapa kwenye kumbukumbu ya bendi nyingi sana kama Jagwa,Wanyamwezi,Chaukucha,Topaz,Kombora,Atomic,Tokyo ngoma,Miami Yankees,New Kiwembe,Seven Survivor,Buti Kubwa,Uraibu na nyingine nyingi.
Nafikiri kwa maelezo hayo utakua umeshapata picha ni wapi mziki huu ulipotoka hadi kuwa mziki kipenzi kwa makundi ya vijana na jamii nzima katika miaka hiyo ya 90 na 2000.