Niulize jambo lolote kuhusu mziki wa Mchiriku/Mnanda

Niulize jambo lolote kuhusu mziki wa Mchiriku/Mnanda

Ashaaaa niambie ukweli kama hunitaki usinitapeli... ilikua balaaa

kondakta kaja juu akasema haiwezekani kupanda bure imeruhusiwa jeshi la polisi..
mnanda [emoji119][emoji119][emoji119] sema tu hawauelewi

Btw Asha imeimbwa na jack simela au
Asha nambie kweli ni wimbo wa Jagwa Music chini Simba baba J ambaye alikuja kufia jela,wakati huo dogo Jack hajulikani bado yupo kwao Mwembesongo kule Moro towm.Na hiyo nyingine inaitwa "Kondakta" (Marumbano na zogo kubwa katika basi lile,kati Kondakta na bwana mgambo yule),nyimbo hii wenyewe ni bendi inayoitwa CHAUKUCHA FAMILY(watoto wadogo waliokomaa vichwa) kutoka Mwananyamala kwa Kopa.Humo kuna watu kama akina Aigosh ambao ni maprofesheno waliojitoa Jagwa baada ya kurumbana.
 
Ebwana mwenye nyimbo yoyote ya eleven stars
Hizo ni zama za chakacha,za bendi kama Dar nyota,Night Star ya akina Haidary Kessy na nyinginezo.Hizi hupatikanaji wake umekua ni watabu sana,lakini wacha nikupekulie maabara.
 
Asha nambie kweli ni wimbo wa Jagwa Music chini Simba baba J ambaye alikuja kufia jela,wakati huo dogo Jack hajulikani bado yupo kwao Mwembesongo kule Moro towm.Na hiyo nyingine inaitwa "Kondakta" (Marumbano na zogo kubwa katika basi lile,kati Kondakta na bwana mgambo yule),nyimbo hii wenyewe ni bendi inayoitwa CHAUKUCHA FAMILY(watoto wadogo waliokomaa vichwa) kutoka Mwananyamala kwa Kopa.Humo kuna watu kama akina Aigosh ambao ni maprofesheno waliojitoa Jagwa baada ya kurumbana.
mkuu kumbe baba j kafia jela.. ilikuwaje mkuu?
 
hatari mkuu..kuna mtu pia alikuwa anaitwa ali tasha aka tasha boy
Yaah,nyakati hizo ndio Jagwa wamepamba moto kuurudisha mziki wao wa mnanda ambao tayari ulishatekwa na watoto wa Temeke kama akina,Omary Omary(Atomic),Chuna(Kombora)IssaKiyange(Buti kubwa/Uraibu),Mwina(Miami Beach)na Matajiri watoto (Seven Survivor).
 
Najua unetumwa na baba mwenye nyumba haya kutufanyia , bendi gani wameimba hivo na wimbo unaitwaje mdau
 
nani mkali kati ya omary omary, baba j na generali juma mpogo???
Mziki una ushabiki kama unavyoona timu za mpira,hao uliowataja wote ni mafundi na kila mmoja ana radha na mashabiki wake hivyo kwenye kuamua nani mkali kila mtu ana sababu zake.Kwa upande wangu mm Juma Mpogo au General Lupozi anajua ingawa wote nawapenda.
 
ni kweli mkuu..ila wote ni marehemu kwa sasa na wameondoka na mchiriku ndio kwisha habari yake!
 
Back
Top Bottom