".......Kama miudaaaa,Kama midaladala yooote anaendesha mdogo wake kachalaaaaa......" huu ulikuwa wimbo gani?..
Enzi hizo tunaishi Temeke Mikoroshini maeneo ya Sandali kuna mahali panaitwa Tops mpaka leo kuna mateja, ndio mitaa unawakuta kina Omary Omary, Charles Tondo, Saidi Ndiga
Nakumbuka Saidi Ndiga alizinguana na anko wangu, basi walileteana mikwara baadae wakaishia kutaniana.
Anyway, hii ndude ilikuwa na vibe fulani hivi mtaani, ile mtu anaimbaaaa halafu ikichanganya unasikia kinanda tuu, hapo masela wanaruka kama wanacheza reggae.
Ujumbe,Vibes, ni muziki wenye mashabiki wengi wahuni ila hakuwa matusi kama miziki ya siku.
Ngoma yangu ya muda wote na hata sasa ninayo kwa simu ni ile, Kivuruge
"......mtazameni kivuruge alivyonyorodoka...., sasa umebaki tuu miguu kama fito.....