Niulize kuhusu fursa ya masomo Sweden

Niulize kuhusu fursa ya masomo Sweden

Wakuu, imekuwa ni adimu sana kuona Wabongo tukishikana mikono ili kuvuka hatua moja kwenda nyingine yenye mafanikio. Tumezoea kupambana wenyewe na wengi wetu huwa hatupo wazi inapokuja suala la kumueleza mtu mwingine juu ya fursa fulani, tunapenda kuwa wabinafsi na wachoyo.

Kauli hii nimeithibitisha baada ya kutembelea nchi za wenzetu walioendelea (Ulaya) na kuona namna ambavyo Waafrika kutoka magharibi wanavyochangamkia fursa za hapa na pale na namna wanavyoshikana mikono ili kuvuka mahala.

Ni kwa mantiki hiyo basi, ili kuvunja kasumba ya ubinafsi wetu Wabongo, nipo hapa kujibu maswali juu ya fursa ya kimasomo unayoweza kuipata Sweden kwa ngazi ya Shahada ya Uzamili (Masters Scholarship).

Sio masuala ya kuja inbox, wewe uliza hapa hapa public nitakujibu. Sihitaji mtu kuja kunifuata inbox.

Karibuni.

Shukrani mkuu,,,mimi nimepiga BSc.Ed (Mathematics) hivi naweza pata scholarship ya MSc Biostatistics huko maana kozi za statistics nimezipiga kama mbili hivi boss
 
Mkuu nina elimu ya diploma ila napenda kuendelea na degree huko kama hutojali naomba abc nijue utaratibu ukojee wa Scholarship za degree,Nashukuru sana
 
Ninahitaji kuja huko kusoma Masters Degree katika masuala ya biashara/uwekezaji/Projects nitapataje hizo scholarship?
 
Wakuu; huu uzi siyo mrefu na hauna wachangiaji wengi. Hivyo ni rahisi kufatilia mjadala kuanzia mwanzo mpaka mwisho.

Naona maswali mengi mapya majibu yake nimeshayatolea ufafanuzi kwenye uzi huu.

Karibuni kwa mwenye swali jipya ambalo sijalitolea ufafanuzi.

Hakikisha unapitia kwanza uzi mzima kabla ya kuuliza swali. Hakuna nanma ya kukwepa kusoma maana shule ya vyuo vikuu unapewa academic papers kuanzia 5-10 kwa wiki na unatakiwa uzisome zote uzielewe. Kwahiyo kusoma vitu ni njia ya kujenga mazoea ya kusoma ili badae usisumbuke sana.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nina uzoefu kuhusu Scholarship za Masters. Sina uzoefu mkubwa wa PhD Scholarship, hata hivyo, naweza kuelezea kidogo nachofahamu. PhD kwa Sweden ukipata fursa ya Scholarship unakuwa regarded kama mwajiriwa.

Yaani unapewa ajira ya muda mfupi kwa kufanya researches na wakati mwingine unaweza kuhusika kufundisha hapa na pale. Unlipwa kabisa mashara kama mwajiriwa mwingine kulingana na matakwa.

Zipo na unaweza kupata. Nimeona baadhi ya wanafunzi wa PhD wakiendelea na masomo yao katika chuo kimojawapo. Kwa maelezo zaidi, tembelea link hii>>>> PhD programmes in Sweden
Mdogo wangu amesoma degree ya community development in social management, je kwa kozi hiyo scholarship zake zipo?
 
Mdogo wangu amesoma degree ya community development in social management, je kwa kozi hiyo scholarship zake zipo?
Ndiyo anaweza kupata. Bila shaka unamanisha Scholarship kwa ajili ya Master program!
 
Ndiyo anaweza kupata. Bila shaka unamanisha Scholarship kwa ajili ya Master program!
Ndiyo, namaanisha scholarship lakini pia ni kozi ipi ambayo akiisoma huko masters yake hata akirudi hapa au sehemu yoyote anaweza kuajirika au kujiajiri mwenyewe kirahisi na inalipa zaidi.
 
VIP mkuu Nina diploma ya HR naweza pata scholarship ya kusoma IT au computer science huko ila kwa 4m4 nilizingu esabu
 
Mambo vipi mkuu, vipi naweza pata scholarship kwaajili ya admissions ya mwaka 23/24 katika education especially in science subjects...

Kama zipo je, mda wake wa kuziomba ni upi...nipe mrejesho mkuu
 
Back
Top Bottom