Mkuu wewe umenielewa vyema, na hao ndio wataalam wa miamba ambao tunawatumia,hawajasoma lakini akiingia shimoni kutafuta mwamba ni lazima aupate, ila kuna tatizo la mwamba kuhamahama njia, hapo ndipo ninapoona umuhimu wa mtu aliyekwenda shule.
Hii industry mtu aliye nje ngumu sana kuelewa na ikikukubali pesa yake ni tamu sana ila ikiamuwa kukupasuwa kichwa kuna sehemu mnapata mawe lakini hayana soko.
Ndio maana utaona wtu wanakwenda mpaka Mozambique wengine Congo ili kupata mawe ambayo ni hot cake, au mtu mwingine anaamuwa kudeal na dhahabu tu.