Niulize swali lolote kuhusu Geology na field zote zinazohusuhiana na Jiolojia

Sasa ulimuuliza umjibu kwa lugha ipi ili iweje?
 
Mkuu hizi mambo unazifanya bado?, na ni wapi haswa unapofanya (field)
Mkuu nipo Bado kwenye hii field ila kimachalemachale, ziko site mpwapwa, kilosa na Lindi.

Isitoshe bado nina code nets za surface area kadhaa ambazo unaweza kuomba Primary licences za utafiti.

Lakini nakwenda kwa hesabu familia inanitegemea ni hatari sana kuinvest nguvu zako zote kwenye mawe, bora biashara nyingine.
 
Wewe una-google halafu unadanganya kwamba hujafundishwa kwa kiswahili!
 
Swali langu ni je unaweza ukaniambia kuhusu kama ninataka kuianza hii biashara ya mawe, niwe na nunua na kuuza je ni taratibu zipi nianze za kihalali au kisheria,

Nenda pale stamico ukakata leseni then ndio uwaze kazi za kununua
 
Una wataalamu wako maalum, au kuna chance pia kwa sie wengine tunaozitaka
 
sijui na hili linakuhusu lkn kama unajua nijibu.
mawe yanaform vipi..?
Miamba inakuwa formed kutokana na hali mbali mbali zinazotokea Kwenye chanzo cha Miamba yote ambayo ni magma.. Na hapo ndipo tunapata aina kuu Tatu za Miamba...
1.Miamba moto-Hii hutokea pale magma kutoka katikati mwa dunia(earth) inapopoa nje ya uso wa dunia au ndani..
2.Miamba tabaka - Hii hutokea pale Miamba moto au Miamba geu(nitaeleza chini) inapomong'onyolewa kwa nguvu mbali mbali na kusafirishwa na kukusanywa Kwenye mabonde, na Muda unavyokwenda joto na mgandamizo huongezeka na kufanya Miamba tabaka.. Na sifa yake kuu ni kuwa inatengenezeka kwa matabaka, la Kwanza kukusanywa linakuwa la zamani kiumri kuliko la mwisho kujikusanya(deposit).
Miamba geu-Kama jina linavyojieleza ni Miamba ambayo mwanzo ilikuwa katika Hali hizo mbili za juu, yaaani "Miamba moto na Miamba tabaka" ila Hali ikatokea ya mabadiliko ya mgandamizo na joto ndipo Hali yake hugeuka na kutengeneza Miamba geu..
Natumai umepata picha kidogo.
 
Una wataalamu wako maalum, au kuna chance pia kwa sie wengine tunaozitaka
Fursa zipo mkuu, kwenye utafutaji huwa hatunyimani chance, inategemea kwenye project ungependa uingie kama nani? Mtaalam au co- partner?

Na nini unachokijuwa katika industry hii? Una order ya mzigo fulani au vipi? Hizo ndio general know how za industry hii kwa sisi wajasiriamali wazawa na wadogo.
 
Nilikua sijui kiswahili cha igneous na metamorphic rocks, mkuu upo vizuri ktk kiswahili..
[emoji1] [emoji1] [emoji2] [emoji2]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…