griffin griffith
JF-Expert Member
- Mar 22, 2017
- 549
- 442
Mkuu
Nakusubiri
Nakusubiri
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Tunakutana sa ngapiHello guys.....
Hopes U mzima!!
Hakika nilizikuta roli kama 4...zinazoelekea huko Capetown.
Mimi nikalipoint roli flan na nikapatana nae yule dereva.
Mishale ya saa 4-5 jioni, roli lilianza kuingia ndani ya highway tayari kwa kuiyanza safari.
Nakumbuka tulikuwa wa 4 ndani ya lile roli akiwemo na dereva.
Safari ilisonga, taratibu tukaanza kukatiza vitongoji mbalimbali.
Kwakweli sikuwa mtulivu wa nafsi
kwasababu nilikuwa na hofu dhidi ya passport yangu kwani ilisha expired
Pia nikawa na wasiwasi dhidi ya wale niliokuwa nao ndani ya lile roli yakwamba huwenda wakanizuru njiani,
Kwasababu wote wa3 walikuwa ni wazawa ispokuwa mimi tu...
Na lugha iliyokuwa inatumika ndani ya lile roli ni lugha yao binafsi na si English
Sasa nikawa najiuliza kimoyomoyo...
iv ni nini kimenileta huku kwenye nchi ya watu???
Mawazo yalizidi kuongezeka haswa nikifikilia huko niendako.
Nikawa nazidi kujiuliza...wapi nitafikia, nitafikia kwa nani, eneo gani, saangapi tutawasili huko' mchana au usiku,
na vipi iwapo askari akilisimamisha hili roli na kukagua passport zetu..he itakuwaje???
Basi ilinibidi nikae kinyonge ndani ya lile roli kama mbuzi wa sikukuu.
Roli lilizidi kutii amri ya dereva na hata kiza kikatanda hatimae usiku bin night ukaingia.....
Kutokana na safari kuwa ndefu dereva na wazawa wenzake walikata maongezi
na hapo gia tu.
Wale abilia wenzangu wa2 waliupiga usingizi, ila kwa upande wangu haikuwa rahisi kulala kwa kujiami, lkn pia kuishangaa nchi kwa ujumla.
Kwakweli safari haikuwa ya kitoto, kwani nilimshuhudia dereva amekamata chupa kubwa ya maji na kujimwagia usoni kila dakika kadhaa bila shaka ilikuwa ni uchovu na usingizi
pia.
Muda wote huo mi niko kimya2..
Safari ilinoga na hatimae asubuhi kulipambazuka, mnamo saa 12-1 PM
Tulifika sehemu flani iv' kusema kweli sipakumbuki wala sipajui palikuwa ni mji gani pale...ambapo..dereva alipaki roli kwenye some mini supermarket,
Na kututaka tushuke kwa muda, nafikili ni sehemu zao madereva za kupumzikia mahala hapo.
Basi...sisi sote tukashuka, muda mchache baadae nikamuona yule dereva wetu...anawaelekeza jambo wale abilia wenzangu, sikuweza kuelewa chochote kwakuwa lugha ngongano.
Sasa nikawa najiuliza....
inamaana ndio tumeshafika Capetown, mbona sioni movement yoyote???
Kwambali nilianza kufikilia kuludi kuleeee Johannesburg ambako nimetoka.
Lakini ghafla nikawaona wale wenzangu wa2 na dereva wanaelekea ndani ya nyumba flani, nami ilibidi niwafuate ili nijue kinachoendelea.
Mule ndani kumbe ndio mini supermarket yenyewe.
Kuona vile, pole pole matumaini ya kuendelea mbele yalianza kuludi taratibu ingawa bado nina wasiwasi juu ya huko niendako.
Punde si punde, tulitoka nje ya ile supermarket...nakumbuka nilinunua biskuti kama 4 iv' na maji.
Baada ya kutoka...nikawaona wale abilia wenzangu, wanachukua mabegi yao wanaondoka.
Nikajalibu kuwauliza kwa bloken English....eh" nyie bha ndugu munakenda wapi tena mbona atuagany?????
Bahati nzuri wale abilia wenzangu walikuwa wazee kiaina na sio vijana,
hivyo haikuwa ngumu sana kuniambia ukweli yakwamba....
Dereva anakwenda kupumzika [ kulala ]
mpaka baadae ndio ataendelea na safari, kwahio sisi tunaharaka na tunakwenda kuchukua usafiri mwingine ili tuwahi kufika.
Kisha wakaniuliza...
kwani wewe unakwenda wapi?
Moyoni nikasema....
hapo ndipo napataka!!!.
Nikawajibu.....
Mimi sijui nakwenda wapi!
nikaishia hapohapo.
Wale wazee wakaangaliana kisha wakaniuliza kwa mshangao...etiii??
Hujui unakokwenda....salsa huku unakwenda kufanya mini?!
Nikawajibu......
Jamani mimi sijui nakwenda wapi kwa maana kwenye hii nchi sina ndugu, jamaa wala rafiki ispokuwa mimi nimekuja hapa nchini kutafuta maisha.
Hapo kidogo walionyesha sura ya hasila niliposema....[nimekuja kutafuta maisha]
Nilipoona wamechukia,MBONGO nikajiongeza fasta na kuwaambia...
Hata hivyo mimi nafanya kazi kama punda, kwahio km kuna kazi yoyote huko nyumbani nibebeni tu, pia kama munataka ulinzi wa mabinti zenu wasisumbuliwe mimi hiyo kazi naiweza.
Wale wazee walicheka....kisha wakaniambia...wee punda ebu twende gari ilepale inakuja.
Basi... tuliisogelea ile gari, ilikuwa ni private car, iliposimama tukaingia ndani ya ile gari na safari iliendelea.
Ndani ya ile gari, wale wazee waliniambia ya kwamba hawana uwezo wowote wa kunisaidia ispokuwa watanielekeza usafili wa kunifikisha Capetown ambako huko ndiko nitawapata watanzania wenzangu na kudai kuwa watanisaidi.
Sikuwa mbishi ktk lile kwakuwa ni moja
kati ya msaada ninaouhitaji.
Masaa kadhaa baadae tulifika kituo kimoja iv' cha treni, sikikumbuki kinaitwaje au panaitwaje pale, ila tulizikuta treni nyingi...
Wale wazee walinisaidia kukata tiketi ya treni inayoelekea Capetown,
Kisha tukaagana uku wakinitania....
Punda kwaheri......
Wao walipanda treni yao, halkadhalika na mimi nikapanda ya kwangu safari kuelekea jijini Capetown.
Kwa mara ya kwanza ninaipanda treni South Africa tangu nizaliwe.
Ilinibidi niuchune tu mule ndani ya treni japo nilitamani nikodoe mimacho dirishani kuushangaa mji ulivyo mzuri,
Ama kwa Hakika mzuri mno!
Acheni South iitwe ULAYA tu jamani loh...
Mishale ya saa 6:15-20 PM,
ninawasili kitovu cha Capetown centre.
Nakumbuka ilikuwa ni siku ya jumapili.
Nimeshuka na kutoka nje ya ile terminal,
Nilitafuta sehemu ya kukaa kidogo ili nitafakali cha kufanya.
Nilikaa kama dakika 3-4 nikapata jibu ya kwamba nianze kumtafuta mtanzania yeyote ili anisaidie.
Nikaanza kukata mitaa polepole kumtafuta mtanzania popote alipo.
Kadri ninavyozunguka ile mitaa,,
nikaanza kupata mawenge *kizunguzungu* na mapigo ya moyo nayo yalianza kwenda mbio kwa kasi kubwa.
Kwasababu kila nilivyokuwa nazunguka naona maghorofa yanafanana urefu, upana, rangi, mitaa yenyewe inafanana urefu, upana muonekano, yaani kilichopo kwenye mtaa huu, ndicho kilichopo mtaa ule.
Kingine nilikuwa sioni watu wengi kupishana nao, yaani inaweza kuchukuwa hata dakika 5-6-7 niko pekeyangu dah!!!!
Kwahiyo nikawa najiona nipo palepale kila ninavyozunguka, haliyakuwa kumbe nimesharuka mitaa kadhaa tangu nilipoanza kuzunguka.
Nikitazama muda.. unazidi kuyoyoma,
hali ya hewa nayo nikawa siielewi nikawa najiuliza kimoyomoyo...mvua inataka kunyesha nini?
Baadae nikaonana na madereva taxi...
Nikawasalimia kisha nikawataka wanisaidie kunikutanisha na mtanzania yeyote au mahala wanakopatikana.
Bilashaka walikuwa ni wacongo au Nigeria wale madereva taxi.
Nilipowauliza walinijibu kuwa hawajui walipo, na mmoja akaongeza kwa kusema...alafu leo ni jumapili huwa hakunaga watu kabbisa mdogowangu.
Nikaachana nao nikazidi kupagawa na kujihisi kanakwamba nimeonewa na dunia.
Katika kuzungukazunguka nikamuona jamaa mmoja iv' nikamsimamisha,
nikampa Hi, kisha nikampasulia live,
nikamwambia ya uongo na kweli...
Jamaa akanisikilizaaaaa,
Kisha akaniambia...basi tuzunguke zunguke ili tuwapate jamii yako!!
Nikamjibu saws.....
Moyoni mwangu nikasema...
Mimi na wewe leo......pumbavvv.
Basi....tukazungukaaa, baadae tukakutana na sijui rafiki yake au dugu yake I don't know....
Wakaanza kuongea kifaransa, na hata kuniuliza km ninajua kuzungumza kifaransa, nikawajibu...hapana mimi sikijui kabbisa kifaransa.
Basi....tukaachana na yule jamaa yake na kusonga mbele.
Punde...tulifika sehemu moja iv'
Na kunitaka nimsubiri hapo kwa muda wa dakika kadhaa.
Jee' unajua nini kilifuata hapo???
Kumbuka muda umeshakwenda...
Alafu ni siku ya weekend,
Mimi mgeni.
Gonga likes nyingi
then tukutane #part5
By: Tooth Brush
#$$$
Hahaha,Mkuu nilikua mwaka gani? Mimi nilizamia 2009 hadi 2010. Jo'burg Na Capetown..
Nimeuza hadi ngadaa
Baadhi walithubutu kufanya hivyoWASANII WETU WALIVYO BONGO LALA HAWAONI FURSA HAPA.WANGESHAONGEA NA HUYU JAMAA KUHUSU KUTENGENEZA MOVIE MOJA KALI SANA.WAMEAKALIA KUZUNGUKA MITAANI KUTUPIGA MIZINGA TU AU KUHUBIRI UZALENDO!!