Niuluze chochote kuhusu utapeli

Akili kubwa.
 
Utapeli wa Dark web unafahamu na vp card zake zinafanya kazi
Usijaribu kununua card kule na kufanyia manunuzi, 1. Zitafanya kazi ila watakudaka kama panzi. Wengi hutumia kadi hizo kununua vitu amazon mfano na unaweka address yako na namba ya simu, hapo unadakwa kenge wewe. Huo uhalifu unaovuka mipaka unashughulikiwa na interpol sio hawa wakwetu wanao fukuzana na bodaboda kila kukicha.
 
utapeli wa kutemeshwa nywele mdomoni huwa ni uchawi au ?

unamkuta babu anauliza directions kisha mwengine anatokea kukusihi mumsindikize, automatically unajikuta unawafata, huko mnakoenda unatemeshwa nywele ..

ulivuma sana miaka ya 2000
 
Kwamba ntadakwa, nataka ninunue nilipe services mfano Upwork 🤣🤣🤣
 

Kwanini tunawapa waarabu watutunzie misitu yetu? Wenyewe wanafanya dili la kuuza carbon credit kupitia misitu yetu wanatupa 10%. Kwanini tusingefanya wenyewe?
 
Tunaweza vipi kuitapeli ATC kuna mchongo lile aibus lina dili Congo....yaani bonge la dili ya kufa ntu.
Karibu
 

Rais wa Tanzania kazi yake ni nini? Utalii? Royal tour, kupiga misele?

Bunge la Tanzania kazi yake ni nini?

Kwanini hatuwezi kujenga matundu ya vyoo bila mikopo?

Kwanini maji ni tatizo nchi hii?

Majambazi, majangili, mafisadi walioko serikalini tuwafanyaje?
 
Hii ni kwa ajili ya carbon trading
Soma hapo kuhusu vitu ambavyo haviko sawa
 
Tunaweza vipi kuitapeli ATC kuna mchongo lile aibus lina dili Congo....yaani bonge la dili ya kufa ntu.
Karibu
Nenda ulaya, tafuta mzungu yeyote asiye na mbele wala nyuma mlete, mvalishe suti na tai, mpe briefcase aende kukutana na waziri wa uwekezaji hapo utapewa shirika lote bure, utumie documents za shirika kukopa kwenye banki za nje halafu unaiachia serikali deni, unamlipa mzungu asepe nawewe unabaki na salio refu, ATC inabaki na deni. Chadema wanabaki na hoja ya kisiasa.
 
Mimi kama Boss la DP World sioni shida kwa wote ulio wataja maana wana roho nzuri ndomaana wamenipa bandari bure. Nawewe nenda kaombe jengo la bunge ufugie kuku.
 
Inakuaje unaambiwa ukachukue kadi ya benki ukatoe hela ukabidhi matapeli.. baada ya dakika ndio unajitambua kuwa nimeibiwa.
 
Inakuaje unaambiwa ukachukue kadi ya benki ukatoe hela ukabidhi matapeli.. baada ya dakika ndio unajitambua kuwa nimeibiwa.
Hiyo dawa inafanya kazi kwa mtu aliye kula/kuliwa ndani ya siku 7 kama wewe sio mzinzi huwezi ibiwa kwa dawa hii.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…